Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, July 21, 2017

WAASTAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA RASMI JIJINI DAR

Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa kwenye gari maalum pamoja na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wao Jeshini. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwapungia mikono Wastaafu wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa kwenye gari maalum pamoja na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakiwapungia mikono Wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza wakifuatilia tukio la kuagwa wastafu hao kama inavyoonekana katika picha.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Magereza, Augustine Mboje alipowasili katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo.
Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi la Magereza likipita mbele ya wastaafu wa Jeshi la Magereza kwa mwendo wa haraka.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa jukwaa kuu wakati Gwaride likipita mbele kwa heshima.
Kamishna wa Fedha na Uatwala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga akisalimiana na Mnadhimu Msaidizi wa Jeshi la Magereza .Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Deogratis Lwanga (wa pili kulia) katika hafla ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo.
Kamishna wa Fedha na Uatwala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga (katikati) akifuatilia matukio ya kuagwa wastaafu wa Magereza, kulia ni  Mnadhimu Msaidizi wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Deogratis Lwanga na wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mlasani Kimaro.
Wastaafu wa Jeshi la Magereza walioagwa leo katika viwanja vya chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga DSM, kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Marcel Lori, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza George Kiria na Kamishna Msaidizi wa Magereza Erasmus Kundy.
Wastaafu wa Jeshi la Magereza (waliosimama nyuma) katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Magereza waliohudhuria hafla ya kuagwa kwao leo tarehe 21 Julai, 2017.  Waliokaa katikati ni Kamishna wa Fedha na Utawala Gaston Sanga, wa kwanza kushoto ni Naibu Kamishna Tusekile Mwaisabila, Naibu Kamishna Uwesu Ngarama na kutoka kulia ni Naibu Kamishna Augustine Mboje na Naibu Kamishna Gedion Nkana.

(PICHA ZOTE na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Makao Makuu ya Magereza)

Saturday, July 15, 2017

WAZIRI MHAGAMA ATEBEMBELEA MRADI WA UWEKEZAJI WA MAGEREZA NA PPF

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) (wa tano kulia) akiwa katika eneo la Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda kipya cha viatu cha Karanga Leather Industries Ltd Karanga Moshi, kinatarajiwa kujengwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF na Jeshi la Magereza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philipo Mpango (Mb) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira. Kiwanda cha viatu Karanga kinatarajiwa kupatiwa teknolojia mpya kutoka PPF itakayokiwezesha kuongeza uzalishaji kutoka Jozi 150 za sasa za viatu hadi jozi 400 kwa siku.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) wa tatu kulia, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philipo Mpango (Mb) (wa pili kulia)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masaun (Mb)  kwa pamoja wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa mafundi wa utengenezaji wa viatu kiwandani hapo leo tarehe 14 Julai, 2017 Karanga Moshi.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philipo Mpango (Mb) akiangalia moja viatu vinavyozalishwa na Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi alipotembelea kiwanda hicho pamoja na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb)   pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masaun (Mb) na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Prof, Adolf Mkenda.leo tarehe 14 Julai, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akichukuliwa vipimo kwa ajili ya kutengenezewa viatu alipotembelea Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi leo tarehe 14 Julai, 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philipo Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masaun wakichukuliwa vipimo vya miguu kwa ajili ya kutengenezewa viatu walipotembelea Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philipo Mpango (Mb) (wa kwanza kushoto) meza kuu akifafanua jambo katika kikao cha ndani kilichofanyika kiwandani Karanga Moshi mara baada yeye na Waziri Jenista Mhagama na Naibu wa Waziri Hamad Masaun kufanya ziara katika eneo la Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda Kipya na Kiwanda cha sasa cha viatu cha Karanga Moshi leo tarehe 14 Julai, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akitoa hotuba fupi kwa wageni waalikwa, baadhi ya viongozi wa Jeshi la Magereza, PPF na Wajumbe wa Bodi ya Karanga Leather Industries Ltd (hawapo pichani) ikiwa ni majumuisho ya ziara yake ya Kutembelea Miradi ya Uwekezaji wa Ubia kati ya Jeshi la Magereza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF, leo katika Ukumbi wa Gereza Karanga Moshi. (Wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt, Juma Malewa na (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu Wa PPF Ndg.William Erio.
Baadhi ya Maafisa  wa Magereza na wafanyakazi wa PPF wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Magereza Karanga Moshi.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mgani Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani) (wa Kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Mwandamizi wa Magereza (SACP) Hamis Nkhubasi na (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Julius Ng’udi
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Karanga Leather Industries Ltd wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi ya uwekezaji kati Jeshi la Magereza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF. (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga.
Picha ya Pamoja ya Mhe. Waziri Jenista Mhagama, (wa nane kulia), Mhe. Dkt. Philip Mgango (wa saba kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masaun (wa sita kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna  Mghwira, (wa nane kushoto) Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa wa tano kulia) Mkurugenzi Mkuu wa PPF Ndg. William Erio (wa tano kushoto) na viongozi wengine waandamizi serikalini.

Tuesday, July 11, 2017

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MUZIKI WA BRASS BAND YA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana alipowasili kwenye hafla ya  kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017(kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa gwaride maalum katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua gwaride maalum katika hafla fupi ya ya kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua Gadi ya wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza wakipita mbele ya jukwaa kwa heshima katika hafla ya kufunga rasmi mafunzo hayo kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa wamesimama kwa heshima kabla ya Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kupita mbele ya jukwaa kwa heshima katika hafla ya kufunga rasmi mafunzo hayo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) akiwa katika jukwaa akifuatilia kwa makini maonesho mbalimbali ya wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Naibu Kamishna wa Magereza Gideon Nkana.
Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza wakionesha onesho maalum la umbo la Mwenge wa Uhuru kama inavyoonekana kaika picha.
Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza wakitoka uwanjani mara baada ya kuonesha maonesho mbalimbali katika hafla fupi ya kufunga rasmi mafunzo hayo. Jumla ya Askari 90 wa Jeshi Magereza wamehitimu mafunzo hayo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wanawake wa  mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza. Walioketi wa pili toka kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga, (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaa, Naibu Kamishna wa Magereza Augustine Mboje, (wa tatu toka kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana, (wa pili toka kulia) ni Boharia Mkuu wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mafunzo Jeshini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Charles Novart.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).