Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, February 24, 2017

JESHI LA MAGEREZA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA NSSF& PPF WAINGIA UBIA RASMI UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI GEREZA MBIGIRI, MOROGORO

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya hafla fupi ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 24, 2017 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya Mkulazi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF, Bw. Nicander Kileo (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) kwa pamoja wakisaini Mkataba wa Makubaliano(Memorundum of Understanding) kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro. Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika leo februari 24, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) na Kaimu Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya Mkulazi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF, Bw. Nicander Kileo(kushoto)wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro.
Maafisa Waandamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF wakifuatilia  hafla ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo kama inavyoonekana katika picha
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF, Bw. William Erio akizungumza katika hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo kama inavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara akizungumza katika hafla fupi ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF & PPF katika ushirikiano wa kufufua Kilimo cha miwa na ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri – Morogoro.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandandamizi wa Jeshi la Magereza(waliosimama) mara baada ya hafla ya uwekaji saini wa Mkataba wa Makubaliano hayo(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF, Bw. William Erio(wa pili toka kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Thursday, February 23, 2017

UJUMBE WA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA - NDC WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA MAGEREZA, JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(meza kuu) akiongea na ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa. Ujumbe huo wa Washiriki wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza hapa nchini leo Februari 23, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akisisitiza jambo kwa Maafisa kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akitoa utambulisho mfupi kwa Wakufunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania alioambatananao katika ziara ya mafunzo.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo hayo kama inavyoonekana katika picha
Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakipata maelezo mafupi toka kwa Wataalam wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya mafunzo katika Kiwanda cha Seremala Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akijalibisha kiti Maalum cha kunesa kilichotengenezwa kwa ustadi mkubwa katika Kiwanda cha Seremala Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novart akiwasilisha mada yake ya uchokozi kuhusu Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele ya Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(hawapo pichani).
Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akikabidhi zawadi kwa Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya(kushoto) mara baada ya uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa(wa sita toka kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania walipofanya ziara ya mafunzo waliyoifanya katika Jeshi la Magereza(wa nne toka kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)

Thursday, February 16, 2017

MAGEREZA WAZINDUA MAZOEZI YA VIUNGO JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (mwenye kofia) akiongoza watumishi  wa Makao Makuu ya  Jeshi la Magereza katika uzinduzi wa mazoezi ya viungo, uzinduzi huo ulifanyika katika ufukwe wa Bahari ya Hindi. Wa tatu kulia Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Mallya
Baadhi ya maafisa, askari na watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Dkt. Juma Malewa (wa tatu kushoto) pamoja na Naibu Kamishna  wa Magereza (DCP) Edith Mallya (wa nne kulia) katika kufanya mazoezi ya viungo ufukweni mwa Bahari ya Hindi 
Sehemu ya maafisa, askari na watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika mazoezi ya viungo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ufanyaji wa mazoezi ya viungo kwa watumishi wa Jeshi hilo, mazoezi ya viungo hufanyika mara mbili kwa wiki siku ya Jumatano na Ijumaa kuanzia saa 10 jioni.
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga  (wa pili kushoto) akiwa pamoja na watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika uzinduzi wa mazoezi ya viungo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jijini Dar es salaam. 
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (mwenye kofia) akiongoza uzinduzi wa zoezi la ufanyaji wa mazoezi ya viungo kwa maafisa, askari na watumishi raia katika ufukwe wa Bahari ya Hindi mwishoni mwa juma.
Baadhi ya watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika mazoezi ya kunyoosha viungo siku ya uzinduzi wa zoezi la ufanyaji mazoezi ya viungo kwa Jeshi hilo.

Sehemu ya watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika mazoezi ya kunyoosha viungo siku ya uzinduzi wa zoezi la ufanyaji mazoezi ya viungo yalizinduliwa mwishoni mwa juma katika ufukwe wa Bahari ya Hindi mwishoni mwa juma.

(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Magereza).

Tuesday, February 7, 2017

RAIS MAGUFULI AMUAPISHA MKUU MPYA WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI KAMISHNA JENERALI DKT. JUMA ALLI MALEWA

Mkuu Mpya wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali Dkt.Juma Alli Malewa akila kiapo mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam februari 6, 2017.
Mkuu Mpya wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali Dkt.Juma Alli Malewa akipokea miongozo na vitendea kazi kutoka kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam februari 6, 2017.
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto walioketi) akiwa na Maafisa Waandamizi wa Magereza wakifuatilia hafla ya hafla ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam februari 6, 2017

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Monday, February 6, 2017

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA APOKELEWA KWA KISHINDO MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokelewa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo baada ya kuapishwa rasmi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokea salaam ya heshima toka katika Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari(hawapo pichani) kwa ajili yake kwa heshima.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake kwa heshima kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(kulia) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kabla ya kuongea na Maafisa na askari wa Jeshi hilo Makao Makuu ya Magereza mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongea na Maafisa, askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
Sehemu ya familia ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa waliohudhuria kuapishwa kwake leo Ikulu, Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja(katikati) ni Mke wa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Bi. Fatuma Malewa.