Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Thursday, November 20, 2014

Uzalishaji wa mifugo katika mashamba ya Jeshi la Magereza waongezeka kwa mafanikio makubwa nchini

Sehemu ya Wanyama kazi katika Shamba Kubwa la Uzalishaji wa ngo'mbe wa nyama katika Gereza Ubena lililopo Mkoani Pwani. Shamba hilo lina takribani jumla ya ngo'mbe zaidi ya 1500. Uzalishaji wa ngo'mbe umekuwa ukiongezeka kwa mafanikio makubwa kila Mwaka hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Uongozi wa Jeshi la Magereza katika kuyahudumia mashamba hayo Nchini.
Lango Kuu la kuingilia Gereza la Mifugo Ubena lililopo Mkoani Pwani ambalo linashughulika zaidi na Uzalishaji wa Mifugo. Wafungwa katika Gereza hilo wanapata elimu ya Ufugaji bora unaozingatia Kanuni za Ufugaji wa Kisasa ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa jukumu la Urekebishaji kwa Wafungwa.
Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Uzalishaji wa Mifugo Gereza la Mifugo Ubena, Mkoani Pwani.
Kundi la ngo'mbe wa maziwa katika Shamba la Mifugo la Mtego wa Simba lililopo Mkoani Morogoro. Shamba hili la Mifugo ni Maalum kwa Uzalishaji wa Ngo'mbe wa maziwa kama inavyoonekana katika picha na Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1944.
Maziwa yakiwa tayari yamekamliwa na kuhifadhiwa kwenye majokovu kabla ya kwenda kwa walaji. Shamba hilo la Uzalishaji ngo'mbe wa maziwa la Gereza Mtego wa Simba limekuwa likipigiwa mfano hapa nchini

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Monday, November 17, 2014

Twiga Cement yamwaga msaada wa vifaa vya ujenzi kwa Jeshi la Magereza katika mradi wa ujenzi wa makazi ya askari gereza wazo jijini Dar es Salaam

 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alphonso Rodrudges(suti ya bluu) akikabidhi mfano wa hundi yenye kiasi cha Tsh. Millioni Miamoja kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza zitakazotumika katika ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni (wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja, (wa kwanza kushoto) ni mtaalam mshauri wa Twiga cement Bw. Saidi Subety. hafla hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2014 katika viwanja vya Gereza Wazo, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil hotuba yake fupi katika hafla ya kupokea vifaa vya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni, hafla hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2014 katika viwanja vya Gereza Wazo, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi katika hafla ya kupokea vifaa vya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni, hafla hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2014 katika viwanja vya Gereza Wazo, Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Vifaa vya ujenzi vilivyokabidhi leo na Kampuni ya Twiga Cement. Kampuni hiyo imekabidhi mifuko 1200 ya saruji pamoja na fedha Tsh. Millioni Miamoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(kushoto) akikata utepe kabla ya kukabidhiwa rasmi vifaa vya ujenzi pamoja na hundi yenye kiasi cha Tsh. Millioni Miamoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza mara  baada ya kukabidhiwa rasmi vifaa vya ujenzi pamoja na hundi yenye kiasi cha Tsh. Millioni Miamoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni(wa tatu toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Magereza Huduma za Urekebishaji, Injinia. Deonice Chamulesile(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa (wa tatu kushoto) ni  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alphonso Rodrudges, (wa pili kulia) ni Mtaalam Mshauri wa Twiga Cement Bw. Saidi Subety.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Friday, November 14, 2014

Taarifa kwa vyombo vya habari

Tarehe 17 Novemba, 2014 saa 4:00 asubuhi Jeshi la Magereza litapokea msaada wa vifaa vya ujenzi na vitendea kazi vitakavyotumika katika ujenzi wa makazi ya Maafisa na Askari wa Gereza Wazo. Tukio ambalo litafanyika katika Viwanja vya Gereza Wazo, Wilayani Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini msaada huo umetolewa na Kampuni ya Twiga Cement ya Jijini Dar es Salaam kufuatia kusainiwa kwa Makubaliano ya kuiuzia Kampuni hiyo madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo.

Mgeni rasmi katika tukio hilo atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias M. Chikawe(Mb). Aidha, Wadau mbalimbali toka nje ya Jeshi la Magereza watakuwepo katika hafla hiyo.

Kuanza kwa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo utapunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa Nyumba zenye hadhi kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Gereza hilo.


Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye shughuli hiyo katika muda ulioelezwa.


Imetolewa na;
Lucas A. Mboje, Mkaguzi wa Magereza;
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza;
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza;
DAR ES SALAAM.
14 Novemba, 2014.

Thursday, November 6, 2014

Wadau mbalimbali wampongeza Kamishna Jenerali wa Magereza kwa kufanikisha kuandaa rasimu ya sera ya Taifa ya Magereza

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi katika ufunguzi wa  Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.

Na Lucas Mboje; Bagamoyo

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja amepongezwa na Wadau mbalimbali nchini kwa kufanikisha kuandaa na kukamilisha rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza ambapo Wadau kutoka nje ya Jeshi la Magereza wamepata fursa ya kujadili kwa siku mbili Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani.

Pongezi hizo wamezitoa kwa nyakati tofauti mjini Bagamoyo katika Mkutano wa siku mbili wa Wadau wa kupokea maoni juu ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza uliofunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw.  Mbarak Abdulawakil Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.

"Tunampongeza sana Kamishna Jenerali Minja hususani kwa kufanikisha rasimu hiyo na tunaamini kutokana na kasi yake ya Utendaji wa kazi rasimu hiyo itawasilishwa mapema Serikali kwa hatua za mwisho," Walisikika wakisema.

Aidha, wameongeza kuwa kukamilika kwa Sera ya Taifa ya Magereza kutaleta ufanisi katika utendaji na uboreshaji huduma mbalimbali zitolewazo ndani ya Jeshi la hilo.

Awali akitoa maelezo mafupi katika ufunguzi wa Mkutano huo wa Wadau wa kupokea maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja alisema kuwa chimbuko la kuwa na Sera hiyo ni kubadili utaratibu wa kuwafunga wahalifu magerezani ambao ulianza wakati wa Ukoloni na ulilenga zaidi kuwakomoa na kuwaadabisha.

Jenerali Minja aliongeza kuwa utaratibu huo ulilenga kuwaweka wahalifu kwenye Ulinzi mkali na kuwafanyisha kazi ngumu zisizo na tija nazisizozingatia haki za Binadamu.

Alisema kuwa baada ya Uhuru mwaka 1961, Falsafa ya Magereza ilibadilika  kutoka ile ya kukomoa na kuwaadabisha wahalifu na kuwa Urekebishaji na kuzingatia haki za Binadamu.

"Mabadiliko ya kifalsafa pamoja na kuridhiwa kwa Mikataba mbalimbali ya Kimataifa yanatulazimu kuwa na Sera ambayo ndiyo itakuwa dira ya Utekelezaji wa shughuli za kila siku za Jeshi la Magereza," alisema Jenerali Minja.

Aidha Jenerali Minja, aliongeza kuwa sera hiyo inalenga pia kubadili mitizamo ya jamii kuwa magereza ni mahali pa mateso. "Tunataka Magereza ya sasa ionekane ni chuo cha kubadili tabia za wafungwa ili wamalizapo vifungo vyao wawe ni raia wema katika jamii."

Jeshi la Magereza kupitia Wataalam wake limeandaa Rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Haji Semboja ambapo tayari wadau wote wa ndani na nje ya Jeshi la Magereza wamepata fursa ya kuchangia maoni yao kikamilifu tayari kuwasilishwa rasmi Serikalini kwa hatua za mwisho.

Mkutano wa wadau wa kupokea maoni juu ya sera ya Taifa ya Magereza wamalizika Wilayani Bagamoyo

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw.  Mbarak Abdulawakil akitoa hotuba ya Ufungaji wa Mkutano wa Wadau uliohusu upokeaji wa maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza. Mkutano huo wa siku mbili umefanyikia katika Hoteli ya Livingstone Bagamoyo ambapo wadau wamepitia rasimu hiyo na kutoa maoni kikamilifu Novemba 05, 2014.
Wadau wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa Mkutano wa Wadau uliohusu upokeaji wa maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza Novemba 05, 2014 katika Hoteli ya Livingstone Bagamoyo .
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw.  Mbarak Abdulawakil kutoa hotuba ya Ufungaji wa Mkutano wa Wadau uliohusu upokeaji wa maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akipitia makabrasha wakati wa majadiliano ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza(kulia) ni Mkurugenzi Idara ya Malalamiko Wizara ya Mambo ya Ndani, Bw. A. Shio(kushoto) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw.  Mbarak Abdulawaki. 
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Deonesia Mjema akichangia maoni katika rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza kabla ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw.  Mbarak Abdulawakil kutoa hotuba ya Ufungaji wa Mkutano wa Wadau uliohusu upokeaji wa maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma malewa akitolea ufafanuzi wa Haki za Wafungwa wanazostahili kupatiwa wawapo Magerezani wakati wa majadiliano Sera ya Taifa ya Magereza Novemba 05, 2014 katika Hoteli ya Livingstone Bagamoyo(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Wednesday, November 5, 2014

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi afungua mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza katika Hoteli ya Livingstone-Bagamoyo

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil akitoa hotuba fupi ya Ufunguzi wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Wadau wakifuatilia kwa Makini Majadiliano ya maoni kuhusu  maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi katika ufunguzi wa  Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Wadau wakifuatilia kwa makini maelezo ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika Ufunguzi wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Mshauri Mwelekezi, Dkt. Haji Semboja toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyeshiriki kikamilifu kuandaa Rasmu ya Sera ya Taifa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Wataalam wa Jeshi la Magereza akiwasilisha rasimu hiyo leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo kabla ya kuanza majadiliano.
Inspeketa Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema(kulia) akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari kutoka Vyombo vya ITV na Channel Ten leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(wa pili kulia) akiteta jambo na Inspeketa Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema(kulia) baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza(kulia) akimuongoza  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(kushoto) alipowasili kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza.
Inspeketa Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema(wa kwanza kushoto) akifuatilia kwa Makini Majadiliano ya maoni kuhusu  maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo. Wengine kulia ni Viongozi Wastafu wa Jeshio la Magereza.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawaki(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki Wadau wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.