Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, October 28, 2016

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA ATEMBELEA MRADI WA UZALISHAJI KOKOTO WA SUMA - JKT, PONGWE MSUNGULA MKOANI PWANI

Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja akisalimiana na baadhi ya Maafisa Watendaji katika mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula, Mkoa wa Pwani leo Oktoba 28, 2016 alipotembelea mradi huo ili kujionea shughuli za uzalishaji wa kokoto.
Meneja Msaidizi wa Mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula, Kepteni Gaspa Rugayana akitoa maelezo mafupi kuhusiana na mradi huo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia).
Ujumbe wa Maafisa Watendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) ambao umefuatana na Kamishna Jenerali wa Magereza katika ziara ya mafunzo kwenye mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula, Mkoa wa Pwani.  Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza linatarajia kuanzisha mradi wa Uzalishaji kokoto katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.
Maafisa Watendaji wa SUMA – JKT katika mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula wakimtembeza katika maeneo mbalimbali Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(wa tatu kulia) alipofanya ziara ya mafunzo katika mradi huo(kulia) ni Meneja Fedha na Utawala katika Mradi huo, Bi. Glory Kimaro.
Meneja Uzalishaji wa mradi wa kokoto, Kepteni Paul Mbeya akimuonesha mtambo wa uzalishaji kokoto Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia).
Mtambo wa Uzalishaji katika mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Msungula kama unavyoonekana katika picha. Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza linatarajia kuanzisha mradi wa Uzalishaji kokoto katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.
Meneja Mkuu wa Mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT, Bw. Semih Yaran akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(wa pili kulia) maeneo mbalimbali ya mradi huo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) akiangalia kokoto za kutengenezea barabara zinazozalishwa katika mradi huo. Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza linatarajia kuanzisha mradi wa Uzalishaji kokoto katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.
Muonekano wa kokoto zinazozalishwa katika Mradi wa Uzalishaji kokoto wa SUMA – JKT uliopo Pongwe Musungula

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Friday, October 21, 2016

MAHAFALI YA 13 YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI BWAWANI YAFANA MKOANI PWANI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akisalimiana na mmoja wa wazazi alipowasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Bwawani kushiriki Mahafali ya 13 ya Shule hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Kidato cha nne katika Mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya hotuba ya Mgeni rasmi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akitoa neno kwa wahitimu katika Mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
 Wahitimu wa Kidato cha Nne wakitoa burudani ya Wimbo Maalum wa Shule hiyo.
 Meza Kuu  wakiimba wimbo wa Shule ya Sekondari Bwawani kama wanavyoonekana katika picha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akizindua rasmi Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Bwawani wakati wa Mahafali ya 13 ya Kidato cha nne.
Muonekano wa Bweni la Wanawake lililokamilishwa kujengwa tayari kwa matumizi katika Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani
Muonekano wa ndani wa Bweni la Wanawake lililokamilishwa kujengwa tayari kwa matumizi katika Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Kidato cha Nne(waliosimama) katika Mahafali ya Shule ya Sekondari Bwawani(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja

(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Thursday, October 20, 2016

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MGENI RASMI MAHAFALI YA 13 YA KIDATO CHA NNE, BWAWANI SEKONDARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tarehe 21 Oktoba, 2016 saa 3:00 asubuhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za mahafali ya 13 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Bwawani iliyopo Mkoa wa Pwani.

Shule ya Sekondari Bwawani inamilikiwa na Jeshi la Magereza, ilianzishwa mwaka 1978 kwa lengo la kutoa elimu ya Sekondari kwa Watumishi wa Magereza ambapo hivi sasa Shule hiyo inatoa elimu ya Sekondari kwa vijana wa kike na kiume kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.

Shule hiyo pia inatoa elimu ya Kidato cha Tano na Sita, katika muunganiko wa masomo ya Historia, Jiografia na Kiswahili (HGK), Historia, Jiographia na Kiingereza(HGL). Aidha, mwaka huu inatarajia kuanzisha mkondo wa masomo ya sayansi(CBG) yaani masomo ya Kemia, Baiologia na Jiografia.

Jumla ya Wanafunzi 94 wa shule hiyo wanatarajia kuhitimu elimu yao ya kidato cha nne  mwezi Novemba mwaka huu.

Sherehe hizo zitajumuisha mambo yafuatayo:-

  • Mgeni rasmi kutembelea maeneo ya shule na kuweka mawe ya ufunguzi katika majengo ya shule;
  • Mgeni rasmi kuangalia Maonesho ya Taaluma kwa Wanafunzi Washiriki;

  • Mgeni rasmi kutoa vyeti na zawadi mbalimbali kwa Wanafunzi wahitimu na;

  • Mgeni rasmi kutoa hotuba

Sherehe za mahafali hayo zinatarajia kukamilika saa 8:00 mchana. Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye sherehe hizo tarehe 21 Oktoba, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Imetolewa na: Lucas Mboje,
Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM

20 Oktoba, 2016.

Friday, October 14, 2016

TAMASHA LA MICHEZO GEREZA KUU UKONGA DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Global Publshers akisalimia wafungwa (hawapo pichani) mara alipowasili gerezani Ukonga katika Tamasha la Kuadhimisha Siku ya Nyerere.(Nyerere Day) leo tarehe 14, 10, 2016 jijini Dar es salaam.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitia saini kitabu kitabu cha wageni gerezani Ukonga katika Tamasha la Michezo wakati wa kuadhimisha Nyerere Day.Kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Stephen Mwaisabila, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Thom Nyanduga, Mkurugenzi wa Global Publishers Erick Shigongo na Abdalah Mrisho ambaye ni meneja wa Global Publshers.
Baadhi ya Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia kwa magunia wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016
Mmoja wa Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia na yai katika kijiti wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016
Sehemu ya Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia mita 100 wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016
Baadhi ya Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wlio kushoto
Baadhi ya Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kushikana mieleka wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016
Mkurugenzi wa Global Publishers Bw.Erick Shigongo (mgeni rasmi) akisalimiana na wachezaji kabla ya mchuano mkali nawakuvutia wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wenye sare Nyekundu kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoshana nguvu ya 2-2 katika muda wa kawaida
Mkurugenzi wa Global Publishers Bw.Erick Shigongo (mgeni rasmi) akisalimiana na wachezaji kabla ya mchuano mkali nawakuvutia wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wenye sare Nyekundu kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoshana nguvu ya 2-2 katika muda wa kawaida

Sehemu ya zawadi zilizoletwa na wageni gerezani wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani humo  tarehe 14.10.2016
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Magereza na wageni mbalimbali wakishiriki chakula cha mchana pamoja na wafungwa (hawapo pichani) gerezani Ukonga wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani humo  tarehe 14.10.2016
Baadhi ya wachezaji wa timu iliyoibuka mshindi wakishangilia baada ya kupachika bao la kusawazisha katika dakika mbili za mwisho na kufanya mchezo kuwa 2-2 na kisha kuingia katika mikwaju ya penati zilizowa ushindi wachezaji wenye uzi mwekundu wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere nchini lililofanyika ndani ya gereza la Ukonga jijini Dar es salaam tarehe 14.10.2016
Kepteni wa Timu iliyoshinda Johnson Nguza (Papii Kocha) akibeba kombe kwa niaba ya timu yake baada ya kulipokea toka kwa Mgeni Rasmi Erick Shigongo wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dar es salaam,  tarehe 14.10.2016
Johnson Nguza aka Papii Kocha akitumbuiza kwa pamoja na wanamuziki wa Twanga Pepeta wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dar es salaam, tarehe 14.10.2016
Picha ya pamoja ya Timu iliyoibuka washindi wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulipatikana kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoshana  nguvu ya 2-2 katika muda wa kawaida.

Picha zote na Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza


Na ASP Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza
Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers limefanya Tamasha la michezo mbalimbali kwa wafungwa wa gereza hilo.

Akiongea katika Tamasha hilo Mkurugenzi wa Global Publishers aliyekuwa pia mgeni rasmi Bwana Erick Shigongo amewaambia wafungwa kuwa dhimra ya ujio wao gereza ni katika kuonesha kuwathamini, kuwahurumia na kuwatia moyo kwamba kuwa kwao gerezani siyo kwamba wametengwa na dunia.

Bwana Shigongo aliwatia moyo wafungwa hao kuwa hawatakiwi kukata tamaa na bado wanayo nafasi ya kubadilika na kuwa raia wema. “Kila mwanadamu anaowajibu wa kubadili maisha yake, Mwalimu Nyerere tunayemuadhimisha leo alizaliwa kama mimi na wewe na kutengeneza maisha yake na leo tunamkubuka kwanini wewe ushindwe?”

Aliongeza “ najua wengi wenu mko hapa mkiwa mmeitwa majina mengi kwakuwa mmehukumiwa, hizini hukumu za wanadamu, mnaouwezo wa kuandika kurasa mpya katika maisha yenu na siku mkitoka duniani waseme mtu mwema ameondoka. Siku moja inatosha kubadili maisha yako, kila siku andika ukurasa mpya wa maisha yako na Mungu atakuongoza alisisitiza Shigongo.

Wadau wengine walioungana na Global Publishers katika tukio hilo ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu Nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Thom Nyanduga na ndugu Rajab Maranda (aliyewahi kuwa mfungwa gereza Ukonga) ambao kwa pamoja walileta zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao ikiwemo vifaa vya, sabuni,soda kikombe ambacho kilitolewa kwa timu iliyofanya vizuri katika mpira wa miguu.

