Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, June 20, 2014

Maadhimisho ya siku ya Magereza (Magereza Day) yafana jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(MB) akipokea Salaam ya heshima toka kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Magereza(Magereza Day). Kushoto katika picha ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja (kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (MB) akikagua Gadi ya Wanawake inayoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika leo Juni 20, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Gadi ya Wanaume iliyoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika mwendo wa haraka wakati wa kutoa heshima katika Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(aliyesimama) akitoa maelezo mafupi kuhusu Madhumuni ya Maadhimisho ya Siku ya Magereza(Magereza Day). Maadhimisho haya ya siku ya Magereza yanafanyika hapa nchini kwa mara ya pili ambapo leo yamefanyika katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam(wa Nne kulia katika vazi la suti nyeusi) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza Nchini wakitoa heshima ya Utii wakati Kikosi cha Bendera kikipita mbele ya Mgeni rasmi(hayupo pichani) katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza(Magereza Day) yaliyofanyika leo Juni 20, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Kilimo na Mifugo Ndani ya Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasan Kimaro(wa pili kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (suti nyeusi) kuhusu uzalishaji wa mafuta ya mawese ambayo hutumika kwa matumizi ya Wafungwa Magerezani alipotembelea Banda la Kilimo na Mifugo (wa pili kulia kwa Waziri) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Msanii Nguza Viking anayetumikia Kifungo chake Gerezani akiwa na Bendi ya Wafungwa(anayepiga gitaa) akiimba Wimbo Maalum kuhusu Urekebishaji wa Wafungwa unavyofanyika Magerezani(wa pili kulia) ni Jonson Nguza Maarufu kwa jina la Papii Kocha wakitumbuiza katika Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika leo Juni 20, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.

Monday, June 2, 2014

Jeshi la Magereza kuingia ushirikiano rasmi na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

 Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara alipowasilishwa katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (kulia)
 Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (wa tatu)  wakisani hati za makubariano ya ushirikiano kati ya Taasisi hizo mbili.  Wakwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa na wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango anayeshughulikia Teknolojia na Huduma za Kujifunzia Chuoni hapo.
 Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa(wa kwanza kulia) na Prof. Modest Valisango (wa kwanza kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
 Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja ( kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete ( kushoto)wakibadilishana nyaraka muhimu za makubaliano ya ushirikiano mara baada ya kutiwa sahini.
 Aliyewahi kuwa mfungwa kwa takribani mika 20 gerezani Ukonga Ng. Haruna Pembe (mwenye suti) akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoweza kusoma na kumaliza shahada yake ya sharia akiwa gerezani.
 Baadhi wa washiriki wa hafla ya utiwaji sahini makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu cha Huria cha Tanzania wakifuatilia kwa karibu simulizi za  aliyewahi kuwa mfungwa Bw. Haruna Pembe (hayupo pichani) alivyosoma na kumaliza shahada yake ya sharia na hivi sasa anasoma shahada ya uzamili chuoni hapo.
 Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya undani wa ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma  Malewa, wa nne  kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango aliyepia Mkuu wa Teknolojia na Huduma za Mafunzo chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya undani wa ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma  Malewa, wa nne  kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango aliyepia Mkuu wa Teknolojia na Huduma za Mafunzo chuoni hapo.


Na Insp Deodatus Kazinja, PHQ

Jeshi la Magereza nchini limeingia katika Makubaliano rasmi na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumatatu 02 Juni, 2014 katika  Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Chuo hicho kilichoko eneo la Biafra Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wajumbe mbalimbali kutoka Chuoni hapo, Jeshi la Magereza pamoja na wanahabari Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tolly Mbwete amesema kuwa ushirikiano kati ya Magereza na OUT umekuwepo kwa muda mrefu ila hivi sasa ni kuuimarisha zaidi kwa kufanya mapitio kwenye maeneo ya ushirikiano kwa lengo kujumuisha maeneo mengi zaidi.

Ametaja maeneo yanayokusuduiwa katika makubaliano hayo kuwa ni Mafunzo na shughuli za utafiti, uandaaji wa mitaala na vifaa vya mafunzo hususani ni katika suala la urekiebishaji wa wahalifu, utoaji wa elimu kwa umma kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hizi mbili, ubadilishanaji wa nyaraka, vitabu vya rejea na vifaa muhimu vya maktaba, maendelea ya kitaaluma kwa watumishi wa Jeshi la Magereza na wafungwa nakadhalika.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja amesema kwa muda wote Jeshi la Magereza limekuwa tayari kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kutoa vibali mbalimbali kwa wanafunzi na wakufunzi wanaotaka kufanya tafiti katika maeneo ya Magereza, kutoa vibali kwa watumishi wa Jeshi la Magereza kusoma katika chuo hicho na kutoa ushirikiano wa dhati kwa wafungwa wanaotaka kusoma kwa kutumia chuo hicho wakiwa gerezani.

Makubaliano haya ya leo yatakuwa ya msaada sana kwa Jeshi la Magereza katika kulifanya liwe la kisasa na kulipunguzia matumizi” Alisema Kamishna Minja.

Katika hafla ushuhuda wa wafungwa kusoma na kufanikiwa wakiwa gerezani ulitolewa na ex-mfungwa Haruna Pembe aliyepata shahada ya sheria (LLB) akiwa gerezani na sasa yuko nje baada ya kushinda rufaa yake akiwa sasa anafanya shahada ya pili ya sheria katika Chuo Kikuu hicho.

(Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja, PHQ)