Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Wednesday, August 7, 2019

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE AWAVISHA VYEO MAAFISA MAGEREZA WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA PWANI WALIOPANDISHWA VYEO HIVI KARIBUNI

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akimvalisha cheo   Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Lipina Lyimo kuwa Kamishina Msaidizi  wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akimvalisha cheo  Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Merkiory Komba kuwa Mrakibu wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2019. Mrakibu wa Magereza, Merkiory Komba ni Msaidizi wa Mkuu wa Jeshi hilo.
Baadhi ya Maafisa waliopandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali wakiwa timamu kabla ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike kuwasili kwa zoezi la uvishaji vyeo , jana Agosti 6, 2019 kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akikagua Gwaride maalum  kabla ya zoezi la uvishaji vyeo kwa Maafisa wa Mkoa wa Dr es Salaam na Mkoa wa Pwani  waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni.
Gwaride maalum likipita kwa mwendo wa pole mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) kwenye hafla ya uvishaji vyeo kwa maafisa wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani jana Agosti 6, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa ngazi mbalimbali wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo (waliosimama)baada ya hafla uvishaji vyeo iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2018(Picha zote na Jeshi la Magereza).