Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, November 13, 2015

Naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi atembelea makao makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dar

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Novemba 13, 2015.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo(katikati). Naibu Katibu Mkuu  yupo katika ziara ya kikazi katika Idara mbalimbali zinazounda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Stephen Pancras.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo akiongea na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza maelekezo ya kiutendaji kazi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimkabidhi taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo mara baada ya kufanya kikao kazi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wandamizi wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo leo Novemba 13, 2015( wa tatu kutoka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga.

Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza