Wednesday, August 8, 2018

WAZIRI WA KILIMO DK. TIZEBA ATEMBELEA BANDA LA MAGEREZA KWENYE UFUNGUZI WA NANE NANE SIMIYU NA KUHIMIZA UFUGAJI NA KILIMO CHENYE TIJA KWA MAENDELEO YA VIWANDA.

Waziri Kilimo Dk. Charles Tizeba akisalimiana na Mkuu wa Kilimo,Mifugo na Utunzaji wa Mazingira wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi  Mlasani Deodathy Kimaro ,katikati yao ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mataka na wa pembeni kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi Kimaro ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi  Shaku Umuya Umba.

Waziri wa Kilimo Dk. Tizeba akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kukaribishwa kwenye banda la Magereza kwenye ufunguzi wa nane nane ambayo inayafanyika Kitaifa Nyakabindi,Bariadi  Mkoani  Simiyu.

Sajini Caroline William Mtolela wa Jeshi la Magereza akimuelimisha Dk. Tizeba jinsi ya kutunza mazingira kwa kutengeneza mkaa nafuu wa taka ngumu.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndugu Adam Malima akifurahia jambo na Waziri wa Kilimo Dk. Tizeba walipokuwa wakipata maelezo kwenye banda la uzalishaji uyoga lililo kwenye eneo la Magereza.

Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Hussein Nyembo akimuelezea Dk. Charles Tizeba uhifadhi bora wa malisho ya mifugo.

Mrakibu Msaidizi wa Magereza Yunge Saganda akimuonesha na kumuelezea Dk. Charles Tizeba utengenezaji na upatikanaji wa bidhaa za ngozi katika Jeshi la Magereza, mwenye miwani katikati yao ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega