Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Sunday, December 31, 2017

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2017 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2018 JIJINI MBEYA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018. Baraza hilo limehudhuriwa na Maafisa na Askari kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Mbeya, Chuo cha Magereza Kiwira na Chuo cha Ufundi Mbeya ambapo Baraza hilo limefanyika leo Desemba 31, 2017 katika Viwanja  vya Magereza Mkoani Mbeya.
Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza ya Mkoa wa Mbeya wakisikiliza hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018.
Wakuu wa Magereza yaliyopo Mkoani Mbeya wakifuatilia kwa umakini mkubwa maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza aliyoyatoa katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018.
Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kijida Mwakingi akitoa taarifa fupi ya Mkoa wake katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018.
Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akitoa ufafanuzi wa masuala yahusuyo Divisheni ya Huduma za Urekebishaji mbele ya  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) katika Baraza la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018 (wa kwanza kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza. Baraza hilo limefanyika katika Viwanja  vya Magereza Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu katika Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Chacha Binna akitolea ufafanuzi kuhusiana na masuala ya madeni ya watumishi yaliyoulizwa na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo Mkoani Mbeya(hawapo pichani) katika Baraza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa gwaride maalum alipowasili katika Viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya kabla ya kuhutubia Baraza la Maalum la Maafisa na Askari kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Mbeya, Chuo cha Magereza Kiwira na Chuo cha Ufundi Mbeya ambapo Baraza hilo limefanyika Desemba 31, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua gwaride la Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kabla ya kuhutubia Baraza Maalum la Maafisa na Askari wa Jeshi hilo lililofanyika katika Viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya leo Desemba 31, 2017

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Friday, October 20, 2017

MAHAFALI YA 14 SHULE YA SEKONDARI BWAWANI

Naibu kamishna wa huduma za urekebishaji Magereza Tusekile Mwaisabila akimkabidhi cheti na fedha tasilimu mwanafunzi alie fanya vizri katika mitahani wa kujipima kidato cha nne Elizabert Victor katika mahafali ya 14 yalio fanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari bwawani mkoa wa Pwani.
Naibu kamishna wa huduma za urekebishaji magereza Tusekile Mwaisabila akiangalia maktaba ya shule ya sekondari bwawani inayo milikiwa na Jeshi la Magereza katika mahafali ya 14 ya shule hiyo yalio fanyika jana katika viwanja vya shule hiyo mkoani Pwani
Naibu kamishna wa huduma za urekebishaji magereza Tusekile Mwaisabila akipata maelekeokutoka kwa mwanafunzi wa shule ya bwawani sekondari kuhusiana na matengenezo ya komputa katika mahafali ya 14 ya shule hiyo yaliofanyika jana.
Wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Bwawani wakitumbuiza hadhira iliyo hudhuria katika mahafali ya 14 ya shule hiyo jana ambapo mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Naibu kamishna wa huduma za urekebishaji Tusekile Mwaisabila kutoka Makao Makuu ya Magereza
Naibu kamishna wa huduma zaurekebishaji magereza Tusekile Mwasabila akiwa kaitka picha ya pamoja na hitimu wa kidato cha nne katika mahafali ya 14 ya shule hiyo yalio fanyika katika jana mkoani Pwani 

NA: CPL. MFAUME

Naibu kamishna wa huduma za urekebishaji magereza amepongeza walimu na bodi ya shule kwa ushirikiano mzuri kwa kujidhatiti  katika kuimasha na kuboresha  miundombinu  katika Shule yasekondari Bwawani kama vile madarasa, maabara ya kisasa, mabweni na afya bora ya mwanafunzi aliyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba yake kwa niaba ya kamishna jenerali wa magereza katika mahafali ya 14 shulen I hapo jana.

Aidha aliwasihi wazazi waweze kulipa ada kwa wakati na kuwaruhusu mapema wanafunzi kurudi shuleni pindi wamalikazo likizo zaoili walimu waweze kwenda na muhutasari iliopo.


Friday, October 13, 2017

MAGEREZA YAPIGWA "JEKI" VIFAA TIBA au MAREKENI YAMWAGA VIFAA TIBA KWA MAGEREZA

Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkurugenzi, Ofisi ya Afya ya Shirika na Misaada la Marekani (USAID) Bi. Laurel Fain (wa pili kulia) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Gereza la Mahabusu Segerea tayari kwa hafla ya makabidhiano ya vifaa Tiba leo tarehe 13.10.2017
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akipokea hati ya makabidhiano ya Vifaa Tiba kutoka kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Afya ya Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bi. Laurel Fain katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika leo tarehe 13.10.2017 katika viawanja vya Gereza la Mahabusu Segerea Jijini Dar Es Salaam.
Mwonekano wa sehemu ya vifaa tiba vya aina tofauti tofauti vilivyokabidhbiwa leo kwa Jeshi la Magereza Tanzania Bara na Chuo cha Mafunzo Zanzibar kutoka serikali ya Marekeni kupitia Asasi ya JSI/AIDSFree. Vifaa hivyo vyenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 1.3 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 2 fedha za Kitanzania vitasambazwa katika Zahanati za Magereza nchini, Vyuo vya Mafunzo Zanzibar na hospitali Mpya ya Jeshi la Maagereza inayojengwa sasa eneo  la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Afisa Muuguzi Staff Sajin wa Magereza Recho Komakoma (kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) jinsi kitanda cha kisasa cha kujifungulia (delivery kit) kinavyofanya kazi. Kitanda hicho ni sehemu ya vifaa mbalimbali vya tiba vilivyokabidhiwa leo tahere 13.10.2017 kutoka Serikali ya Marekani kupitia USAID chini ya Mradi wa JSI/AIDSFree. Wa kwanza kulia ni Naibu Kamishna wa Mafunzo Zanzibar Haji Omar.
Mkaguzi wa Magereza Dr. Abdilatif Mkingule (kushoto) ambaye ni daktari kutoka Zahanati ya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga akitoa maelezo ya matumizi ya mashine ya uchunguzi (surgical microscope) wa magonjwa ya koo,pua masikio na macho  katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika leo tarehe 13.10.2017 katika viawanja vya Gereza la Mahabusu Segerea Jijini Dar Es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akiwahutubia wageni waalikwa pamoja na maofisa na askari wa Jeshi la Magereza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka serikali ya Marekani kupitia Asasi ya misaada ya USAID, JSI/AIDSFree iliyofanyika leo tarehe 13.10.2017 katika viwanja vya Gereza la Segerea jijini Dar es salaam. Kamishna Malewa alizishukuru serikali ya Marekani kupitia Asasi ya USAID, AIDSFree, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano wanaoutoa katika kuboresha huduma za Afya ndani ya Jeshi la Magereza.
Mkurugenzi Mkaazi wa JSI/AIDSFree Dr. Beati Mboya akitoa maneno mafupi ya ufunguzi katika hafla ya Makabidhiano ya vifaa tiba kwa Jeshi la Magereza na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar. Dr. Mboya Ameiambia hadhira kuwa Asasi yake imekuwa nchini Tanzania tangu mwaka 2015 ikivijengea uwezo vituo vya Afya katika Jeshi la Magereza na Polisi kwa kuimarisha ubora wa huduma zao hasa katika magonjwa ya Ukimwi na Kifua Kikuu.Kwamba walengwa ni wafanyakazi katika taasisi hizi, familia zao, wafungwa,mahabusu na jamii nzima inayozunguka maeneo hayo.
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza (hayupo picha) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka Serikali ya Marekani kupitia Asasi ya USAID JSI/AIDSFree. Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 13.10.2017 katika viwanja vya Gereza Segerea Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi,Ofisi Ya Afya Bi. Laurel Fain kutoka USAID akitoa hotuba katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa Tiba kwa Jeshi la Magereza kutoka Serikali ya Marekeni kwa Jeshi la Magereza nchini.
Baadhi ya askari wa gereza la Mahabusu Segerea waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhiana vifaa tiba kutoka serikali ya Marekani kupitia Asasi ya USAID JSI/AIDSFree iliyofanyika leo tarehe 13.10.2017 jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (katikati) katika picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa Asasi ya JSI/AIDSFree waliosimama. Waliokaa kutoka kuli ni Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama na Naibu Kamishna wa Mafunzo Haji Omar kutoka Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Mkaazi wa JSI/AIDSFree Dr. Beati Mboya na Mkurugenzi, Ofisi ya Afya wa USAID Bi. Laurel  Fain.

Wednesday, September 13, 2017

FOMU ZA UN AFRIKA YA KATI

Maafisa waliopewa maelekezo ya kujaza fomu za UN Afrika ya kati wajaze fomu hizo hapa chini na wazitume kama walivyoelekezwa.

  1. Annex 1: United Nations Personal History Profile for Government Provided Corrections Personnel
  2. Entry Medical Examination
  3. MINUSCA P5 Senior Corrections Officer

Friday, September 8, 2017

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, DKT JUMA MALEWA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA, MKOANI KILIMANJARO

Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao (kulia) akikabidhi misaada ya kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani nchini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa. Hafla fupi ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Septemba 08, 2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi wakati wa hafla ya kupokea misaada ya kibinadamu kwa Wafungwa waliopo Magerezani iliyotolewa na Asasi ya "New Life In Christ" leo Septemba 08, 2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga - Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Doricas Aide International - Tawi la Tanzania, Bi. Lilian Urasa akitoa maelezo mafupi namna Shirika linavyoshirikiana na Serikali katika Nyanja mbalimbali hapa nchini.
Aina mbalimbali ya misaada ya kibinadamu iliyotolewa kwa Wafungwa waliopo Magerezani nchini na Asasi ya "New Life In Christ". Hafla ya Makabidhiano ya misaada hiyo imefanyika leo Septemba 08, 2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akiwakabidhi cheti cha shukrani Viongozi wa Asasi ya "New Life In Christ" kwa kutambua mchango wao kwa niaba ya Jeshi la Magereza Tanzania na Serikali kwa ujumla.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akimsukuma askari ambaye ameketi kwenye Baiskeli Maalum ya kubebea wagonjwa wasiojiweza ambayo ni miogoni mwa vifaa mbalimbali vilivyotolewa kama msaada kwa Jeshi la Magereza na Asasi ya "New Life In Christ"(kushoto) ni Mkurugenzi wa Doricas Aide International anayeshughulikia Miradi ya Afya katika nchi za Africa, Bi. Mirjam Verwij.
Baadhi ya Wakuu wa Magereza waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia kwa umakini hafla ya tukio hilo kama inavyoonekana katika picha.
Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Julius Sangu’udi(wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Magereza Mkoa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga na Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Ramadhani Nyamka kama inavyoonekana katika picha.
Wafungwa wa Kike wa Gereza Kuu Karanga, moshi wakionesha mikate na skonsi zinazotengenezwa na wafungwa wa Kike katika gereza hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa programu mbalimbali za urekebishaji magerezani.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja Askari wa Magereza Mkoani Kilimanjaro(waliosimama) pamoja na Viongozi Wawakilishi wa Asasi ya "New Life In Christ" mara baada ya kupokea misaada ya kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani nchini (wa kwanza kushoto) ni Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao(wa pili kushoto) ni Mratibu wa Huduma za Magereza toka Asasi ya "New Life In Christ", Bw. Charles Shang'aa (wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Khamis Nkubasi( wa tatu kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche. 

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Tuesday, September 5, 2017

KAMISHNA WA FEDHA NA UTAWALA GHASTON K. SANGA APOKEA VIFAA NYA KUHIFADHIA TAKATAKA KUTOKA KWA TAASISI YA MIKOPO YA FAIDIKA.

KAMISHNA WA FEDHA NA UTAWA WA JESHI LA MAGEREZA GHASTON K. SANGA AKIPOKEA BAADHI YA VIFAA VYA KUHIFADHIA TAKATAKA KUTOKA KWA MKURUGENZI WA HUDUMA ZA WATEJA WA FAIDIKA BW. MBUSO DLIMIN ALIPO TEMBELEA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA MAGEREZA.
KAMISHNA WA FEDHA NA UTAWALA WA JESHI LA MAGEREZA GHASTAN K. SANGA AKIWASHUKURU TAASISI YA MUKOPO YA FAIDIKA KWA KULIUNGA MKONO JESHI LA MAGEREZA  KWA KUTUZA MAZINGIRA  AMBAPO FAIDIKA IMETOA MSAA WA VIFAA VYA KUDIFADHIA TAKATAKA.
BAADHI YA MAAFISA WA MAGEREZA WAKIANGALIA KWA MAKINI MAKABIDIANO YA VIFAA VYA KUHIFADHIA TAKATAKA VILIVYO TOLEWA NA TAASISI YA MIKOPO YA FAIDIKA.
BAADHI YA MAAFISA WA MAGEREZA WAKIANGALIA KWA MAKINI MAKABIDIANO YA VIFAA VYA KUHIFADHIA TAKATAKA VILIVYO TOLEWA NA TAASISI YA MIKOPO YA FAIDIKA.
KAMISHNA WA FEDHA NA UTAWALA WA JESHI LA MAGEREZA AKIWA NA BAADI YA MAAFISA WA MAGEREZA NA MAAFISA WA TAASISI YA MIKOPO YA FAIDIKA NA LETSHEGO WALIPOKUJA MAKAO MAKUU YA MAGEREZA KUTOA MSAADA WA VIFAA VYA KUHIFADHIA TAKATAKA.

Saturday, September 2, 2017

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb)  akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mifuko ya Jamii ya PPF na NSSF limeingia ubia katika mradi huo wa uchumi wa viwanda chini ya Kampuni ya MKULAZI.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akiangalia mbegu za miwa kabla ya kuzipanda katika eneo la Shamba la miwa alipowasili Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.
Shamba la miwa katika mradi wa Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa - MKULAZI katika eneo la Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro likiwa limestawi kama inavyoonekana katika picha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba fupi kwa  Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Morogoro, Watendaji wa Kampuni ya MKULAZI pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ufufuaji wa Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro unakamilika kama ilivyopangwa ambapo matarijio ni kuwa Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka.
Maafisa Waandamizi wa PPF na NSSF wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa(hayupo pichani).
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoani Morogoro wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kyaharara akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage(kulia) mara baada ya ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambapo amekagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio akitoa neno la shukurani mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
Ujenzi wa maghala ya kuhifadhia sukari katika mradi wa Kiwanda cha Sukari cha MKULAZI kilichopo Gereza Mbigiri ukiendelea katika hatua mbalimbali kama inavyoonekana katika picha
Wataalam wazalendo ambao wanajitolea katika ujenzi wa mradi wa Kiwanda cha Sukari – MKULAZI Mbigiri wakitambulishwa mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa(hayupo pichani.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).