Banner

Banner

Tuesday, December 18, 2018

MAGEREZA YAZINDUA MKAKATI WA KUMALIZA UHABA WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JESHI HILO, DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiwasili katika viwanja vya gereza Kuu Isanga Dodoma kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za maafisa na askari kwa njia ya kujitolea. Uzinduzi huo umefanyika Desemba 17, 2018 ikiwa ni ishara ya uzinduzi programu ya ufyatuaji na uchomaji wa tofali kitaifa ili kukabiliana na changamnto ya makazi kwa watumishi wa Jeshi la Magereza kote nchini.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa miradi ya ufyatuaji matofali za kuchoma na hydrofom kitaifa kutegemeana na hali ya udongo katika kituo husika. Zoezi la uzinduzi kitagaifa limefanyika  Desemba 16, 2018 katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, Dodoma. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Mipango,Gedeon Nkana, Kamishna wa Miundombinu ya Magerezana Uzalishaji, Tusekile Mwaisabila na Mkuu wa Gereza Isanga ACP Keneth Mwambije. Kushoto ni Kamishna wa Huduma za Urekiebishaji Augostine Mboje na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Omary Salum.

Mtaalam na msimamizi wa mradi wa ufyatuaji tofali katika Gereza Kuu Isanga Dodoma Sajin Modern Mwakialinga wa Gereza Isanga akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali wa Jeshi la Magereza  juu ya namna mradi huo unavyotekelezwa.

Baadhi ya wafungwa waliopo katika programu za urekebishaji ambao wanafundishwa kufyatua, kuchoma tofali na wengine kujenga nyumba wanaotumika katika mradi wa ujenzi wa nyumba za kujitolea katika Gereza Kuu Isanga mkoani Dodoma wakionesha umahiri wao wa kufyatua tofali  Desemba 17, 2018.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi la magereza nchini.

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiangalia ubora wa tofali  za kuchoma alipofanya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za maafisa na askari wa Jeshi hilo ili kukabiliana na tatizo la makazi kwa watumishi.
Muonekano wa sehemu ya tofali 100,000 moja zilizofyatuliwa na kuchomwa tayari kwa ujenzi wa nyumba 30 za maafisa na askari wa Gereza Kuu Isanga na Ofisi ya Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Dodoma.Nyumba hizo zitakuwa na vyumba vitatu kila moja na mambo mengine muhimu kama sebule, choo, bafu, jiko na store na zinatarajiwa kukamilika kwa mwaka 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna, Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Mikoa ya kiutawala ya Magereza waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi hilo. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga Dodoma Desemba 17, 2018.Katika hafla hiyo Kamishna Kasike amewataka Wakuu wa Magereza wa Mikoa yote nchini kwa wale ambao hawajaanza utekelezaji wa agizo la ufyatuaji tofali kuanza mara moja kwa kuzingatia hali ya udongo katika maeneo yao. Jeshi la Magereza linaupungufu wa nyumba za watumishi zaidi ya 9000 kote nchini.Picha zote na Jeshi la Magereza)