Friday, February 28, 2020
WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA POLISI KUACHA KUZALISHA MAHABUSU MAGEREZANI
4:09 PM
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee(kulia) leo alipotembelea Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu
ateuliwe katika Wizara hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Maafisa na askari
wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani)leo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la
Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe katika
Wizara hiyo. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee(
Kulia )ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu, Uwesu Ngarama.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene(meza kuu katikati) kabla ya
kuongea na Maafisa na askari wa Jeshin hilo. Kulia ni Kamishna wa Utawala na
Rasilimali watu, Uwesu Ngarama.
Baadhi
ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa
Mambo ya ndani ya Nchi, George Simbachawene (hayupo pichani).
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene(kulia) akitoa maelekezo kwa
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee(wa pili toka kushoto) leo
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara
yake ya kwanza tangu ateuliwe katika Wizara hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George
Simbachawene(Kaunda suti) akiingia Gereza Kuu la Isanga, jijini Dodoma, leo,
tayari kwa kuzungumza na Wafungwa na Mahabusu waliopo katika Gereza hilo.
Wednesday, February 19, 2020
JESHI LA MAGEREZA KUJITEGEMEA KWA KUTUMIA RASILIMALI ZAKE
5:19 PM
Kamishna Jenerali wa Magereza,
Suleiman Mzee akiongoza Kikao kazi cha siku moja cha Maafisa Waandamizi wa
Jeshi la Magereza, Kikao hicho
kimefanyika leo Februari 19, 2020 katika
Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Magereza Mikoa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi
la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa
Magereza, Suleiman Mzee(hayupo pichani)katika Kikao kazi kilichofanyika leo
katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma.
Kamishna wa Utawala na Rasilimali
watu wa Jeshi la Magereza, Uwesu Ngarama akitoa taarifa fupi katika Kikao kazi
cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha
Mipango, Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Sekretarieti wakifuatilia kikao kazi hicho kilichoongozwa na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza leo Februari 19, 2020 katika Ukumbi Chuo
cha Mipango, jijini Dodoma (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Friday, February 14, 2020
MAAFISA WASHIRIKI KUTOKA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA(NDC) WATEMBELEA KIWANDA CHA GEREZA KUU UKONGA JIJINI DSM
7:58 AM
Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Bregedia
Jenerali Cherestino Msolla (kushoto) akisalimiana
na Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga, ACP. Nsajigwa Mwankenja walipofanya ziara ya
mafunzo katika Jeshi la Magereza Februari 12, 2020.
Maafisa Washiriki kutoka
Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakitembelea sehemu mbalimbali katika Kiwanda cha
Gereza Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.
Maafisa Washiriki kutoka
Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakizungumza na mfungwa ambaye amepatiwa ujuzi
gerezani wa fani ya ushonaji katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu Ukonga
kama inavyoonekana katika picha.
Maafisa Washiriki kutoka
Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakitoka katika
Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kuendelea na ziara yao ya mfunzo katika maeneo
mbalimbali ya Jeshi la Magereza.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la
Magereza, SSP. Amina Kavirondo akiwasilisha andiko linalohusu majukumu ya Jeshi
hilo mbele ya Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa (hawapo pichani).
Maafisa Washiriki kutoka
Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa mbalimbali
nkuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza ikiwemo program
za urekebishaji, Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Askari wa
Kikosi Maalum cha Magereza kikionesha onesho la ukakamavu mbele ya Maafisa
Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(NDC) walipotembelea Makao Makuu ya
Kikosi hicho, jijini Dar es Salaam.
Maafisa Washiriki kutoka
Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania wakiburudika na matunda ya madafu katika
ziara yao ya mafunzo katika Jeshi la Magereza.
Kamishna wa Magereza,
Uwesu Ngarama(wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa
Washiriki waliotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jana(waliosimama
mstari wa nyuma) kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(wa pili toka kushoto
walioketi) ni Mkufunzi Mwandamizi wa
Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Bregedia Jenerali Cherestino Msolla (kushoto) ni Naibu Kamishna
wa Magereza, Jeremiah Katungu (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Tuesday, February 11, 2020
MAAGIZO
8:36 AM
#MAAGIZO - KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza, Suleiman Mzee amepiga marufuku mazoea ya baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi hilo kulima mashamba yao, kufuga mifugo katika mazizi yanayomilikiwa na Jeshi pamoja na matumizi binafsi ya nguvu kazi ya wafungwa. #MagerezaTz
Monday, February 10, 2020
CGP SULEIMAN MZEE AONGOZA KIKAO KAZI LEO CHA MAAFISA NA ASKARI MAGEREZA TOKA VITUO VYA KANDA YA DAR ESALAAM
3:05 PM
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji Tanzania, ACP. Joel Matani kabla ya kikao kazi cha Maafisa na
Askari wa Jeshi la Magereza kutoka katika vituo vilivyopo Kanda ya Dar es
Salaam, leo Februari 10, 2020.
Kamishna wa Magereza anayeshughulika na Utawala na
Rasilimali watu, Uwesu Ngarama akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha
Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(katikati meza kuu) kuzungumza
katika kikao kazi cha Maafisa na Askari wa Jeshi la
Magereza kutoka katika vituo vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam, leo Februari
10, 2020.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akiongoza
kikao kazi cha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka katika
vituo vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam, leo Februari 10, 2020.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia
kwa umakini mkubwa maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza aliyoyatoa katika
Kikao kazi cha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka
katika vituo vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la
Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza, Kanda ya Dar es Salaam
wakisikiliza maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (hayupo
pichani) katika Kikao kazi hicho (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Sunday, February 9, 2020
WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KIWANDA KIPYA CHA NGOZI KARANGA, MOSHI
12:46 PM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Uwekezaji)
Jenista Mhagama (wa tatu toka kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Andrew Massawe (wa pili toka kushoto)
wakiongozana na Makamanda Waandamizi wa Jeshi la Magereza Nchini wakati wa
ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi wa kiwanda cha Ngozi cha Karanga
kinachojengwa kwa Ubia baina ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF) na Gereza la Karanga lilolopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Februari 8,
2020.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Uwekezaji) Jenista Mhagama (wa pili
toka kulia) akitoa maelekezo leo kwa watendaji mbalimbali Naibu Kamishna wa
Magereza, Afwilile Mwakijungu(kushoto) ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la
Uzalishaji Mali la Magereza wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi wa
kiwanda cha Ngozi cha Karanga kinachojengwa kwa Ubia baina ya Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)
na Jeshi la Magereza.
Moja ya majengo katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Ngozi cha Karanga kinachojengwa kwa Ubia
baina ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Jeshi la
Magereza likiwa limefikia hatua mbalimbali za ujenzi kama inavyoonekana katika
picha. Jengo hilo litatumika kuhifadhia mashine ambazo tayari zimewasili
bandarini
Mhandisi wa Mradi wa ujenzi wa
Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi, Mrakibu wa Magereza, Julius Sukambi (kulia)
akisoma taarifa ya ujenzi mbele ya Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Uwekezaji) Jenista
Mhagama (kushoto).
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa majengo ya kiwanda hicho (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Wednesday, February 5, 2020
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, SULEIMAN MZEE AKAGUA USIMIKAJI WA MIUNDOMBINU YA MAJI KATIKA MAJENGO YA MAKAZI YA MAAFISA NA ASKARI MAGEREZA, UKONGA DSM
1:07 PM
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee
akisalimiana na Mkuu wa Kiwanda cha Samani cha Gereza Kuu Ukonga, ACP. John
Itambu mapema leo alipokagua zoezi la uwekaji miundombinu ya maji katika
majengo ya makazi ya Maafisa na askari Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya
kutembelea eneo la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi hilo.
Mkuu wa Magereza Mkoani Dar es Salaam, SACP.
Julius Ntambala(kushoto) akitoa taarifa fupi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Suleiman Mzee(wa pili toka kulia) mapema leo alipokagua zoezi la
uwekaji miundombinu ya maji katika majengo ya makazi ya Maafisa na askari
Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya kutembelea eneo la ujenzi wa Hospitali
Kuu ya Jeshi hilo.
Moja
ya majengo ya makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza yaliyopo Ukonga
Dar es Salaam ambayo yamekabidhiwa hivi karibuni na Rais Magufuli.
Mkuu
wa Magereza Mkoani Dar es Salaam, SACP. Julius Ntambala akitoa taarifa fupi kwa
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(wa pili toka kulia) mapema
leo alipokagua zoezi la uwekaji miundombinu ya maji katika majengo ya makazi ya
Maafisa na askari Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya kutembelea eneo la
ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi hilo (Picha
zote na Jeshi la Magereza).
