Tuesday, December 18, 2018
MAGEREZA YAZINDUA MKAKATI WA KUMALIZA UHABA WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JESHI HILO, DODOMA
11:07 AM
Kamishna Jenerali wa Magereza
Phaustine Kasike akiwasili katika viwanja vya gereza Kuu Isanga Dodoma kwa
ajili ya uzinduzi wa mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma kwa ajili ya ujenzi
wa nyumba za maafisa na askari kwa njia ya kujitolea. Uzinduzi huo umefanyika
Desemba 17, 2018 ikiwa ni ishara ya uzinduzi programu ya ufyatuaji na
uchomaji wa tofali kitaifa ili kukabiliana na changamnto ya makazi kwa
watumishi wa Jeshi la Magereza kote nchini.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akikata utepe kuashiria uzinduzi wa miradi ya ufyatuaji matofali za
kuchoma na hydrofom kitaifa kutegemeana na hali ya udongo katika kituo husika. Zoezi
la uzinduzi kitagaifa limefanyika Desemba 16, 2018 katika viwanja vya Gereza
Kuu Isanga, Dodoma. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Mipango,Gedeon Nkana, Kamishna
wa Miundombinu ya Magerezana Uzalishaji, Tusekile Mwaisabila na Mkuu wa Gereza
Isanga ACP Keneth Mwambije. Kushoto ni Kamishna wa Huduma za Urekiebishaji
Augostine Mboje na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Omary Salum.
Mtaalam
na msimamizi wa mradi wa ufyatuaji tofali katika Gereza Kuu Isanga Dodoma Sajin
Modern Mwakialinga wa Gereza Isanga akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali wa
Jeshi la Magereza juu ya namna mradi huo
unavyotekelezwa.
Baadhi ya wafungwa waliopo katika
programu za urekebishaji ambao wanafundishwa kufyatua, kuchoma tofali na
wengine kujenga nyumba wanaotumika katika mradi wa ujenzi wa nyumba za
kujitolea katika Gereza Kuu Isanga mkoani Dodoma wakionesha umahiri wao wa
kufyatua tofali Desemba 17, 2018.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi
la Magereza kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliohudhuria uzinduzi wa mradi
wa ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa
na askari wa Jeshi la magereza nchini.
Kamishna Jenerali wa Magereza
Phaustine Kasike akiangalia ubora wa tofali za kuchoma alipofanya uzinduzi wa programu ya
ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za maafisa na askari wa
Jeshi hilo ili kukabiliana na tatizo la makazi kwa watumishi.
Muonekano
wa sehemu ya tofali 100,000 moja zilizofyatuliwa na kuchomwa tayari kwa ujenzi
wa nyumba 30 za maafisa na askari wa Gereza Kuu Isanga na Ofisi ya Mkuu wa
Magereza wa Mkoa wa Dodoma.Nyumba hizo zitakuwa na vyumba vitatu kila moja na
mambo mengine muhimu kama sebule, choo, bafu, jiko na store na zinatarajiwa
kukamilika kwa mwaka 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza
Phaustine Kasike (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Makamishna, Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Mikoa ya kiutawala ya Magereza waliohudhuria
hafla ya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi
wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi hilo. Uzinduzi huo umefanyika
leo katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga Dodoma Desemba 17, 2018.Katika
hafla hiyo Kamishna Kasike amewataka Wakuu wa Magereza wa Mikoa yote nchini kwa
wale ambao hawajaanza utekelezaji wa agizo la ufyatuaji tofali kuanza mara moja
kwa kuzingatia hali ya udongo katika maeneo yao. Jeshi la Magereza linaupungufu
wa nyumba za watumishi zaidi ya 9000 kote nchini.Picha zote na Jeshi la
Magereza)
MAGEREZA SACCOS YATAO MAFUNZO KWA MAAFISA WAANDAMISHI WA JESHI LA MAGEREZA TAREHE 16 DEC,2018
10:29 AM
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike
ambaye pia ni mlezi wa Magereza Saccos akisalimiana na Makamishna wa
Magereza mara alipowasili katika viwanja
vya Chuo cha Mipango Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na
Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa
waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi
hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika Desemba 16, 2018.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimpokea Kamishna Jenerali wa
Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) alipowasili katika ukumbi wa mikutano katika chuo cha mipango Dodoma kwa
ajili ya mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha
Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na
Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika Desemba 16, 2018.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) akiwa meza kuu na Makamishna
wa Magereza pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza ambaye hivi karibuni aliteuliwa kushika
wadhifa huo akitokea Jeshi la Magereza.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Magereza Saccos Kamishna wa
Fedha na Utawala wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Zemwanza akitoa mada
katika ya mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha
Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na
Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika Desemba 16,
2018.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP)
Ramadhan Nyamka akichangia hoja
katika ya mafunzo ya Ushirika
yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa
maafisa waandamizi kutoka Makao Makuu ya
Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika
Desemba 16, 2018.
Kamishna
Msaidizi wa Magereza (ACP) Hasseid Mkwanda
akichangia hoja katika ya mafunzo
ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na Mikopo cha Magereza (Magereza
Saccos) kwa maafisa waandamizi kutoka
Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya
kiutawala yaliyofanyika Desemba 16, 2018.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo Ushirika yaliyoandaliwa na Chama cha Akiba na
Mikopo cha Magereza (Magereza Saccos) kwa maafisa waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na
Wakuu wa Magereza wa mikoa yote ya kiutawala yaliyofanyika Desemba 16, 2018.(Picha zote na Jeshi la Magereza)
Friday, December 7, 2018
JESHI LA MAGEREZA LAFANYA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA DAWATI LA JINSIA JIJINI DAR TAREHE 6 DEC, 2018
9:55 AM
Kamishna
Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa hotuba katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu
na Watendaji wa Dawati hilo kutoka Magereza yote nchini leo Desemba 06, 2018 ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la
Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika Desemba
07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Dawati la Jinsia katika Jeshi la
Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila akichangia jambo wakati wa
ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kuhusu
mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo kutoka Magereza yote nchini ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la
Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza yatakayofanyika Desemba
07, 2018.
Meneja Huduma na Mikopo Binafsi kutoka Benki ya NMB Bw. Emmanuel Mahodaga
akitoa mada kuhusu huduma za NMB hasa kwa watumishi wa Umma. NMB ni mmoja wa
wadhamini wa shughuli za Uzinduzi wa Dawati la jinsia katika Jeshi la Magereza
unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 07 Desemba, 2018 katika viwanja vya
Karimjee, Dar es salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi. Tike Mwambipile akichangia
mada katika mafunzo kuhusu mambo ya
Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji
wa Dawati hilo wa Magereza yote nchini
yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Bwalo Kuu la Magereza ikiwa ni
maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika
Desemba 07, 2018 katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya washiriki wakifuatilia mafunzo kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu
na Watendaji wa Dawati hilo kutoka Magereza yote nchini yanayofanyika katika
Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam
ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi hilo.
Uzinduzi huo utafanyika Desemba 07, 2018
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar
es salaam.
Baadhi
ya askari ambao ni Waratibu na
Watendaji wa Dawati kutoka Magereza mbalimbali nchini wakifuatilia mafunzo
kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo
Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam Desemba 06, 2018 ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la
Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika
Desemba 07, 2018 katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es salaam.
Mtoa
Mada kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.
Mapunda John ambaye ni Afisa Maendeleo
ya Jamii akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya jinsia kwa Waratibu na
Watendaji wa Dawati la Jinsia
kutoka Magereza yote nchini
yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza
Ukonga, Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike
(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari
wa kike kutoka magereza mabalimbali hapa nchini ambao ni waratibu wa Dawati la
Jinsia waliohudhuria mafunzo kuhusu Dawati la Jinsia yaliyofanyika leo Desemba
06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya
pamoja na maafisa wenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza waliohudhuria
mafunzo kuhusu Dawati la Jinsia yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika
Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam.
