Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Tuesday, January 27, 2015

Ujumbe kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) watembelea makao makuu ya jeshi la magereza jijini Dar

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto) akisalimiana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 27, 2015(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto) akisaini katika kitabu cha wageni mapema leo alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza kwenye ziara ya mafunzo kuhusu uendeshaji wa Jeshi la Magereza(kulia) ni Kamishna wa Magereza, Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwasilisha mada yake ya uchokozi kuhusu Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele ya Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(hawapo pichani)
Wakufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Kamishna wa Magereza, Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania walipofanya ziara ya mafunzO(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Bregedia Jenerali Sylivester Minja

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Tuesday, January 13, 2015

Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja ampandisha cheo cha Sajin wa magereza askari wa kike, mwanariadha wa kimataifa jijini Dar

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimvisha cheo cha Sajin wa Magereza, Askari Mwanariadha wa Kimataifa,  CPL. Catherina Lange(hivi sasa cheo cha sajin) wa Gereza Kuu Arusha ambaye ambaye hushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla. hafla hiyo imefanyika leo Januari 13, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza Sajin wa Magereza, Askari Mwanariadha wa Kimataifa, wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla rasmi ya kumvalisha cheo hicho ambapo askari huyo hushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.
Wanahabari toka Vyombo mbalimbali vya Habari wakifanya mahojiano Maalum na Askari Mwanariadha wa Kimataifa,  Sajin wa Magereza Catherina Lange(hayupo pichani) wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(Meza kuu) akitoa maelezo mafupi kwa Waandishi wa Habari(hawapo pichani) namna Askari Mwanariadha wa Kimataifa,  CPL. Catherina Lange(hivi sasa cheo cha sajin) wa Gereza Kuu Arusha alivyoshiriki kwa mafanikio makubwa katika mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe akimpa pongezi Askari Mwanariadha wa Kimataifa,  Sajin wa Magereza Catherina Lange(kulia) wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hamis Nkubas akiwa katika picha ya pamoja na Askari Mwanariadha wa Kimataifa,  Sajin wa Magereza Catherina Lange(katikati) wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Kuu Arusha, Themistocles Ifunya.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)


Saturday, January 10, 2015

Sherehe ya maofisa magereza kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015 yafana Jijini Dar

Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015. sherehe hiyo imefanyika Januari 9, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga, Jijini Dar s Salaam.
Makamanda na Wapiganaji wa Jeshi la Magereza wakiwa katika sherehe  ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015. sherehe hiyo imefanyika Januari 9, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga, Jijini Dar s Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(wa tatu kushoto) atoe hotuba yake (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Bw. Daud Msangi(wa pili kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa tatu kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. Dickson Mwaimu(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa) .
Maofisa wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni waalikwa wakipita mbele ya Mgeni rasmi kwa ajili ya kutosi glasi za vinywaji katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015.
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akikabidhi zawadi ya Luninga mmoja wa Maofisa wa Jeshi la Magereza ambaye ni Mhakiki wa Sanaa na Lugha Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Mrakibu wa Magereza, Rashid Mtimbe katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015.
Maofisa wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni waalikwa wakisakata rumba katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015.