Thursday, May 30, 2019
WAZIRI LUGOLA AZINDUA BODI MPYA YA SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA MAGEREZA, AWATAKA WAJUMBE KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA MIRADI YA JESHI
5:29 PM
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoa maelekezo kwa wajumbe wa Bodi
mpya ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza, kabla ya kuizindua
Bodi hiyo, jijini Dodoma, leo. Wapili kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Phaustine Kasike.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza kabla ya Waziri
wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (wapili kushoto) kuizindua Bodi mpya ya Shirika la
Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza, jijini Dodoma, leo. Wapili kulia ni
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike, akitoa historia fupi ya
Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi hilo, kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Kangi Lugola (kushoto) kuizindua Bodi hiyo, Jijini Dodoma, leo. Katikati
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Mwenyekiti
wa Bodi Mpya ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, Meja Jenerali Mstaafu,
Raphaeli Muhuga, akitoa neno la shukrani baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo, jijini
Dodoma leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, na
kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kulia), Kamishna Jenerali wa Magereza,
Phaustine Kasike (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi
mpya ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza, baada ya uzinduzi wa
Bodi hiyo, jijini Dodoma leo.
Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Friday, May 17, 2019
KATIBU MKUU WA MAMBO YA NDANI, MEJA JENERALI JACOB KINGU AFUNGUA KIKAO KAZI CHA WAKUU WA MAGEREZA YOTE TANZANIA BARA, LEO MKOANI MOROGORO
7:50 PM
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kushoto) akiwasili katika Viwanja vya
NaneNane, Mkoani Morogoro tayari kwa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa
Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 –
18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kulia ni Kamishna Jenerali
wa Magereza, Phaustine Kasike
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu akihutubia katika Kikao Kazi cha Wakuu wa
Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 –
18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza,
Phaustine Kasike.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu akihutubia katika Kikao Kazi cha Wakuu wa
Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 –
18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza,
Phaustine Kasike.
. Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Usalama, Mhe. Salum Rehani(vazi la
kiraia) akiongea katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara, leo Mei 17, 2019
katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kushoto ni Kamishna Jenerali
wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike
Baadhi
ya Wakuu wa Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi,
Meja Jenerali, Jacob Kingu(hayupo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu baada ya ufunguzi wa Kikao
kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara.