Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Thursday, March 19, 2020

TAARIFA KWA UMMA


TAARIFA KWA UMMA


Tuesday, March 17, 2020

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA (NUU) YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MRADI WA UJENZI WA KIWANDA CHA USEREMALA GEREZA MSALATO ILI KUONA HALI YA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO LEO TAREHE 17 MACHI 2020

Katibu Mkuu Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi ndugu Christopher D. Kadio(wannetokakushoto) akimkaribisha Mkuu wa Msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,ambaye ni  Mbungewa Zanzibar Jimbo la Uzini ndugu Salum Rehani (wannetokakulia) walipowasili eneo la Mradi, Msalato. WatatutokakushotoniK amishna Jenerali wa Magereza Seleman Mzee.

Katibu Mkuu Wizara Ya Mambo ya Ndani ya Nchi ndugu Christopher D. Kadio akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Msafara kuzungumza na viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na Mafundi wa mradi

    Mkadiriaji Mkuu wa Ujenzi Makao Makuu ya Magereza Kamishna Msaidizi  Aron Lunyungu akitoa maelezo ya ramani ya mradi kwa Mkuu wa Msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,ambaye ni Mbunge wa Zanzibar Jimbo la Uzini ndugu Salum Rehani.

Msimamizi Mkuu wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Useremala Gereza Msalato Mrakibu Mkandarasi Bonanza Malata akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama( Picha zote na Jeshi la Magereza)