Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Wednesday, August 15, 2018

Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa Apongeza Jeshi la Magereza.

Rais Mstaafu Benjamini Mkapa Akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la  Magereza Nanenane Mkoa wa Simiyu.

Asp Yunge Saganda akimpa Maelezo ya Bidhaa za Ngozi  Rais Mstaafu Benjamin Mkapa



Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Akiangalia Bidhaa za Nafaka zinazozalishwa na Jeshi la Magereza katika Mkakati wake wa Kujitosheleza kwa Chakula.

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akikagua Samani zinazotengenezwa na Jeshi la Magereza katika Programu zake za Urekebishaji wa Wafungwa.

Wednesday, August 8, 2018

WAZIRI WA KILIMO DK. TIZEBA ATEMBELEA BANDA LA MAGEREZA KWENYE UFUNGUZI WA NANE NANE SIMIYU NA KUHIMIZA UFUGAJI NA KILIMO CHENYE TIJA KWA MAENDELEO YA VIWANDA.

Waziri Kilimo Dk. Charles Tizeba akisalimiana na Mkuu wa Kilimo,Mifugo na Utunzaji wa Mazingira wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi  Mlasani Deodathy Kimaro ,katikati yao ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mataka na wa pembeni kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi Kimaro ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi  Shaku Umuya Umba.

Waziri wa Kilimo Dk. Tizeba akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kukaribishwa kwenye banda la Magereza kwenye ufunguzi wa nane nane ambayo inayafanyika Kitaifa Nyakabindi,Bariadi  Mkoani  Simiyu.

Sajini Caroline William Mtolela wa Jeshi la Magereza akimuelimisha Dk. Tizeba jinsi ya kutunza mazingira kwa kutengeneza mkaa nafuu wa taka ngumu.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndugu Adam Malima akifurahia jambo na Waziri wa Kilimo Dk. Tizeba walipokuwa wakipata maelezo kwenye banda la uzalishaji uyoga lililo kwenye eneo la Magereza.

Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Hussein Nyembo akimuelezea Dk. Charles Tizeba uhifadhi bora wa malisho ya mifugo.

Mrakibu Msaidizi wa Magereza Yunge Saganda akimuonesha na kumuelezea Dk. Charles Tizeba utengenezaji na upatikanaji wa bidhaa za ngozi katika Jeshi la Magereza, mwenye miwani katikati yao ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega

KAMISHNA WA HUDUMA ZA PAROL,VIWANDA,HUDUMA ZA JAMII NA PROGRAMU ZA UREKEBISHAJI AF. MBOJE ATEMBELEA BANDA LA MAGEREZA NA KUJIONEA MAZAO NA BIDHAA MBALIMBALI ZITOKANAZO NA UREKEBISHAJI WA WAFUNGWA.

 Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Augustine Mboje  Sangalali(suruali nyeupe) akisalimiana na Mkuu wa Kilimo,Mifugo na Utunzaji wa Mazingira, Kamishna Msaidizi  Mwandamizi wa Magereza Mlasani Deodath Kimaro, alipotembelea Banda la Magereza katika maonesho ya Nane nane yanayofanyika Kitaifa Nyakabindi,Wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.

Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Mboje akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda la Magereza kwenye Nane nane inayofanyika Nyakabindi,Bariadi Mkoani Simiyu.

   Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Mboje akipata maelezo ya jinsi ya Utunzaji wa Mazingira toka kwa Staff sagin Petro Thomas alipotembelea banda la Magereza kwenye Nane nane inayofanyika    Nyakabindi,Bariadi Mkoani Simiyu.

Sagin Caroline Mtolera wa Jeshi la Magereza akimuelezea Af. Kamishna Mboje namna ya kutunza mazingira kwa kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya taka ngumu.

Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Binamungu Rwetela wa Jeshi la Magereza akimuelezea  Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Mboje namna ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya aina mbalimbali ambayo kwa kiwango kikubwa imepandwa katika Magereza mbalimbali nchini.