Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Tuesday, June 13, 2017

WAZIRI MKUU AHIMIZA HAKI NA USAWA MAGEREZA

Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ahimiza haki na usawa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Tazama video hapo chini




Video kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu

Monday, June 12, 2017

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAVISHA VYEO MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA KWA NIABA YA RAIS, AHIMIZA HAKI NA USAWA MAGEREZANI

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa salaam ya heshima kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alipowasili kwenye hafla ya  kuwavalisha Vyeo Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa gwaride maalum katika hafla fupi ya kuwavalisha Vyeo Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika hafla fupi ya kuwavalisha Vyeo Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  hafla hiyo .
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Joel Bukuku kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Maafisa wandamizi wa Jeshi la Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu, Mhe. Kasim Majaliwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni aweze kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa ili aweze kuongea machache kwenye hala hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akitoa neno kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla fupi ya kuvalisha vyeo Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo na Mhe. Rais Magufuli akifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu.
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka maeneo ya jirani na Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam wakifuatilia tukio hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa magereza aliowavalisha Vyeo kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 12, 2017. Walioketi(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni 
(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wote wa Jeshi la Magereza nchini kuendelea  kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao wa kila siku.

Ametoa wito huo leo jioni (Jumatatu, Juni 12, 2017) wakati akizungumza na maafisa na makamanda wa jeshi hilo katika hafla ya kuwavisha vyeo maafisa waandamizi wa magereza 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye amefanya kazi hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa waandamizi wa magereza watano kuwa Manaibu Kamishna wa Magereza (DCP) na maafisa waandamizi wa magereza 24 kuwa Makamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP). Maaafisa hao walipandishwa vyeo na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mei 25, mwaka huu.

“Ninyi ni viongozi wakuu katika mikoa mnayotoka. Huko kuna makamanda walio chini yenu na jamii inayowazunguka. Endeleeni kuwahudumiana na kulitumikia Taifa hili kwa weledi mkubwa. Endeleeni kusimamia usawa na haki katika kazi zenu za kila siku,” amesema.

Waziri Mkuu amesema hana shaka na utendaji kazi wa jeshi la Magereza kwani watumishi wake ni waadilifu. “Jeshi hili linayo nidhamu ya hali ya juu, mbali ya jukumu lenu la ulinzi, mnafanya kazi nidhamu, weledi na uadilifu mkubwa,” amesema.

Amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kila siku na kwamba inajitahidi kuzishughulikia hasa baada ya kukamilisha zoezi la kuondoa watumishi hewa.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia maafisa hao, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Yusuph Masauni amewataka maafisa waliovishwa vyeo hivyo wazingatie maadili ya kazi zao na uzalendo kama ambavyo wameapa kwenye kiapo cha maadili.

Maafisa Waandamizi watano waliovalishwa vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni SACP Uwesu Ngarama; SACP Gideon Mkana (Mkuu wa Chuo cha TCTA); SACP Jeremiah Nkondo (RPO-Kagera); SACP Tusekile Mwaisabila (RPO-Lindi) na SACP Augustine Mboje (RPO-DSM).

Maafisa Waandamizi  24 waliovalishwa vyeo kuwa Makamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP) ni ACP Mbaraka Semwanza; ACP George Mwambashi; ACP Charles Novati; ACP Faustine M. Kasike; ACP Joel Bukuku; ACP Deogratius Lwanga; ACP Boyd P. Mwambingu (RPO Pwani); ACP Athumani Kitiku (RPO Mwanza) na ACP Hassan Mkwiche (RPO Kilimanjaro).

Wengine ni ACP Luhende D. Makwaia; ACP Hamza R. Hamza; ACP Jeremiah Y. Katengu; ACP Mzee R. Nyamka (Kaimu RPO Morogoro); ACP Afwilile Mwakijungu (Mkuu wa gereza la Isupilo, Iringa); ACP Ali Kaherewa (Kaimu RPO Singida); ACP Ismail Mlawa (RPO Mtwara); ACP Chacha B. Jackson; ACP Rajab N. Bakari; ACP Kijida P. Mwankingi; ACP Julius C. Ntambala; ACP Mussa M. Kiswaka; ACP Justin Kaziulaya na ACP Bertha J. Minde.

Sunday, June 11, 2017

MKUTANO WA WAKUU WA MAGEREZA /TAASISI ZA UREKEBISHAJI ZA NCHI ZA SADC WAFANYIKA JIJINI DAR

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni(wa pili toka kulia) akiwaongoza kuimba wimbo wa Taifa la Tanzania Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika - SADC – Corrections/Prisons Sub Committee(hawapo pichani). Wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, (wa kwanza kutoka kushoto) ni Mjumbe wa Sekretarieti ya SADC, Bw. Maemo Machete. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika - SADC – Corrections/Prisons Sub Committee akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni kufungua rasmi mkutano huo wa siku moja.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika - SADC – Corrections/Prisons Sub Committee uliofanyika leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano huo toka nchi za SADC wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga.
Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika - SADC – Corrections/Prisons Sub Committee ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao hicho kama inavyoonekana katika picha.
Wajumbe wa Mkutano huo toka nchi za SADC wakifuatilia majadiliano kama wanavyoonekana katika picha(katikati) ni Mkuu wa Magereza nchini Botswana, Silas Motlalekgosi.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo akiteta jambo na Mjumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC, Bw. Maemo Machete.
Wajumbe wa kutoka Jeshi la Magereza Tanzania wakipitia baadhi ya nyaraka mbalimbali za Mkutano huo(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani, SACP. Boyd Mwambigu(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP. Mzee Ramadhan Nyamka(kushoto) ni SACP. Justine Kaziulaya.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Magereza toka nchi za SADC. Wa tatu toka kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Magereza toka nchi za SADC. Wa tatu toka kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa

(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza).

Tuesday, June 6, 2017

RAIS MAGUFULI AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA MAGEREZA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Simu: +255-22-2112035/40
Nukushi: +255-2122617/2120486
Baruapepe: ps@moha.go.tz
9 Barabaraya Ohio
S.L.P. 9223
11483 DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa watano wa Magereza kuwa Naibu Makamishna na wengine 24 kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza kuanzia tarehe 25 mwezi Mei, 2017.

Waliopandishwa vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Uwesu H. Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon M. D. Nkana, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Jeremiah .M.C. Nkondo, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Tusekile S. Mwaisabila, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Augustine S. Mboje ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam.

Waliopandishwa vyeo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Mbaraka Sultan Semwanza, Mwalimu wa Hisabati na Kemia shule ya Sekondari Bwawani inayosimamiwa na Jeshi Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza George Togholai Mwambashi, Mkuu wa Kitengo cha Sheria Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Charles R. Novat, Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Faustine Martin Kasike Mkufunzi Mwandamizi Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Kunduchi Dar es Salaam.

Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Joel Silverster Bukuku, Mdhibiti wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Deogratius Ndaboine Lwanga, Afisa Mnadhimu, Magereza Makao Makuu Ukonga, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Boyd Patric Mwambingu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Magereza Athuman Ambayuu Kitiku, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Hassan Bakari Mkwiche, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Magereza Luhende DAVID Makwaia, Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi na Msaidizi wa Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza Hamza Rajab Hamza, Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Tabora na Kamishna Msaidizi wa Magereza Jeremiah Yoram Katungu, Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Dar es Salaam.

Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Mzee Ramadhan Nyamka, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Gereza Isupilo Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Magereza Ally Abdallah S. Kaherewa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Magereza Salum Omar Hassan, Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Magereza Ismail T. Mlawa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza Chacha Bina Jackson, Mdhibiti wa Fedha Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam na Kamishna Msaidizi wa Magereza Rajab Nyange Bakari, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Ghasia Magereza Ukonga Dar es Salaam.

Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Kijida Paul Mwankingi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza Julius Cosmas Ntambala, Msimamizi Mkuu wa Ujenzi wa Nyumba 320 za Kuishi Askari Gereza la Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza Mussa Musuluzya Kaswaka, Afisa Mkaguzi Makao Makuu Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Justine M. Kaziulaya, Mratibu Msaidizi Baraza la Usalama la Taifa na Kamishna Msaidizi wa Magereza Bertha Joseph Minde ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara.

Imetolewa na
Meja Jenerali Projest Rwegasira
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
6 Juni 2017