Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Wednesday, February 26, 2014

Magereza mkoa wa Tanga yaanza maandalizi ya ukarabati wa ofisi mpya za utawala

 Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa pili kulia) akielezea hatua mbalimbali za Maandalizi ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga(wa kwanza kulia) ni Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja alipotembelea kujionea hatua mbalimbali za ukarabati unaoendelea leo Februari 7, 2014 Jijini Tanga.
Muonekano wa mbele wa Jengo la Kikoloni ambalo linalotarajiwa kukarabatiwa kwa ajili ya Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Jengo hilo hapo awali lilitumika kama Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Tanga ambapo hivi sasa Jeshi la Magereza tayari limeanza ukarabati wa jengo hilo. Wa kwanza katika picha ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya akiwa ameongozana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza leo Februari 07, 2014 Jijini Tanga.

Tuesday, February 25, 2014

Kamishna wa Magereza Nchini Zambia ahitimisha ziara yake Tanzania


Kamishna wa Magereza wa Zambia Percy K. Chato akitoa neno la shukrani na kuwaaga maafisa na watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania (hawapo pichani) katika hafla fupi iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake katika Bustani ya Bwalo Kuu Ukonga, Dar es salaam, Februari 13,2014 (Picha zote Insp. Deodatus Kazinja, wa Jeshi la Magereza)

Sunday, February 23, 2014

Kamishna wa Magereza Nchini Zambia atembelea Magereza Tanzania


Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (mwenye suti) akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Paredi maalum (halipo pichani) lililoandaliwa maalum kwa jairi yake katika uwanja wa paredi wa Chuo Cha Maafisa wa Magereza Ukonga.Nyuma yake ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa na mwenye nguo za kijani ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kamishna Msaidizi wa Magereza Erasmus Kundi. Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (mwenye suti)