Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Wednesday, January 20, 2021

TANZIA: NAIBU KAMISHNA WA MAGEREZA JULIUS SANG'UDI AFARIKI DUNIA JIJINI DODOMA.

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

(Jeshi la Magereza)

TANZIA

 

 

 

Kamishna Jenerali wa Jeshi Magereza Mej. Jen Suleiman M. Mzee anasikitika kutangaza kifo cha Naibu Kamishna wa Magereza Julius Mayenga Sang’udi kilichotokea Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma leo tarehe 20 Januari, 2021.

Aidha anatoa pole kwa Familia ya Marehemu, Watumishi wote wa Jeshi la Magereza Nchini, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.

Jeshi  la Magereza kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaendelea kuratibu taratibu za Mazishi nyumbani kwake Kisasa nyumba 300, Dodoma.

Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa Ijumaa tarehe 22 Januari,2021 na Mazishi yatafanyika Mkoani Simiyu Kijiji cha Ikulilo – Mwandete Jumamosi tarehe 23 Januari,2021.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amen.

 

Imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Magereza,

Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya Umma,

Dodoma.

Saturday, January 16, 2021

MAGEREZA WAOKOA BILIONI 11 ZA CHAKULA CHA WAFUNGWA.


Na Mwandishi Wetu


Jeshi la Magereza nchini limeokoa jumla ya Shilingi Bilioni 11, ikiwa
ni gharama ya chakula cha wafungwa tangu lianze kujitegemea kwa
chakula ikiwa  ni maelekezo ya Rais  Dkt. John Pombe Magufuli ya
kulitaka jeshi hilo litumie nguvu kazi ya wafungwa ilionao kuzalisha
chakula.

Akizungumza leo katika ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,iliyofanyika katika Makao Makuu Mapya ya Jeshi hilo ,Msalato
jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee amesema
walikuwa wanatumia Shilingi Bilioni Moja kila mwezi kulipa wazabuni wa
chakula waliokuwa wanaliuzia chakula  jeshi hilo.

“Sasa hivi tunajitegemea asilimia kubwa kwa chakula, Serikali kabla ya
mwezi wa tatu mwaka jana kila mwezi kulikua kuna deni la Bilioni Moja,
lakini baada ya mwezi huo wa tatu sasa tunaokoa kiasi hicho cha fedha
shilingi bilioni moja na mpaka sasa tuna miezi kumi na moja
tunajilisha wenyewe kupitia shirika la magereza” alisema CGP Mzee

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo
alilipongeza Jeshi la Magereza kwa kutekeleza vyema agizo la Rais
Magufuli ikiwa sambamba na ujengaji wa kiwanda kikubwa cha samani
ambapo mpaka kukamilika kwake kitagharimu shilingi Bilioni
1,101,743,123/=

“Niwapongeze kwa hatua mbalimbali za maendeleo ambazo zingine
nimeshuhudia mwenyewe,lakini kubwa kuweza kujitegemea kwa chakula cha
wafungwa hali iliyopelekea kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho
kinabaki humu humu ndani na mnakitumia kwa shughuli zingine za
maendeleo hongereni sana” alisema Naibu Waziri Chilo

Kamishna Jenerali wa Magereza Mej. Jen. S.M Mzee akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa mambo ya ndani  ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (MB) wakati wa Ziara ya Kikazi Makao Makuu ya Jeshi la Magereza  Jijini Dodoma jana tarehe 15 Jan, 2021.

Kamishna Jenerali  Suleiman M. Mzee (kushoto  akimpa taarifa fupi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Khamis Hamza Chilo  alipotembelea Makao Makuu ya Magereza Jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (MB) akipanda Mti mbele ya Ofisi ya Ofisi ya  Makao Makuu Ya Magereza eneo la Msalato Jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Khamis Chilo akitoa maelekezo alipotembelea Makao Makuu ya Magereza sehem ya Kiwanda cha Samani Msalato jijini Dodoma.

Mrakibu msaidizi wa Magereza Malima akifafanua jambo mbele ya Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Khamis Chilo katika Mashine za Kiwanda cha Samani Msalato jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Chilo (kushoto,mbele) akipokewa na Mwenyeji wake Kamishna Jenerali wa Magereza Mej. Jen. Suleiman Mzee ( kulia, mbele) alipotembelea Makoa Makuu ya Magereza katika ziara ya kikazi jijini Dodoma jana.

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Chilo akikagua gwaride la heshima lilioandalia kwa ajili yake wakati  wa Ziara ya kikazi Makao makuu ya Magereza Jijini Dodoma.