Tuesday, February 4, 2020
NIPENI USHIRIKIANO - KAMISHNA JENERALI MPYA WA MAGEREZA, SULEIMAN MZEE
11:57 AM
Na ASP Lucas Mboje, DSM
KAMISHNA Jenerali mpya wa Magereza
nchini, Suleiman Mzee (pichani) amewataka
Maofisa na askari wote wa Jeshi la Magereza kumpa ushirikiano katika uongozi
wake ili aweze kusimamia vyema maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Rais Dkt.
John Pombe Magufuli kwa Jeshi hilo ikiwemo jukukumu la kujitegemea kwa chakula
cha wafungwa magerezani.
Akizungumza
na Maofisa, askari na watumishi raia wa Jeshi hilo katika Ofisi ndogo za Makao
Makuu ya Magereza, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Suleiman Mzee amesema
kuwa anayomatarajio makubwa ya kuhakikisha kuwa Jeshi la Magereza linakuwa na
miradi mingi ya uzalishaji mali ili kuwezesha kujitegemea badala ya kutegemea
bajeti kuu ya Serikali.
“Ni
lazima tuzalishe kwa wingi na kila gereza lizalishe kulingana na fursa zilizopo
ikiwa tunataka kujiwekea mazingira ya kuaminika. Pia, tuhakikishe kuwa utaalam
wetu katika nyanja mbalimbali lazima uwe na manufaa Jeshini”, amesisitiza Jenerali
Mzee.
Aidha,
Kamishna Jenerali Mzee ameongeza kuwa ni vyema maofisa na askari wa Jeshi hilo
wakazingatia utii, uaminifu pamoja na uhodari katika kazi ili kuyafikia
matarajio hayo makubwa ndani ya Jeshi.
“Mkizingatia
utii, uaminifu pamoja na uhadari katika kazi naamini matokeo chanya yataonekana
katika muda mfupi kwani upo uwezekano wa kufanya mambo makubwa ambayo yataliletea
heshima na sifa Jeshi letu la Magereza”, amesema Jenerali Mzee.
Kuhusu
mafunzo mbalimbali kwa maafisa na askari, amesema kuwa atapitia mitaala ya
mafunzo ili kuona kama inaendana na mazingira yaliyopo pamoja na kuifanyia
maboresho mbalimbali kwani mafunzo ni nguzo muhimu katika kujenga nidhamu kwa maafisa
na askari.
Kwa
upande wake aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike(sasa Balozi Mteule) alimpongeza Jenerali Mzee kwa kuteuliwa na Rais
kushika nafasi hiyo na alibainisha baadhi ya changamoto ambazo zinalikabili
Jeshi hilo ikiwemo uchakavu wa makazi ya askari.
“Nafurahi
kuwa naliacha Jeshi la Magereza likiwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na kuwa
na baadhi ya changamoto mbalimbali ikiwemo makazi duni ya askari, naamini
changamoto hizo utazifanyia kazi kwani tayari tulikwishaanza kuchukua hatua”,
amesema Mhe. Balozi Kasike.
Jeshi
la Magereza linamiliki ardhi yenye ukubwa wa ekari 326,205 Tanzania Bara, kati
ya hizo ekari 151,350 zinafaa kwa shughuli za kilimo na mifugo. Eneo
linalotumika kwa shughuli za kilimo kwa sasa ni ekari 20,580 pekee sawa na
asilimia 13.60 ya eneo linalofaa kwa shughuli za kilimo. Jeshi hilo likijipanga
kimkakati linaweza kujilisha, kuongeza pato serikalini pamoja na kufanya
mapinduzi makubwa ya kilimo hapa nchini.
MAPOKEZI YA KAMISHNA JENERALI MPYA WA MAGEREZA OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA MAGEREZA, JIJINI DAR
9:17 AM
Kamishna Jenerali mpya wa
Magereza, Suleiman Mzee akipokea salaam ya heshima toka Gwaride Maalum
lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kwa
ajili yake kwa heshima katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Magereza,
Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akikagua
Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa
ajili yake kwa heshima kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akisalimiana na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa
Magereza, Phaustine Kasike (sasa Balozi
mteule) alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo baada ya kuapishwa rasmi kuwa
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari
3, 2020. Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Uwesu
Ngarama.
Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akifanya
mahojiano maalum na wanahabari baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za Makao
Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akiongea na
Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza baada ya kutoka
kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Februari 3, 2020.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa
Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali mpya wa Ma gereza, Suleiman
Mzee mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020 (Picha zote na Jeshi la Magereza).