Wednesday, August 8, 2018

KAMISHNA WA HUDUMA ZA PAROL,VIWANDA,HUDUMA ZA JAMII NA PROGRAMU ZA UREKEBISHAJI AF. MBOJE ATEMBELEA BANDA LA MAGEREZA NA KUJIONEA MAZAO NA BIDHAA MBALIMBALI ZITOKANAZO NA UREKEBISHAJI WA WAFUNGWA.

 Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Augustine Mboje  Sangalali(suruali nyeupe) akisalimiana na Mkuu wa Kilimo,Mifugo na Utunzaji wa Mazingira, Kamishna Msaidizi  Mwandamizi wa Magereza Mlasani Deodath Kimaro, alipotembelea Banda la Magereza katika maonesho ya Nane nane yanayofanyika Kitaifa Nyakabindi,Wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.

Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Mboje akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda la Magereza kwenye Nane nane inayofanyika Nyakabindi,Bariadi Mkoani Simiyu.

   Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Mboje akipata maelezo ya jinsi ya Utunzaji wa Mazingira toka kwa Staff sagin Petro Thomas alipotembelea banda la Magereza kwenye Nane nane inayofanyika    Nyakabindi,Bariadi Mkoani Simiyu.

Sagin Caroline Mtolera wa Jeshi la Magereza akimuelezea Af. Kamishna Mboje namna ya kutunza mazingira kwa kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya taka ngumu.

Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Binamungu Rwetela wa Jeshi la Magereza akimuelezea  Kamishna wa Huduma za Parol,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Mboje namna ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya aina mbalimbali ambayo kwa kiwango kikubwa imepandwa katika Magereza mbalimbali nchini.