Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Tuesday, December 18, 2018

MAGEREZA YAZINDUA MKAKATI WA KUMALIZA UHABA WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JESHI HILO, DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiwasili katika viwanja vya gereza Kuu Isanga Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za maafisa na askari kwa njia ya kujitolea. Uzinduzi huo umefanyika Desemba 17, 2018 ikiwa ni ishara ya uzinduzi programu ya ufyatuaji na uchomaji wa tofali kitaifa ili kukabiliana na changamnto ya makazi kwa watumishi wa Jeshi la Magereza kote nchini.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa miradi ya ufyatuaji matofali za kuchoma na hydrofom kitaifa kutegemeana na hali ya udongo katika kituo husika. Zoezi la uzinduzi kitagaifa limefanyika  Desemba 16, 2018 katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, Dodoma. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Mipango,Gedeon Nkana, Kamishna wa Miundombinu ya Magerezana Uzalishaji, Tusekile Mwaisabila na Mkuu wa Gereza Isanga ACP Keneth Mwambije. Kushoto ni Kamishna wa Huduma za Urekiebishaji Augostine Mboje na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Omary Salum.

Mtaalam na msimamizi wa mradi wa ufyatuaji tofali katika Gereza Kuu Isanga Dodoma Sajin Modern Mwakialinga wa Gereza Isanga akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali wa Jeshi la Magereza  juu ya namna mradi huo unavyotekelezwa.

Baadhi ya wafungwa waliopo katika programu za urekebishaji ambao wanafundishwa kufyatua, kuchoma tofali na wengine kujenga nyumba wanaotumika katika mradi wa ujenzi wa nyumba za kujitolea katika Gereza Kuu Isanga mkoani Dodoma wakionesha umahiri wao wa kufyatua tofali  Desemba 17, 2018.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi la magereza nchini.

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiangalia ubora wa tofali  za kuchoma alipofanya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za maafisa na askari wa Jeshi hilo ili kukabiliana na tatizo la makazi kwa watumishi.
Muonekano wa sehemu ya tofali 100,000 moja zilizofyatuliwa na kuchomwa tayari kwa ujenzi wa nyumba 30 za maafisa na askari wa Gereza Kuu Isanga na Ofisi ya Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Dodoma.Nyumba hizo zitakuwa na vyumba vitatu kila moja na mambo mengine muhimu kama sebule, choo, bafu, jiko na store na zinatarajiwa kukamilika kwa mwaka 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna, Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Mikoa ya kiutawala ya Magereza waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi hilo. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga Dodoma Desemba 17, 2018.Katika hafla hiyo Kamishna Kasike amewataka Wakuu wa Magereza wa Mikoa yote nchini kwa wale ambao hawajaanza utekelezaji wa agizo la ufyatuaji tofali kuanza mara moja kwa kuzingatia hali ya udongo katika maeneo yao. Jeshi la Magereza linaupungufu wa nyumba za watumishi zaidi ya 9000 kote nchini.Picha zote na Jeshi la Magereza)

MAGEREZA SACCOS YATAO MAFUNZO KWA MAAFISA WAANDAMISHI WA JESHI LA MAGEREZA TAREHE 16 DEC,2018

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike ambaye pia ni mlezi wa Magereza Saccos akisalimiana na Makamishna wa Magereza  mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Mipango Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi  kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika Desemba 16, 2018.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimpokea Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) alipowasili katika ukumbi wa  mikutano katika chuo cha mipango Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi  kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika  Desemba 16, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) akiwa meza kuu na Makamishna wa Magereza pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos  Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza ambaye hivi karibuni aliteuliwa kushika wadhifa huo akitokea Jeshi la Magereza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos  Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Zemwanza akitoa mada katika ya mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi  kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika  Desemba 16, 2018.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Ramadhan Nyamka  akichangia hoja katika  ya mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi  kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika Desemba 16, 2018.

Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Hasseid Mkwanda  akichangia hoja katika  ya mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi  kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika Desemba 16, 2018.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi  kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika  Desemba 16, 2018.(Picha zote na Jeshi la Magereza)

Friday, December 7, 2018

JESHI LA MAGEREZA LAFANYA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA DAWATI LA JINSIA JIJINI DAR TAREHE 6 DEC, 2018

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa hotuba  katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo kutoka  Magereza yote nchini leo Desemba 06, 2018  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika  Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es salaam.
Mwenyekiti  wa Taifa wa Dawati la Jinsia katika Jeshi la Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila akichangia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo kutoka  Magereza yote nchini  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza yatakayofanyika  Desemba  07, 2018.
Meneja Huduma na Mikopo Binafsi kutoka Benki ya NMB Bw. Emmanuel Mahodaga akitoa mada kuhusu huduma za NMB hasa kwa watumishi wa Umma. NMB ni mmoja wa wadhamini wa shughuli za Uzinduzi wa Dawati la jinsia katika Jeshi la Magereza unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 07 Desemba, 2018 katika viwanja vya Karimjee, Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi. Tike Mwambipile akichangia mada katika mafunzo  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo wa Magereza yote nchini  yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Bwalo Kuu la Magereza ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia  mafunzo  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo kutoka  Magereza yote nchini yanayofanyika katika Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi hilo. Uzinduzi huo utafanyika Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es salaam.

Baadhi ya askari  ambao ni Waratibu na Watendaji  wa Dawati kutoka  Magereza mbalimbali nchini wakifuatilia  mafunzo  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam  Desemba 06, 2018  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza  utakaofanyika Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es salaam.
Mtoa Mada kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Mapunda  John ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati la Jinsia kutoka  Magereza yote nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa kike kutoka magereza mabalimbali hapa nchini ambao ni waratibu wa Dawati la Jinsia waliohudhuria mafunzo kuhusu Dawati la Jinsia yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam.

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza waliohudhuria mafunzo kuhusu Dawati la Jinsia yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam.
Baadhi ya watoa mada na wafadhili  wakiwa katika picha ya pamoja na  Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo kutoka magereza yote nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Pwani ACP Rehema Songelaeli,  Mratibu wa Dawati la Jinsia Makao Makuu ya Magereza SACP Betha Minde na Mwenyekiti waTaifa wa Dawati la Jinsia ndani ya Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila. Kulia ni Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Morogoro ACP Elizaberth Mbezi, Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi ACP Josephine Semwenda na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam SACP Julius Ntambala. (Picha zote na Jeshi la Magereza)

Tuesday, December 4, 2018

CGP KASIKE AFUNGUA MKUTANO WA WANGANGA WAKUU WA VITUO VYA AFYA VYA MAGEREZA NCHINI LEO DESEMBA 4, 2018.


Na ASP Deodatus Kazinja, Dodoma.

Wataalam wa  afya wa vituo vya magereza nchini wameaswa kufanya kazi kwa weledi na juhudi kubwa ili kutimiza malengo yanayotarajiwa na jeshi la magereza na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya Jeshi la Magereza uliofanyika katika Ukumbi wa Morena Hoteli leo jijini Dodoma.

Aidha, CGP Kasike amemuagiza Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza kufuatilia kwa ukaribu utendaji wa kituo kimoja kimoja na kuhakikisha wataalam waliopo jeshini wanafanya kazi zao kwa uweledi ikiwa ndiyo matarajio ya jeshi.

Wakati huo huo CGP amewatolea wito wataalam hao wa afya magerezani kuhakikisha wanatekeleza muongozo wa serikali unaoagiza kuwaanzishia dawa watu wote wanaogundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kuhakikisha wanakuwa na ufuasi mzuri wa dawa.

Waganga wakuu wa vituo vya afya katika Jeshi la magereza wapo katika mkutano huo  unaofadhiliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  ukiwa na lengo la kufanya tathmini ya mwenendo wa Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.

Asasi ya JSI AIDS Free chini ya serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani na Wziara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa miaka minne sasa imekuwa ikishirikia na Jeshi la Magereza katika kuboresha Huduma za Afya hasa mapambano ya Ukimwi.
Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike akisalimiana na baadhi ya wajumbe na viongozi wa Asasi ya kiraia ya JSI AIDS Free mara alipowasili leo Desemba 4, 2018  katika viwanja vya Morena Hotel jijini Dodoma kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha siku moja cha kutathmini ya mwenendo  wa  Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.
Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike akitoa hotuba katika mkutano wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza yote nchini kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  kwa ajili ya kutathmini ya mwenendo wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18 leo Desemba 4, 2018 Morena Hoteli jijini Dodoma.  Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Omary Salum, Mtendaji Mkuu wa AIDS Free Tanzania Dkt. Deogratias Kakiziba. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza INSP Adili Kachima na wapili kulia  ni SSP Dkt. Richard Mwakina kutoka kituo cha afya chama magereza Ukonga, Dar es salaam.

Washiriki wa kikao wakifuatilia hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) katika kikao cha waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza nchini kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  kwa ajili ya ufuatiliaji wa mwenendo  wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18 kilichofanyika leo tarehe 04 Desemba, 2018 jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Gereza Kuu Butimba Mwanza ASP. Dkt.  Alex Lukuba akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi (CGP Kasike) ikiwa ni utambuzi wa kufanya vizuri kwa kituo anachokisimamia katika kusimamia masuala yahusuyo Ukimwi katika kituo chake.

Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza kote nchini na watendaji wakuu wa Asasi ya isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free ambayo ndiyo wafadhili wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya Magereza na polisi nchini. (Picha zote na Jeshi la Magereza)