Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Saturday, January 30, 2016

Naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi, balozi Yahya aridhishwa na uzalishaji wa mifugo katika shamba la mifugo la gereza Mtego wa Simba, mkoani Morogoro

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Magereza alipotembelea  Gereza la uzalishaji mifugo Mtego wa Simba lililopo Mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Gereza la uzalishaji mifugo Mtego wa Simba. Kulia ni Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Omari Msepwa.
Mtaalamu wa Mifugo katika shamba la uzalishaji mifugo katika Gereza la Mtego wa Simba Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Constatus Magori akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya( kushoto)alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji  zinazofanywa gerezani hapo.
Kundi la ng’ombe wa maziwa wanaofugwa katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba wakiwa malishoni kama wanavyoonekana katika picha.
Mtaalamu wa mifugo katika mradi wa ufugaji kuku wa mayai na nyama uliopo Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, Sajeni taji Sarah Kabunda akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya(kushoto) alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji  zinazofanywa gerezani hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya(wa pili kutoka kushoto), akiangalia mojawapo  ya mashuka yanayofumwa kwa ustadi mkubwa na wafungwa wa kike katika  Gereza Kuu la Wanawake Tanzania- Kingolwira, lililopo mkoani Morogoro.

(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi atembelea mradi wa umwagiliaji gereza la kilimo Idete, mkoani Morogoro

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mhe. Balozi Simba Yahya akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili gerezani hapo kwa ziara ya kikazi Januari 29, 2016 kujionea ujenzi wa mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete lililopo Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro(anayefuatia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(wa pili kulia) akiwa ameongozana na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) kuelekea katika Ukumbi wa Gereza hilo kwa ajili ya kupata taarifa kamili ya utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kutoka kwa Wakandarasi wa mradi na Mshauri Mwelekezi mradi(kulia) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Yahya Sinaniya.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya akiangalia sehemu ya banio la kutunzia maji ya mradi wa Gereza la Kilimo Idete akiwa pamoja na msafara wa Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Manyama Mapesi(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Muonekano wa mfereji wa maji yatakayokuwa yakitumika katika mradi wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete, Mkoani Morogoro kama inavyoonekana katika picha.
Mshauri wa Mradi, Mhandisi Nzobonaliba Imani akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(katikati) alipotembelea mradi wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete lililopo Mkoani Morogoro(kulia) ni Mkuu wa Gereza hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja wakiaangalia ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza hilo.
Wakandarasi wa Kampuni ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza Kilimo Idete, lililopo Mkoani Morogoro wakiendelea na ujenzi wa mifereji ya maji kama inavyoonekana katika picha.
Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata maelezo ya Kitaalam kutoka kwa Mshauri Mwelekezi walipotembelea mradi huo kujionea hatua mbalimbali za ujenzi. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kilombero.


Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Morogoro

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya "Tanzania Building Works ya Jijini, Dar es Salaam" inayojenga mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kuukamilisha mradi huo katika muda walioongezewa ili kuwezesha kuanza kwa shughuli za uzalishaji gerezani hapo.

Akizungumza na Wakandarasi wa Kampuni hiyo alipofanya ziara ya kikazi Gereza Idete, Balozi Yahya amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mkombozi kwa Jeshi la Magereza kwani utawezesha uzalijashi wa chakula cha kutosha cha wafungwa waliopo magerezani pamoja na kuzalisha ziada itakayouzwa kwa Wananchi ili kuongeza Mapato Serikalini.

"Ni matarajio yangu kuwa Mkandarasi wa Mradi huu kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi na Wadau wa Jeshi la Magereza atakamilisha mradi huu kwa wakati kama alivyotuahidi hivyo kuanza mara moja shughuli za uzalishaji". Alisisitiza Balozi Yahya.

Naye Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Lodia Mallion alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo tayari uchimbaji na ujenzi wa mifereji itakayokuwa ikipitisha maji kwenda mashambani imekwisha kukamilika.

"Mito inayotumika kama vyanzo vya maji ni mto Kilombero pamoja na mto Kiwiliwili ambapo banio linalotunza maji kwa shughuli za umwagiliaji tayari limekamilika". Alisikika Mhandisi Mallion.

Awali Mkuu wa Gereza Idete, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja akiwasilisha taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Yahya amesema kuwa kazi ya kuandaa mradi huu ilianza rasmi mwaka 2013 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka huu 2016 ambapo gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha Tsh. 2.5 Bilioni.

Aidha amesema kuwa chakula kitakachopatikana katika mradi huo wa Gereza Idete kitatumika kulisha wafungwa waliopo magerezani na ziada itakayopatikana itauzwa kwa Wananchi hivyo kuongeza pato la Taifa.

Gereza la Kilimo Idete lipo Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro linajishughulisha na Kilimo cha mpunga wa chakula na pia mpunga kwa ajili ya mbegu bora za Kilimo hapa nchimi. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1983 kwa ajili ya Kilimo cha mazao mbalimbali hususani Kilimo cha mpunga.

Thursday, January 21, 2016

Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu mambo ya ndani yanchi wafanya ziara jeshi la magereza, walipongeza kwa utendaji mzuri wa kazi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali (CGP), John Minja wakati alipokuwa anawasili ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katibu Mkuu Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga, na anayefuata ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi hilo, Dk Juma Malewa.  
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali (CGP), John Minja akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Magereza wakiongozwa na Kamishna Jenerali, John Minja (kushoto meza kuu) wakati Katibu Mkuu na Naibu wake walipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Meja Jenerali Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamanda wa Jeshi la Magereza wakiongozwa na Kamishna Jenerali, John Minja (wapili kulia) wakati Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo walipofanya ziara ya kikazi ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Balozi Simba alilitaka jeshi hilo wawatumie wafungwa wenye makosa madogomadogo kama nguvu kazi ili waongeze uzalishaji ndani ya jeshi hilo.  
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) taarifa ya kiutendaji ya Jeshi hilo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Viongozi hao wa Wizara walifanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Makao Makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo.

Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi