Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Tuesday, June 30, 2015

Waziri Chikawe azindua kikosi kazi cha kupambana na uhalifu wa mazingira nchini

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Katika hotuba yake IGP Mangu aliomba ushirikiano na wananchi katika kupambana na uharibifu  wa mazingira nchini. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.  Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Utunzaji wa Mazingira (ICCF) la nchini Marekani, Dk Kaush Arha akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali nchini pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana na uhalifu wa kimazingira kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu nchini. Uuzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu.

Viongozi mbalimbali wa Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.

Viongozi mbalimbali wa Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.

Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Saturday, June 27, 2015

Rais Kikwete mgeni rasmi siku ya Magereza, afunga rasmi mafunzo ya uofisa ngazi ya juu ya Jeshi la Magereza, jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Casmir Minja akimkarisha Rais Jakaya Kikwete (kushoto) katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufunga mafunzo ya uofisa wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo. Maafisa 104 wa kozi hiyo walihitimu mafunzo hayo na kuvishwa vyeo hivyo. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Casmir Minja akitoa hotuba yake kabla ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo. Katika hotuba yake CGP Minja alisema jeshi lake linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu mkubwa wa nyumba za askari na maafisa Magereza.
Kikosi cha gwaride wa Askari wa Jeshi la Magereza la zamani (askari jela) likionyesha jinsi kipindi cha zamani jeshi hilo lilivyokuwa linafanya gwaride lake katika sherehe na shughuli mbalimbali za Jeshi hilo. Tukio hilo lilifanyika kabla ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo katika sherehe iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride liloandaliwa kwa ajili yake na wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kabla ya kuyafunga mafunzo ya Cheo cha Mrakibu Msaidiziyaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo hayo ambayo yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo alikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.


Rais Jakaya Kikwete (wakumi kushoto-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Maafisa wa Jeshi la Magereza, wahitimu pamoja na wageni waalikwa, baada ya kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi pamoja na kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa ajili ya kuzungumza na askari, maafisa wa Jeshi la Magereza pamoja na wageni waalikwa na baadaye kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo cha Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo. Katika hotuba yake Waziri Chikawe alisema Jeshi hilo linakabiliwa na upungufu mkubwa wa magereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia), akimkarisha Rais Jakaya Kikwete kuketi baada ya kukagua gwaride la wahitimu 104 wa kozi ya Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza kabla ya Rais huyo kuyafunga mafunzo hayo katika sherehe iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
Rais Jakaya Kikwete akimvisha muhitimu Amina Lidenge, Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza kwa niaba ya wenzake 104 waliomaliza mafunzo hayo katika Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo hayo ambayo yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo baada ya kuyafunga aliweza kutembelea mabanda na kuonyeshwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Askari na Maafisa wa Jeshi la Magereza, wageni waalikwa na wananchi wakati akiyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshihilo na kuwatunukia vyeo vya Warakibu Wasaidizi 104. Katika hotuba yake Rais Kikwete aliwapongeza wahitimu hao kwa kutunukiwa vyeo hivyo, na pia aliwataka maafisa wa Jeshi hilo wafuate sheria kwa wawatendea haki Mahabusu na Wafungwa katika magereza nchini.
Kikosi Maalumu cha Ukakamavu cha Jeshi la Magereza (KMKM) kikimuonesha Rais Jakaya Kikwete na wageni waalikwa (hawapo pichani)  jinsi kikosi hicho kinapokuwa kazini wakati wanapopambana na wahalifu wa aina tofauti. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kutoa heshima kwa mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) katika sherehe ya ufungaji wa mafunzo hayo ya Cheo cha Mrakibu Msaidizi  yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wahitimu 104 walivishwa cheo hicho. Ufungaji wa mafunzo hayo yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo Rais KIkwete alikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.
Rais Jakaya Kikwete akiiangalia bilinganya wakati alipokuwa anatembelea mabanda yenye bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Jeshi la Magereza nchini. Rais Kikwete alitembelea maonyesho hayo maalumu yanayofanyika kila mwaka katika Siku ya Magereza, mara baada ya kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo, katika tukio lililofanyika Uwanja wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Kilimo wa Jeshi hilo, Yesaya Kitundu. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na anayefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick. 

Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Friday, June 26, 2015

Taarifa kwa vyombo vya habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Tarehe 27 Juni, 2015 saa 2:00 asubuhi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kufunga Mafunzo ya Uofisa Ngazi ya Juu Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam.

Bofya hapa kupata taarifa kamili

Thursday, June 25, 2015

Wakuu wa Taasisi ya Magereza kutoka nchi za Afrika watembelea kiwanda cha viatu cha gereza kuu Karanga Moshi, mkoani Kilimanjaro

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Botswana, Silas Motlalekgosi akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wa Mkoani Kilimanjaro alipotembelea Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi leo Juni 25, 2015 akiwa na Viongozi Wakuu wa Taasisi za Urekebishaji/ Magereza kutoka Nchi za Swaziland, Uganda, Kenya, Zambia.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Swaziland, Isaya Ntshangase akisaini kitabu cha Wageni alipowasili katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Viongozi hao wa Magereza kutoka Nchi za Afrika wapo ziara ya kikazi nchini Tanzania.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile akitoa utambulisho kwa Ujumbe wa Viongozi wa Magereza kutoka Nchi za Afrika ambao wapo Nchini kwa ziara ya kikazi. Viongozi hao wametembelea Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi.
Wafungwa wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakiwa wanashona viatu aina ya Buti ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini kama wanavyoonekana katika picha wakishona sehemu ya juu ya viatu hivyo. Wafungwa hao wa Gereza Kuu Karanga wananufaika na Stadi ya Ushonaji viatu katika Kiwanda hicho kwa kujipatia ujuzi wa Ushonaji.
Muonekano wa viatu aina ya Buti vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi, viatu hivyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikiwa tayari vimekwishatengenezwa kama vinavyoonekana katika picha.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
    

Monday, June 22, 2015

IGP Mangu afunga rasmi mafunzo ya uongozi wa Magereza daraja la pili jijini Dar

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambayo yamefungwa rasmi leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Mhitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambaye amefanya vizuri kwa upande wa Gwaride, Stafu Sajini Boniphace Felix. Mhitimu huyo amevishwa cheo hicho kwa niaba ya Wahitimu 216 wa Mafunzo hayo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza.
Kikundi cha kwaya kinachoundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga kikitumbuza mbele ya Mgeni rasmi, IGP Ernest Mangu(hayupo pichani)katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi Daraja la Pili, Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali katika sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akifurahia onesho Maalum la Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani(katikati) ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu(kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile wakifurahia onesho hilo kama wanavyoonekana katika picha.
 
Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili wakipita mbele ya Mgeni rasmi IGP Ernest Mangu(hayupo pichani) katika mwendo wa haraka wakitoa heshima leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga. Jumla ya Wahitimu 216 wamehitimu Mafunzo Uongozi Daraja la Pili na kupandishwa cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili(kushoto katika Jukwaa) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Maafisa wa Jeshi la Magereza wakionyesha umahiri mkubwa wa mbinu mbalimbali za kujihami na adui kama wanavyoonekana kikakamavu katika picha wakati wa hafla fupi ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Friday, June 19, 2015

Taarifa kwa vyombo vya habari


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest J. Mangu
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini, IGP Ernest Mangu kufunga mafunzo ya uongozi wa Magereza daraja la pili, jijini Dar.
Bofya HAPA kupata taarifa kamili

Friday, June 5, 2015

Mazishi ya marehemu kamishna mkuu mstaafu wa jeshi la Magereza, Onel Malisa yafanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro

Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiweka jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa kwenye nyumba yake ya milele. Mazishi hayo yamefanyika leo Juni 05, 2015 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa tayari limewekwa kwenye nyumba yake ya Milele.
Askofu Mstaafu Dkt. Martin Shayo wa Diyosisi ya Kasikazini akiweka akiongoza Ibada Maalum ya mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye amefariki Juni 2, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi ka Magereza, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiweka Shada la Maua kwenye kabuli la Marehemu.
Gadi Maalum ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa katika Gwaride la mazishi yake.
Kabuli la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa limepambwa na mashada ya maua baada ya mazishi.
Umati wa watu waliojitokeza katika mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiimba wimbo kwenye Ibada Maalum ya kumuombea kheri Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa baada ya shughuli za mazishi kukamilika(kulia) ni Mchungaji Frank Machanga kutoka Jimbo la Kasikazini.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Thursday, June 4, 2015

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi awaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu kamishna mkuu mstaafu wa jeshi la Magereza, Onel Malisa jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye ameagwa leo Kijeshi Juni 04, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwa mazishi kwao Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Mwili wa Marehemu, Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ukiwa umebebwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza tayari kwa zoezi la kuagwa Kijeshi katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiwa amesimama wakati mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ulipokuwa ukiwasili katika Viwanja vya Chuo Cha Maafisa Magereza Ukonga(katikati) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kulia) ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisaini katika Kitabu cha Maombolezo kabla ya kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu wa Magereza Mstaafu Onel Malisa.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini salaam mbalimbali za rambirambi zilizokuwa zikitolewa katika hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa.
 
Kiongozi Mwakilishi wa Wastaafu wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka akitoa salaam za rambirambi.
Gadi Maalum ya Maafisa wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya paredi la kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa.
 
Umati wa ndugu na Jamaa waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa.