Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Saturday, February 28, 2015

Kamishna jenerali wa Magereza azindua huduma za "Duty Free Shop" Magereza Uyui Tabora

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashilia uzinduzi rasmi wa "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora leo februari 28, 2015. Kamishna Jenerali Minja amesema kuwa Huduma hiyo itatolewa pia kwa Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoani Tabora(kulia) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika  "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora mara tu baada ya uzinduzi rasmi leo februari 28, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Uyui, Tabora.
Muonekano wa Jengo la "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora ambalo limzunduliwa leo februari 28, 2015 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani)
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora.
Kikundi cha ngoma za asili ambacho kinaundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Tabora kikitumbuiza katika hafla ya "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora(wa pili kulia) ni RPC Tabora, ACP Suzani Kaganda(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga, SACP. Anet Laurent(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tabora, SACP. Rajab Mbilo(wa tatu kushoto) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji(wa tatu kulia) ni Katibu Tawala Mkoani Tabora, Bi. Kudra Mwinyimvua.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Wednesday, February 25, 2015

Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi azindua rasmi "Rest House" ya Magereza, mkoani Morogoro

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(suti nyeusi) akijiandaa kukata utepe kwenye hafla ya Ufunguzi wa Jengo la "Rest House" ya Magereza leo februari 25, 2015 Mkoani Morogoro ambapo ukarabati wa Jengo hilo umefanyika chini ya Kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Magereza(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akisoma jiwe la msingi mara baada ya ufunguzi wa Jengo la "Rest House" ya Magereza leo februari 25, 2015 Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akiangalia vyumba mbalimbali vya kulala Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza vilivyopo katika Jengo la "Rest House" ya Magereza, Mkoani Morogoro(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.

Muonekano wa Jengo la "Rest House" ya Magereza  Mkoani Morogoro ambalo limezinduliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil. kukamilika kwa jengo hilo kutaondoa usumbufu wa kutafuta hoteli kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanapokuwa safari za kikazi Mkoani Morogoro na pia kuipunguzia gharama Serikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akiwa ameketi kwenye Sofa zilizopo katika "Rest House" ya Magereza kama anavyoonekana katika picha. Sofa hizo zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa na Mafundi mahili wa Jeshi la Magereza.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Mafundi wa Kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Magereza ambao wamesimamia kikamilifu ujenzi wa "Rest House" ya Magereza (wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) niKamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, James Selestine(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunula.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Tuesday, February 24, 2015

Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi afungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa TPS Saccos Ltd leo, mkoani Morogoro

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza mara tu baada ya kumpokea Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Bw. Mbarak Abdulwakil(suti nyeusi) ambaye amefungua Mkutano Mkuu wa TPS SACCOS Ltd unaofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro kuanzia leo februari 24, 2015.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Bw. Mbarak Abdulwakil akisoma Hotuba ya Ufunguzi wa  Mkutano Mkuu wa tatu wa TPS SACCOS Ltd leo februari 24, 2015unaofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro.
Maafisa wa Jeshi la Magereza wenye vyeo mbalimbali ambao ni Wanachama wa TPS SACCOS Ltd kutoka Mikoa yote Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa tatu wa TPS SACCOS Ltd leo februari 24, 2015 unaofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro.
Meza Kuu wakiwa wameketi wakifuatilia zoezi la Utambulisho wa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tatu wa TPS SACCOS Ltd leo februari 24, 2015unaofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro(katikati) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Bw. Mbarak Abdulwakil(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akifanya mahojiano maalum na Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari walioshiriki kikamilifu katika Ufunguzi wa  Mkutano Mkuu wa tatu wa TPS SACCOS Ltd leo februari 24, 2015unaofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Bw. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tatu wa TPS SACCOS Ltd leo februari 24, 2015 unaofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Magereza, Deonice Chamulesile(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Mwenyekiti TPS SACCOS Ltd, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Joel Bukuku

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Saturday, February 21, 2015

Taarifa kwa vyombo vya habariFriday, February 20, 2015

Asasi ya "AIDS-free" kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi ndani ya jeshi la Magereza

 Mkurugenzi wa Mradi wa "AIDS free", Bw. Samson Kironde(wa pili kushoto) akitoa maelezo mafupi namna mradi huo utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza na Polisi katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza leo februari 20, 2015(wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Operesheni na Fedha, Bw. Mike Hames(wa kwanza kushoto) ni Afisa Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya UKIMWI kutoka USAID, Bw. Erick Mlang'ha.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisisitiza jambo katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Polisi na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa "AIDS - free" utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioshriki katika mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa "AIDS - free" unaotarajiwa kutekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gedion Nkana(wa kwanza kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja.
Maofisa Wasimamizi wa Sekta ya Afya kutoka Jeshi la Polisi wakifuatilia mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa "AIDS - free"(wa kwanza kushoto) ni Dkt. Nyanda Lushina(katikati) ni Mrakibu wa Polisi, Husein Yahya.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(meza kuu) akiongoza mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa "AIDS - free" utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Tuesday, February 17, 2015

Waziri wa katiba na sheria atembelea makao makuu ya jeshi la magereza, jijini Dar

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akimkaribisha Ofsini kwake Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo februari 17, 2015, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiendelea na mazungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro(hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo februari 17, 2015, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo februari 17, 2015, Jijini Dar es Salaam.

Thursday, February 5, 2015

Kikao cha kwanza cha bodi ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji gereza Kigongoni-Bagamoyo kati ya shirika la Magereza na kampuni ya Tarbim chafanyika leo mjini Bagamoyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu akitoa maelezo mafupi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo(kushoto) ni Mjumbe wa Bodi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Green Park iliyoko Bagamoyo.
Wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji kutoka Jeshi la Magereza wakisikiliza maelezo ya utambulisho kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim Bw Baddal Calikusu (hayupo pichani)

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (aliyesimama) akitoa utambulisho kwa wajumbe wapya wa Bodi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo .
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana akiwa na Wajumbe wengine wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni wakikagua eneo la Mradi utakapotekelezwa.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni mara baada ya Kikao cha kwanza kilichofanyika katika Hoteli ya Green Park iliyopo Mjini Bagamoyo (wa kwanza kulia) ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana (wa tatu kulia) ni Mjumbe wa Bodi, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Masunga.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)