Wednesday, February 25, 2015

Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi azindua rasmi "Rest House" ya Magereza, mkoani Morogoro

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(suti nyeusi) akijiandaa kukata utepe kwenye hafla ya Ufunguzi wa Jengo la "Rest House" ya Magereza leo februari 25, 2015 Mkoani Morogoro ambapo ukarabati wa Jengo hilo umefanyika chini ya Kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Magereza(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akisoma jiwe la msingi mara baada ya ufunguzi wa Jengo la "Rest House" ya Magereza leo februari 25, 2015 Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akiangalia vyumba mbalimbali vya kulala Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza vilivyopo katika Jengo la "Rest House" ya Magereza, Mkoani Morogoro(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.

Muonekano wa Jengo la "Rest House" ya Magereza  Mkoani Morogoro ambalo limezinduliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil. kukamilika kwa jengo hilo kutaondoa usumbufu wa kutafuta hoteli kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanapokuwa safari za kikazi Mkoani Morogoro na pia kuipunguzia gharama Serikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akiwa ameketi kwenye Sofa zilizopo katika "Rest House" ya Magereza kama anavyoonekana katika picha. Sofa hizo zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa na Mafundi mahili wa Jeshi la Magereza.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Mafundi wa Kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Magereza ambao wamesimamia kikamilifu ujenzi wa "Rest House" ya Magereza (wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) niKamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, James Selestine(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunula.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).