Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, July 12, 2019

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE AKAGUA SHAMBA LA KIMKAKATI LA MAHINDI KATIKA GEREZA LA KILIMO NA MIFUGO KITENGULE, MKOANI KAGERA

Kamishna Jenerali wa Magereza( wa Kwanza kulia) akikagua shamba la mahindi ambalo liko katika hatua za mwisho za kuvunwa la gereza Kitengule.

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akikagua ghala la kuhifadhia chakula cha wafungwa Gereza Kitengule alipotembelea gereza hilo leo Julai 11, 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akiangalia moja ya mashine maalum inayotumika katika upandaji wa mbegu katika mashamba ya Gereza Kitengule alipotembelea gereza hilo leo Julai 11, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza)

ZAIDI YA WAFUNGWA 640 WAMENUFAIKA NA MPANGO WA BODI YA PAROLE NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU


                      


 
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) afungue rasmi Kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga,  Jijini Dar es Salaam.


           Baadhi ya Wajumbe Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.


Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(hayupo pichani) akifungua kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole.

      Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(meza kuu) akiongoza Kikao cha 41 cha Bodi hiyo.

Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Jeshi la Magereza).



Thursday, July 4, 2019

JESHI LA MAGEREZA WAIBUKA WASHINDI WA JUMLA MAONESHO YA 43 YA BIASHARA YA KIMATAIFA KWA MWAKA 2019, JIJINI DAR

SABASABA2019 - Jeshi la Magereza limeibuka Mshindi wa Kwanza wa jumla(Overal Winner) kwenye maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam. Pichani ni Maafisa Washiriki kutoka Jeshi la Magereza wakiwa na tuzo hizo(Picha na Jeshi la Magereza)