Baadhi
ya watoa mada na wafadhili wakiwa katika
picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa
Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo kutoka magereza yote
nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Magereza wa Mkoa
wa Pwani ACP Rehema Songelaeli, Mratibu
wa Dawati la Jinsia Makao Makuu ya Magereza SACP Betha Minde na Mwenyekiti
waTaifa wa Dawati la Jinsia ndani ya Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile
Mwaisabila. Kulia ni Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Morogoro ACP Elizaberth
Mbezi, Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi ACP Josephine Semwenda na Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Dar es Salaam SACP Julius Ntambala. (Picha zote na Jeshi la Magereza)
Tuesday, December 4, 2018
CGP KASIKE AFUNGUA MKUTANO WA WANGANGA WAKUU WA VITUO VYA AFYA VYA MAGEREZA NCHINI LEO DESEMBA 4, 2018.
7:44 PM
Na
ASP Deodatus Kazinja, Dodoma.
Wataalam
wa afya wa vituo vya magereza nchini
wameaswa kufanya kazi kwa weledi na juhudi kubwa ili kutimiza malengo
yanayotarajiwa na jeshi la magereza na taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike wakati
wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya Jeshi
la Magereza uliofanyika katika Ukumbi wa Morena Hoteli leo jijini Dodoma.
Aidha,
CGP Kasike amemuagiza Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza kufuatilia kwa ukaribu
utendaji wa kituo kimoja kimoja na kuhakikisha wataalam waliopo jeshini
wanafanya kazi zao kwa uweledi ikiwa ndiyo matarajio ya jeshi.
Wakati
huo huo CGP amewatolea wito wataalam hao wa afya magerezani kuhakikisha
wanatekeleza muongozo wa serikali unaoagiza kuwaanzishia dawa watu wote
wanaogundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kuhakikisha wanakuwa na ufuasi
mzuri wa dawa.
Waganga
wakuu wa vituo vya afya katika Jeshi la magereza wapo katika mkutano huo unaofadhiliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya
JSI AIDS Free ukiwa na lengo la kufanya
tathmini ya mwenendo wa Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo
vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.
Asasi
ya JSI AIDS Free chini ya serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Wizara ya
Mambo ya Ndani na Wziara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
kwa miaka minne sasa imekuwa ikishirikia na Jeshi la Magereza katika kuboresha Huduma
za Afya hasa mapambano ya Ukimwi.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP)
Phaustine Kasike akisalimiana na baadhi ya wajumbe na viongozi wa Asasi ya
kiraia ya JSI AIDS Free mara alipowasili leo Desemba 4, 2018 katika viwanja vya Morena Hotel jijini Dodoma
kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha siku moja cha kutathmini ya mwenendo wa Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi
katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akitoa hotuba katika
mkutano wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza yote nchini
kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free kwa ajili ya kutathmini ya mwenendo wa Mradi
Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza
kwa mwaka 2017/18 leo Desemba 4, 2018 Morena Hoteli jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma
SACP Omary Salum, Mtendaji Mkuu wa AIDS Free Tanzania Dkt. Deogratias Kakiziba.
Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza INSP Adili
Kachima na wapili kulia ni SSP Dkt.
Richard Mwakina kutoka kituo cha afya chama magereza Ukonga, Dar es salaam.
Washiriki
wa kikao wakifuatilia hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike
(hayupo pichani) katika kikao cha waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza
nchini kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free kwa ajili ya ufuatiliaji wa mwenendo wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi
katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18 kilichofanyika
leo tarehe 04 Desemba, 2018 jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Gereza Kuu
Butimba Mwanza ASP. Dkt. Alex Lukuba
akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi (CGP Kasike) ikiwa ni utambuzi wa kufanya
vizuri kwa kituo anachokisimamia katika kusimamia masuala yahusuyo Ukimwi
katika kituo chake.
Kamishna
Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine
Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa
vituo vya afya vya magereza kote nchini na watendaji wakuu wa Asasi ya isiyo ya
kiserikali ya JSI AIDS Free ambayo ndiyo wafadhili wa Mradi Uimarishaji wa
Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya Magereza na polisi nchini. (Picha zote
na Jeshi la Magereza)
Sunday, November 18, 2018
KATIBU MKUU WA MAMBO YA NDANI, MEJA JENERALI JACOB KINGU AKAGUA MABORESHO YA KIWANDA CHA VIATU GEREZA KUU KARANGA MOSHI
2:01 PM
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Jacob Kingu akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoani
Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika ziara Maalum ya kukagua maboresho
mbalimbali katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi jana Novemba 17, 2018. Kushoto kwake ni Kamishna
Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu(meza kuu) akitoa maelekezo kwa
Kaimu Mkuu wa Kiwanda hicho, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Hamis
Nyaku(aliyesimama). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu na Kamishna Jenerali wa
Magereza, Phaustine Kasike wakiangalia Buti za aina mbalimbali za Jeshi zinazotengenezwa
katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi.
Sehemu
ya viatu aina mbalimbali ikiwemo viatu vya maafisa na Buti za Jeshi zinazotengenezwa
katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi kwa ajili ya Jeshi la Polisi nchini. Jeshi
la Polisi limetengenezewa viatu aina ya buti pea elfu kumi (10,000) na pea elfu
tano (5,000) za viatu vya maafisa zenye thamani ya Tsh. 1, 237, 666, 600/=, tayari
buti zimekabidhiwa kwa Jeshi hilo na hivi sasa kiwanda kinamalizia utengenezaji
wa viatu vya maafisa wa Jeshi la Polisi.
Maafisa
Masoko wa Kiwanda cha viatu Karanga Moshi wakivipanga viatu vya kiraia aina
mbalimbali vinavyotengenezwa katika kiwanda hicho kama inavyoonekana katika
picha.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akipata
maelezo ya kitaalam juu ya utengenezaji wa Buti za Jeshi kutoka kwa Mtaalam wa
utengenezaji viatu wa Jeshi la Magereza
(Picha zote na Jeshi la Magereza).
KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI NA CGP KASIKE WATEMBELEA KIWANDA CHA SAMANI CHA JESHI LA MAGEREZA CHA ARUSHA KILICHOTEKETEA KWA MOTO
1:27 PM
Na
Lucas Mboje, Arusha
KATIBU Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Jacob Kingu pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike leo wametembelea Kiwanda cha Samani cha Arusha, mali ya Jeshi la
Magereza ili kujionea athari mbalimbali iliyosababishwa na ajali ya moto
iliyotokea juzi Novemba 16, 2018.
Akizungumza
eneo la tukio Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob
Kingu amesema kuwa ni vyema taasisi mbalimbali nchini pamoja na wananchi
wakachukua tahadhali za majanga ya moto ili kuepusha hasara zinazoweza
kujitokeza kufuatia majanga hayo.
Amesema
kuwa Wizara yake itaendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vifaa vya
kisasa ili liweze kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza.
Aidha,
Katibu Mkuu huyo, Meja Jenerali Kingu amelitaka Jeshi la Magereza kuhakikisha
kuwa linafanya jitihada za haraka za kurejesha shughuli za uzalishaji katika
kiwanda hicho ikiwemo kufanyia matengenezo baadhi ya mashine zilizoteketezwa na moto.
Kwa
upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amevishukru
vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha sambamba na wananchi waliojitokeza kusaidia
katika uzimaji wa moto huo ambao umeunguza sehemu ya kiwanda hicho.
“Nawashukru
sana Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Arusha, Jeshi la Polisi pamoja na wananchi
kwa kazi kubwa waliyoifanya siku ya tukio kwani niliarifiwa kuwa moto ulikuwa
mkubwa lakini tunashukuru Mungu hatimaye uzimaji ulifanikiwa pamoja na hasara
iliyojitokeza”. Alisema Jenerali Kasike.
Akizungumzia
chanzo cha moto huo na hasara iliyojitokeza, Kamishna Jenerali Kasike amesema
kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya
umeme ambayo ilisababisha kuteketea kwa baadhi ya mashine za kiwanda hicho
pamoja na uharibu wa nyaraka mbalimbali za ofisi katika jengo la utawala.
Wakati
huo huo, Kamishna Jenerali Phaustine Kasike ameunda Kamati maalum ya Maafisa
watano kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza ambayo itachunguza chanzo cha
moto huo pamoja na kuwasilisha taarifa kamili ya hasara iliyojitokeza. Tume
hiyo itaongozwa na Kamishna wa Fedha na Mipango wa Jeshi hilo, Kamishna wa
Magereza, Gideon Nkana.
Kiwanda
cha samani cha Magereza Arusha kilimikishwa rasmi kwa Jeshi la Magereza mwaka
1973 baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967 ambapo tangu kipindi hicho kiwanda
hicho kinajishughulisha na utengenezaji wa samani mbalimbali za ofisi na samani
za majumbani. Pia kiwanda hiki hutumika kuwafundisha na kuwarekebisha wafungwa
ili wamalizapo vifungo vyao waweze kujitegemea kupitia ujuzi waliojifunza.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akiwasili Novemba 17, 2018 katika Kiwanda cha samani cha Magereza Arusha kukagua sehemu
mbalimbali ambazo moto umeteketeza sehemu ya kiwanda hicho. Kushoto kwake ni
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
Mkuu
wa Magereza Mkoa huo, ACP Anderson Kamtiaro akisoma taarifa ya janga la moto
mbele ya Katibu Mkuu Mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu
aliwasili kiwandani kujionea uhabribu mbalimbali uliojitokeza.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu
Mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu kuhusu hatua mbalimbali
ambazo amezichukua ikiwemo kuunda kamati maalum ya watu watano ambayo
itachunguza tukio la moto katika kiwanda hicho.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike (wa pili toka kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia kwake), wakiangalia moja ya mashine mbalimbali ambazo zimeteketezwa na moto katika kiwanda cha Samani cha Magereza Arusha. Chanzo cha moto huo inasemekana ni hitilafu ya umeme ndani ya kiwanda hicho.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (wa kwanza
kushoto) akitoa maelekezo mbalimbali kwa Kamishna Jenerali wa Magereza,
Phaustine Kasike(katikati). Kulia ni Kamishna wa Fedha na Mipango, Kamishna wa
Magereza, Gideon Nkana ambaye ni Kiongozi wa Kamati Maalum ya kuchunguza tukio
hilo.
Jengo
la kiwanda cha samani cha Magereza Arusha ambalo limeteketea kwa moto.
Muonekano
wa baadhi ya mashine pamoja na vifaa mbalimbali na nyaraka nyinginezo za ofisi
zilizoungua kufuatia janga la moto.
Samani
mbalimbali zinazotengenezwa katika kiwanda cha samani cha Magereza Arusha kama
inavyoonekana katika picha zikiwa tayari kwenda sokoni(Picha na Jeshi la Magereza).
Friday, November 16, 2018
MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AKUTANA NA RC NJOMBE KABLA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE TAREHE 15/11/2018
10:20 AM
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole
Sendeka akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike
alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa
kabla ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi, Novemba 15, 2018.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole
Sendeka akitoa taarifa fupi ya Mkoa wake alipotembelewa na Mkuu wa Jeshi la
Magereza Ofsini kwake.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP)
Phaustine Kasike akielezea malengo ya ziara yake ya kikazi mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Njombe alipotembelea Ofisi za Mkoa huo.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza, CGP. Phaustine Kasike akiagana na baadhi ya askari wa
Gereza Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe.
Christopher Ole Sendeka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini,
Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Njombe. Wa pili toka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa
Njombe, Bw. Erick Shitindi ( Picha
na Jeshi la Magereza).
Thursday, November 15, 2018
ZIARA YA CGP KASIKE GEREZA LA WILAYA MAKETE, MKOANI JOMBE
1:34 AM
Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine
Kasike akizungumza jambo alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya Makete Novemba 14, 2018. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza
wakiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ambapo
askari hao wamempongeza Mkuu wa Jeshi hilo kwa uamuzi wake wa kutembelea magereza
mbalimbali hapa nchini.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine
Kasike akiwasili Gereza Makete tayari kwa ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe, Novemba 14, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua
maandalizi ya mashamba ya kilimo cha mahindi katika eneo la Gereza Ludewa
mapema leo asbuhi Novemba 14, 2018 kabla
ya kuelekea Gereza Makete kuendelea na ziara yake ya kikazi.
Mkuu wa Gereza Makete, SP. Aloyce
Kayera(kushoto) akisoma taarifa ya Gereza mbele ya Kamishna Jenerali wa
Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(kulia) alipotembelea gereza hilo leo
Novemba 14, 2018.
. Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Veronica Kessy
akiagana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya Makete.