About Us

HISTORIA YA JESHI LA MAGEREZA TANZANIA BARA                                                                                                                                                   
1.0.Utangulizi                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                          Jeshi la Magereza lilianzishwa rasmi mwezi Agosti 25,1931 baada ya mgawanyo wa majeshi ya Polisi na Magereza kutokea.  Licha ya kuwa na majukumu ya kulinda usalama na mali za wageni, kabla ya mwaka 1931 Jeshi la Polisi lilifanya pia kazi za Magereza kama zilivyokuwa kwa tafsiri na madhumuni ya wakoloni.  Jeshi la Magereza wakati lilipoanzishwa liliitwa Idara ya Jela ambapo shughuli zake zilibaki kuwa zile za kikoloni za utesaji wa wafungwa pamoja na kazi ngumu bila kujali kama ni ya manufaa kwao au kwa Taifa.

2.0    Dira na dhima ya Jeshi la Magereza

Jeshi la Magereza katika miaka ya 1990 lilianzisha dira na dhima yake kulingana na mabadiliko mbalimbali yaliyojitokeza.Dira ya Jeshi la Magereza ni kuwa Jeshi la kurekebisha wahalifu lenye utaalam wa hali ya juu linaloendeshwa katika kanuni na viwango vilivyowekwa Kitaifa na Kimataifa.

Dhima ya Jeshi la Magereza ni kutekeleza wajibu ipasavyo katika kuimarisha ulinzi wa jamii kupitia usimamizi wa kifungo na kuwasimamia wahalifu, huduma za mahabusu, programu na huduma zinashughulikia mahitaji ya urekebishaji wa wahalifu na ushauri wa Sera kuhusu uzuiaji wa uhalifu na ushughulikiaji wa wahalifu.

3.0    Majukumu na malengo ya Jeshi la Magereza

Majukumu ya Jeshi la Magereza ni kuchangia katika kuleta, kuendeleza na kudumisha usalama wa jamii nchini kwa kufanya yafuatayo:-
•    Kuwahifadhi wafungwa wa aina zote wanaowekwa chini ya ulinzi halali kisheria ndani ya magereza.
•    Kuandaa na kutekeleza programu za urekebishaji wa wahalifu na kuwafundisha wahalifu shughuli za uzalishaji na ujuzi mbalimbali kwa njia ya vitendo na ushauri.

•    Kuendesha shughuli na huduma za watuhumiwa (Mahabusu) kwa mujibu wa sheria.

•    Kuchangia katika ushauri kuhusu uzuiaji na udhibiti wa uhalifu na urekebishaji wahalifu.

Kwa kuwahifadhi wafungwa katika mazingira ambayo ni salama, Jeshi la Magereza linalenga kuilinda jamii dhidi ya wahalifu hao na hivyo kuiwezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za uzalishaji kwa ajili ya kupata maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Aidha, kupitia utoaji wa programu za urekebishaji na ufundishaji wa shughuli za uzalishaji na ulinzi, Jeshi la Magereza linakusudia kuwawezesha wahalifu kuachana na mwenendo wa kihalifu Magerezani na watakaporejea kwenye jamii baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao waishi maisha yanayozingatia sheria za nchi.

4.0    Sheria na Kanuni mbalimbali zinazotumika katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza.

•    Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977
(The Constitution of United Republic of Tanzania, 1977);

•    Sheria ya Magereza Na. 34 ya 1968
(The Prisons Act, No. 34 of 1967);

•    Kanuni za Kifungo cha Nje, 1968
(The Prisons (Extra Mural Employment Regulations, 1968);

•    Kanuni za Makosa ya Magereza, 1968
(The Prisons (Prison Offences) Regulations, 1968);

•    Kanuni za Uendeshaji wa Magereza, 1968
(The Prisons (Prison Management) Regulations, 1968;

•    Kanuni za matumizi ya Pingu, 1968
(The Prison (Restraint of Prisoners Regulations. 1968;

•    Sheria ya Bodi za Parole, 1994
(The Parole Boards Act, 1994;

•    Kanuni za Bodi za Parole, 1997
(The Parole Boards Regulations, 1997;

•    Sheria ya kuhamishiana Wafungwa, 2004
(The Transfer of Prisoners Act,2004;

•    Kanuni za kuhamishiana Wafungwa, 2004
(The Transfer of Prisoners Regulations, 2004;

•    Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, 2001
(The Commission for Human Rights and Good Governance, Act, 2001;

•    Sheria ya Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza. 1990
(The Police Force and Prisons Service Commission Act, 1990;

•    Sheria ya Watoto na Vijana ya Mwaka 1937, sura ya 13
(The Children and Young Persons Ordinance 1937 (Chapter 13 of the Revises Laws);

•    Kanuni za Watoto na Vijana (Shule Maadilisho) za Mwaka 1945
(The Children and Young Persons (Approved School) Annual Holiday) Rules, 1945);

•    Sheria ya Uangalizi wa Wahalifu ya Mwaka 1947, Sura ya 247
(The Probation of Offenders Ordinance, 1947 (Chapter 247 of the Revised Laws);

•    Sheria ya Wakimbizi ya Mwaka, 1998
(The Refugees Act, 1998);

•    Sheria ya Kutangaza Uangalizi wa Wahalifu, 1950 – 1961
(The Probation of Offenders Proclamations, 1950 – 1961);

•    Sheria ya Kima chini cha Adhabu za Makosa ya Jinai ya Mwaka 1972
(The Minimum Sentences Act, 1972);

•    Sheria kwa Huduma kwa Jamii, 2002
(The Community Service Regulations, 2002);

•    Sheria ya Utumishi wa Jeshi la Magereza Mwaka 1997
(The Prisons Service Regulations, 1997);

•    Sheria Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002
(The Public Service Act, 2002);

•    Kanuni za Kudumu za Jeshi la Magereza, Toleo la 4 la 2003
(Prison Standing Prders (4th Edition 2003).