Katika Tamasha hilo wafungwa walishiriki michezo ya kukimbia katika magunia, kukimbia na yai katika kijiti, mbio za mita 100 vijana kwa wazee, mita 400 kupokezana vijiti, kuvuta kamba, mieleka, mpira wa miguu, mashairi, kuonesha vipaji vya uchekeshaji, kuimba kwa mtindo kufokafoka, ngoma za jadi  na burudani kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Twanga pepeta.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA ATEMBELEA ENEO LITAKALOJENGWA KIWANDA KIPYA CHA KUTENGENEZA VIATU, MJINI MOSHI

Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(vazi la kiraia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Gereza  Karanga, Moshi, ACP. Hassan Mkwiche (kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Karanga, ASP. Michael Minja(kulia) alipotembelea Kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa ajili ya  ujenzi wa Kiwanda kipya cha kisasa cha viatu leo Oktoba 14, 2016. Wengine pichani ni Maafisa wa Jeshi la  Magereza Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akiangalia eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda kipya cha viatu .
Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Magereza Mkoa Kilimanjaro, ACP. Anderson Kamtearo(kulia) alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho kipya cha kutengeneza viatu.
Eneo litakalojengwa kiwanda kipya cha kisasa cha kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngozi. Kiwanda hicho kitakuwa cha ubia baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa jamii wa PPF.
Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja akiangalia kiatu aina ya buti ndefu zinazotengenezwa kiwandani hapo kwa ajili ya Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama inavyoonekana katika picha

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Thursday, October 13, 2016

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN MINJA AWASILI MKOANI KILIMANJARO - KUKAGUA ENEO LITAKALOJENGWA KIWANDA KIPYA CHA VIATU

Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kushoto) akipokea salaamu ya heshima kutoka kwa Afisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro alipowasili Mkoani humo katika ziara ya kikazi ambapo atafanya ukaguzi wa eneo la mradi wa Uwekezaji  wa Kiwanda kipya cha Viatu Gereza Karanga, Moshi ambapo mradi huo ni wa ubia baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa Jamii wa PPF, leo Oktoba 13, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, ACP. Anderson Kamtearo mara baada ya kuwasili Mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Gereza Kwamugumi, SP. Christopher Mwenda(kushoto) pamoja na  Mkuu wa Gereza Korogwe, ACP. Lenard Mushi wakimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) aliposimama kwa muda kukagua Gereza la Wilaya Korogwe wakati akielekea katika ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro, leo Oktoba 13, 2016. 

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Tuesday, October 4, 2016

SHIRIKA LA MAGEREZA NA MFUKO WA PPF WAINGIA UBIA WA UJENZI WA KIWANDA KIPYA CHA VIATU HAPA NCHINI

Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) akizungumza katika hafla fupi ya utiwaji saini wa Mkataba wa wa Uwekezaji  wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza Karanga, Moshi baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa Jamii wa PPF(kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio, Oktober 4, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio(kushoto) na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) kwa pamoja wakisaini Mkataba wa Uwekezaji baina ya Taasisi hizo mbili katika Ukumbi wa Mkao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar salaam, Oktoba 4, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio  wakibadilishana nyaraka mbalimbali za Makubaliano katika Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya utiwaji saini wa Mkataba wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha Viatu.
Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Mfuko wa Jamii wa PPF wakifuatilia utiwaji saini wa Mkataba wa Uwekezaji.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiwaji wa Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza,
Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la uzalishaji mali (Prisons Corporation Sole) limeingia Makubaliano na Mfuko wa Jamii wa PPF katika ujenzi na uboreshaji wa mradi wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
 
Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumanne 04 Oktoba, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es salaam.
 
Akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wanahabari, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Minja amesema uhirikiano huo unalenga kuliimarisha Shirika la Magereza ili liweze kujiendesha kibiashara pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara.
 
Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa uwekezaji katika kiwanda hicho utalisaidia Jeshi la Magereza kufikia kiu ya kuzalisha bidhaa za ngozi zenye ubora wa hali ya juu na zinazochochea ushindani katika soko la ndani na nje.
 
“Naamini uwekezaji huu wa Kiwanda kipya cha Viatu cha Karanga Moshi ni ishara tosha ya kuunga mkono dhamira ya dhati ya Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Tanzania mpya ya Viwanda inawezekana hivyo kutimiza malengo na Dira ya Taifa ya Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025”. Alisema Kamanda Minja.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Jamii wa PPF, Bw. William Erio amesema kuwa PPF ipo tayari kwa dhati kushirikiana na Shirika la Magereza katika mradi huo wa ujenzi wa Kiwanda cha Viatu kwani yapo mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo ya ngozi hapa nchini.

“Makubaliano haya yanahusisha ujenzi wa Kiwanda kipya cha viatu pamoja na uwekezaji wa mashine za kisasa za kutengenezea bidhaa za ngozi katika Kiwanda cha Viatu cha Karanga Moshi kinachomilikiwa na Jeshi la Magereza”. Alisema Bw. Erio
 
Pia, aliongeza kuwa uwekezaji huo utawezesha Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama hapa nchini kununua sare za viatu na vifaa vingine vya bidhaa za ngozi zitakazozalishwa katika Kiwanda hicho badala ya kuagiza nje ya nchi.
 
Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.