Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Thursday, May 29, 2014

Magereza na GEPF watiliana mkataba wa uwekezaji

Kamishna Jenerali wa Magereza Jonn Minja (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (GEPF) Bw. Daud Msangi (kulia) Alhamis 29, 2014
 Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Bw. Daud Msangi   Mkurugenzi Mkuu wa GEPF (kulia) wakisaini Mkataba wa Uwekezaji baina ya Taasisi hizo mbili leo Alhamis 29 Mei, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Jijini Dar es salaam.
 Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Bw. Daud Msangi   Mkurugenzi Mkuu wa GEPF (kulia) wakikabidhiana nyaraka za makubaliano ya uwekezaji baada ya kutiwa sahini.leo Alhamis 29 Mei, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Jijini Dar es salaam
 Mkuu wa Shirika la Magereza ( Prisons Corporation Sole) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) John Masunga (kushoto) pamoja na Mwanasheria wa GEPF Anna Shayo (kulia) wakisaini nyaraka muhimu za makubaliano ya uwezekaji kati ya Magereza na GEPF).
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria hafla ya utiliwaji sahini wa Mkataba wa Uwekezaji kati ya Jeshi la Magereza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa GEPF. Waliokaa ni Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw.Daud Msangi (kulia). Kutoka kushoto ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Kizito Jaka, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) John Masunga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Gideon Nkana, Festo Fute (GEPF), Anna Shayo (GEPF) na Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Issack Kangura. 

Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja wa Magereza


Na Deodatus Kazinja-PHQ

Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la uzalishaji mali (Prisons Corporation Sole) limetiliana Mkataba wa uwekezaji na Mfuko wa Jamii wa GEPF ambapo majengo ya vitega uchumi yatajengwa katika maeneo ya Kihonda Mkoani Morogoro na Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro. Tukio hilo la utiwaji sahini mkataba huo limefanyika leo Alhamis 29, 2014 katika ukumbi wa mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la 

Magereza Jijini Dar es salaam. Akiongea katika hafla hiyo Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja amesama ni kiu yake kuona mradi huo unaanza kutekelezwa ifikapo Julai Mosi, 2014. Naye Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw. Daud Msangi amesema ukiwepo ushirikiano wa kutosha miradi hii itaweza kukamilika mapema iwezekanavyo kwa faidi ya pande zote mbili.