Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Tuesday, September 29, 2015

Taarifa kwa umma kuhusu ajira katika Jeshi la Magereza zilizosambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii

Hii ni taarifa ya kukanusha kuhusiana na tangazo la ajira katika Jeshi la Magereza ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi na Uongozi wa Jeshi kwa ujumla.

Bofya hapa kupata taarifa kamili

Friday, September 18, 2015

Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi azindua huduma za "Duty Free Shop" magereza mkoani Arusha

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(wa pili kushoto)akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Huduma za Magereza Duty free shop Mkoani Arusha leo Septemba 18, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Arusha(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Smart LTD, Bw. Mohamed Panjwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(kulia)akisoma jiwe la Msingi kwenye hafla ya uzinduzi wa Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi wakati wa kumkaribisha Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Huduma za Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha.
Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Magereza mbalimbali yaliyopo Mkoani Arusha wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbaraka Abdulwakil(hayupo pichani).
 Bidhaa za majumbani zinazopatikana katika Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Arusha waliosimama mara tu baada ya kuzindua Huduma za Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, SACP. Hamis Nkubasi(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, SACP. Venant Kayombo(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Mart LTD, Bw. Mohamed Panjwani


Na Lucas Mboje, Arusha
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil amepongeza kasi ya Utendaji kazi wa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja pamoja na Uongozi wote wa Jeshi hilo kwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa mpango wa Serikali ya Awamu ya Nne wa kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa Maafisa, askari Magereza na familia zao katika maeneo yao ya kazi hususani huduma za "Duty free shops".
Mhe. Mbarak Abdulwakil ameyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa "Duty free shop"ya Magereza Mkoani Arusha iliyofanyika leo Septemba 18, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Arusha ambapo baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Binafsi wa Mkoa wa Arusha walihudhuria hafla hiyo.
"Nampongeza kwa dhati Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja kwa jitihada hizi ambapo matunda yake yanaonekana na amethibitisha kwamba azma ya kusambaza huduma hii nchi nzima ipo pale pale na jitihada zinaonekana". Alisema Abdulwakil.

Ameongeza kuwa lengo la Mpango huu ni kuhakikisha kuwa ustawi wa maisha ya Maafisa na Askari wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama unatekelezwa ipasavyo kwa kuwapatia bidhaa zenye bei nafuu ili kuwapunguzia ukali wa maisha.

Aidha, Mhe. Abdulwakil amewaasa Maafisa na askari watakaotumia huduma husika kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu pamoja na maadili ya uendeshaji wa maduka hayo ili kuhakikisha kuwa adhima ya Serikali ya kuwapunguzia makali ya maisha Maafisa, askari pamoja na familia zao wananufaika ipasavyo na si vinginevyo.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi,Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja alisema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Kampuni ya Dar Mart LTD limeazimia kusambaza huduma za Duty Free Shop nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari.

Kamishna Jenerali Minja alimhakikishia Mgeni rasmi kuwa maduka hayo yataendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za "Duty Free Shop" na akasema kuwa hata sita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na askari watakao kwenda kinyume na uendeshaji wa huduma hizo.

Hivi sasa Jeshi la Magereza limefanikiwa kuzindua jumla ya "Duty Free Shops" tisa(09) ikiwemo Gereza Kuu Ukonga na Keko - Dar es Salaam, Gereza Isanga - Dodoma, Gereza Kuu Karanga - Moshi, Gereza Butimba - Mwanza, Gereza Ruanda - Mbeya, Gereza Lilungu - Mtwara, Gereza Uyui - Tabora, Chuo KPF - Morogoro na duka la tisa(09) ni Gereza Kuu Arusha.


(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Friday, September 4, 2015

Kamishna wa sheria na uendeshaji wa magereza afunga rasmi kongamano la wasaidizi wa kisheria magerezani mkoani Morogoro

Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye hafla ya ufungaji wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la Envirocare ambapo Kongamano hilo limefanyika kwa siku tatu kuanzia Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema akitoa neno la shukrani kwa Washiriki kabla ya kumkaribisha Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza kufunga Kongamano hilo.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akiwa ameongozana na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(kushoto) tayari kwa ufungaji rasmi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria ambalo limefanyika Mkoani Morogoro kuanzia Septemba 02 - 04, 2015

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Thursday, September 3, 2015

Jeshi la Magereza nchini kushirikiana na asasi za kiraia katika kupunguza msongamano magerezani

Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kutoka Magereza Mkoani tanga wakiendelea na majadiliano katika Kongamano hilo linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku tatu.

Na, Lucas Mboje, Morogoro

Jeshi la Magereza nchini limeahidi kuendelea kushirikiana na Asasi ya Envirocare katika kuimarisha Madawati ya Msaada wa Kisheria Magerezani ili kuleta tija katika utatuzi wa changamoto ya Msongamano wa Mahabusu inayolikabili Jeshi hilo.

Kauli hiyo imetolewa jana Mkoani Morogoro na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja alipokuwa Mgeni rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani na Mahabusi za Watoto.

Jenerali Minja amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukulia kwa uzito stahiki suala la Msongamano wa Mahabusu Magerezani ikiwemo kushirikiana na Wadau wa Haki Jinai katika kupunguza changamoto ya Msongamano wa Mahabusu Magerezani.

"Napenda kutoa rai kwa Asasi zingine zenye malengo yanayofanana na Asasi hii nazikaribisha kuja kufanya kazi na Jeshi la Magereza kwani mwelekeo wa Jeshi kwa sasa ni Urekebishaji wa Wafungwa(From Prisons to Corrections) ambapo Jeshi la Magereza watafanya kazi kwa karibu na Asasi za Kiraia na Jamii kwa ujumla". Alisema Jenerali Minja.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Envirocare, Bi. Loyce Lema amesema kuwa imekuwa ni faraja kwao kupata ushirikiano kama huo kutoka Jeshi la Magereza kwani umewezesha kutekelezwa kwa mradi huo wa kutoa Msaada wa Kisheria kwa Mahabusu waliopo Magerezani kwa matokeo chanya kwa muda mufupi.

Bi. Lema alisema kuwa mradi huo umetekelezwa kwa miaka mitatu(2012 - 2015) na umetekelezwa kwenye Magereza 20 na Mahabusu 04 za Watoto katika Mikoa 05 ambayo ni Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam.

Asasi ya Envirocare kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza ilifanya utafiti wa awali wa kuangalia hali halisi ya Msongamano katika Magereza yaliyopo katika Mikoa mitano ya mradi. Matokeo ya jumla ya utafiti huo yalionesha kuwa kuna tatizo kubwa la Msongamano ambao unasababishwa na idadi kubwa ya Mahabusu katika Magereza ya Mikoa hiyo.

Wednesday, September 2, 2015

Kamishna Jenerali wa Magereza afungua rasmi kongamano la wasaidizi wa kisheria magerezani mkoani Morogoro

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye ufunguzi wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la Envirocare ambapo Kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Meza Kuu wakimsikiliza Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani - Jeshi la Polisi, Kamisheni ya Upelelezi, Mrakibu wa Polisi Emmy Mkonyi(hayupo pichani). Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bw. Joseph Ndunguru(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema akitoa maelezo mafupi ya lengo la Kongamano hilo ambalo ni kutoa msaada wa Kisheria Magerezani ili kupunguza Msongamano Magerezani.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza baada ya kukabidhi cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwa mmoja wa Washiriki wa Kongamano hilo linalofanyika Mkoani Morogoro.
Mwandishi wa Habari wa ITV, Bi. Devotha Minja akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja mara baada ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria katika Viwanja vya Ukumbi wa CCT uliopo Mkoani Morogoro(wa pili kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(kulia) ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Jeshi la Polisi, Mrakibu wa Polisi Emmy Mkonyi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) walioketi akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria kutoka Mikoa Mitano ya Magereza Tanzania Bara(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato Rugainunula(wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Joseph Ndunguru(wa kwanza kushoto) ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Jeshi la Polisi, Mrakibu wa Polisi, Emmy Mkonyi(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).