Banner

Banner

Thursday, March 11, 2021

WAFUNGWA, MAHABUSU KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA ILIYOBORESHWA (CHF).


 DODOMA. Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleimani Mzee Leo Tarehe 11 Machi 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Francis Lutalala, ambaye ni Mratibu wa Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF) Jijini Dodoma kwa lengo la kuona  uwezekano wa  kuboresha afya ya Watumishi wa Jeshi hilo pamoja na Wafungwa na Mahabusu waliopo Magerezani.


Jenerali Mzee amesema kuwa amefurahishwa na ujio wa Dkt. Lutalala, kwakuwa umetoa mwangaza kuelekea mpango wa kupunguza gharama za matibabu kwa Wafungwa kutokana na bima hiyo kuchukua watu Sita kwa gharama nafuu ya Shilingi Elfu 30 kwa mwaka, huku akiweka wazi nia yake ya kujenga Hospitali kubwa katika eneo la Msalato yalipo Makao Makuu ya Jeshi Hilo.

''Niseme tu nimefurahishwa na ujio wako, hii bima nimekubaliana nayo na Nina mpango wakujenga hospitali kubwa kwahiyo ninaimani Mambo yataenda vizuri na tutaboresha zaidi Afya za watu wetu"

Kwaupande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Gereza Msalato Dkt. Mpamba Juma amesema, wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wananchi wa maeneo ya jirani pamoja na Wafungwa kwa kushirikiana na CHF.

''Sisi tumejipanga vizuri Sana katika kutoa huduma, hivyo kuja kwa CHF kutapelekea huduma kuwa Bora zaidi kwakuwa wanachi wengi Sasa wenye bima hii wataanza kuja katika Zahanati yetu'' alisema Mpamba.

Akizungumzia mafanikio ya ujio wake Dkt. Lutalala mratibu wa CHF amesema, anashukuru kukutana na Jenerali Mzee na kufanya nae mazungumzo chanya, ambapo amemueleza namna walivyo itangaza Zahanati ya Gereza Msalato na Mafanikio yanayoanza kuonekana kwa muda mfupi, huku akiahidi kulichukua wazo la kujenga Hospitali kubwa zaidi na kulifikisha kwa Mkuu wa Mkoa ili kupata msaada zaidi.

Monday, February 22, 2021

MKURUGENZI MKUU WA TBC DR. RYOBA AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Dkt Ayubu
Rioba, leo tarehe 22,February,2021 amefanya ziara katika Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza yaliyoko Msalato Jijini Dodoma.
Akizungunza muda mfupi baada ya kuwasili ofisini hapo Rioba amesema,
madhumuni ya ziara hiyo ni kujifunza namna  Jeshi la Magereza
limefanikiwa kujenga Makao yake Makuu kwa muda mfupi na kwa gharama
nafuu huku akisisitiza kuwa kilichofanywa na Jeshi hilo kinafaa
kuigwa.
‘‘ Hakika ziara yangu hii katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
imenifanya kujifunza na kunipa mwanga zaidi wa namna ya kujipanga
kwani hata sisi TBC tunao mpango  wa kujenga ofisi zetu za shirika
hapa Dodoma. Pia nashauri taasisi nyingine hazina budi kuja kujifunza
mahali hapa.’’ Amesema mkurugenzi huyo.
Awali akimpokea mkurugenzi mkuu wa TBC kwa niaba ya Kamishna Jenerali
wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza  Jeremiah Katungu amesema kuwa
amefurahi kwa ujio wake hivyo awe huru kujifunza na kuuliza pale
anapohitaji ufafanuzi.
Aidha Naibu Kamishna wa Magereza  Jeremiah Katungu Katungu amesema,
mafanikio ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza yametokana na
mpango kabambe wa Kamishna Jenerali wa Magereza Meja Jenerali Suleiman
Mzee.
‘‘Kimsingi tunamshukuru Kamishna Jenerali wa Magereza kwa juhudi
alizozionyesha mpaka kufanikisha ujenzi wa ofisi hizi kwa muda
mfupi.’’
Pia Katungu amesema kuwa rasilimali zilizotumika kukamilisha ujenzi
huu ni za ndani tu kwani waliotumika ni maafisa na askari pamoja na
wafungwa.
Aidha amesema kuwa ujenzi huo ulianza mwezi wa tano mwaka jana hadi
kufikia mwezi Disemba mwaka jana ulikuwa umekamilika kwa kiasi kikubwa
na gharama ya ujenzi huo uligharimi kiasi cha milioni 900 taslimu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika l Utangazaji Tanzania (TBC)Dr.
Riyoba akiangalia akiangalia eneo la Makao Makuu Ya Magereza alipo
fanya ziara yake akiongozana na Naibu Kamishna Wa magereza Jeremia
Katungu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Justine Kaziulaya na
Mandarasi wa mradi wa jengo La Makao Makuu ya Jeshi Mkaguzi wa
Magereza Belela
 
Mkurugenzi  mkuu wa Shirika la utangazaji Tbc Dr. Rioba
akiangalia Ramani ja majengo ya makao makuu ya jeshi la Magereza alipo
tembelea makao makuu hayo
 

                           Mkurugenzi wa TBC akiangalia Bustani ya maua ya Makao makuu ya
                                                                       Jeshi la Magereza

 

Mkurugrenzi Kuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC Dr. Rioba
akiangalia baadhi ya ofisi akiongozana na Naibu kamishna wa Jeshi la
Magereza Jeremiah  Katungu.