Tuesday, February 5, 2019
WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH. KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA MAGEREZA KATIKA WIKI YA SHERIA JIJINI DODOMA TAR. 02 FEB,2019
10:01 AM
Waziri
Mkuu wa Tanzania Mh. Khasim Majaliwa akihutubia katika ufunguzi wa wiki ya
Elimu ya Sheria ambapo kitaifa yanaendelea kufanyika Jijini Dodoma, kaulimbiu ni utoaji haki ni
jukumu la mahakama na wadau.
Waziri
Mkuu wa Tanzania Mh. Khasim Majaliwa akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh.Profesa Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Tanzania
, Mh. Tulia Akson Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.B. Mahenge Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika
matembezi ya ufunguzi wa wiki ya Sheria yaliofanyika
asubuhi ya tarehe 02 Feb, 2019 Jijini Dodoma ambapo yalianzia katika viwanja
vya Mahakama Kuu na kuishia katika viwanja vya Nyerere Squire.
Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu ya Magereza
, Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma na Gereza Kuu Isanga wakiwa katika matembezi ya wiki ya elimu ya
sheria jijini Dodoma kutoka kushoto ni
Kamishna wa Magereza anayesimamia Fedha
na Mipango (CP) Gideon Nkana , Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Salum
Hussein, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Rajabu Nyange,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza(SACP) Mzee Ramadhan Nyamka, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi (SACP) Chacha Jackson Bina, Mkuu wa Gereza Kuu Isanga Kamishna Msaidizi wa
Magereza(ACP) Keneth Mwambije.
Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini Mrakibu wa Magereza (SP)
Amina Kavirondo akimpa ufafanuzi Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Khasim Majaliwa kuhusu masuala ya
haki na ulinzi wa watoto walioko Magerezani kutokana na Mama zao kukinzana na
sharia.
Baadhi ya Maafisa na askari wa jeshi la Magereza
wakishiriki katika matembezi ya maadhimisho ya wiki ya sheria Dodoma.( picha na
Cpl Mfaume Ally- Jeshi la Magereza)
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA KUU LA WANAWAKE TANZANIA - KINGOLWIRA, MOROGORO
9:21 AM
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa
Gereza Kuu la Wanawake Tanzania - Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe alipotembelea alipotembelea
Gereza hilo jana februari 4, 2019 katika ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro
Mkuu
wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe akitoa
taarifa fupi ya uendeshaji wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania – Kingolwira kwa
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto meza kuu) jana
februari 4, 2019 alipotembelea Gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike(katikati) akikagua maeneo mbalimbali ya Gereza Kuu la Wananwake(kulia)
ni Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe.
Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Udereva cha Magereza – Kingolwira, ACP. Lazaro
Nyanga.
Askari wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira wakiwa
timamu kazini wakati Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani)
akizungumza na Wafungwa wa Gereza hilo jana februari 4, 2019 alipotembelea
Gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini,
Phaustine Kasike(kulia) akiangalia mradi wa kuku wa mayai katika Gereza Kuu la
Wanawake Tanzania – Kingolwira alipotembelea jana februari 4, 2019.
Ujenzi
wa nyumba kwa njia ya ubunifu katika Kambi mojawapo ya Gereza Mtego wa Simba,
Morogoro ukiendelea katika hatua awali za ujenzi.
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Phaustine Kasike akiangalia mashine kufunga majani ya malisho ya mifugo
katika mradi wa ng’ombe wa maziwa Gereza Mtego wa Simba.
Mkuu wa Chuo cha Udereva cha Magereza – Kingolwira,
ACP. Lazaro Nyanga akimuongoza Kamishna Jenerali
wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) kukagua majenego mbalimbali
yanayokarabatiwa katika chuo hicho kwa kutumia ubunifu (Picha na Jeshi la
Magereza).