Friday, May 29, 2015
Sherehe za kufunga mafunzo ya awali ya jeshi la magereza kozi na. 27 chuo cha magereza Kiwira zafana, jijini Mbeya
9:58 PM
Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza wakipita kwa mwendo wa
haraka mbele ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani) leo Mei 29, 2015 katika Chuo
cha Magereza, Kiwira Kilichopo Mkoani Mbeya.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa
maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi aweze kutoka hotuba ya kufunga rasmi Mafunzo ya
Uaskari Magereza katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil
akipokea Salaam ya heshima akiwa jukwaan kabla ya kukagua Gwaride Maalum
katika sherehe za kufunga Mafunzo ya Uaskari Magereza, Kiwira
Mbeya(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir
Minja(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Stanford Ntirundura.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil
akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali
ya Uaskari Magereza leo Mei 29, 2015 Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.
Katibu Mkuu akikabidhi zawadi kwa Mhitimu wa Kozi Na. 27 ya Uaskari
Magereza ambaye amefanya vizuri katika Somo la Gwaride na Ukakamavu
Askari Mhitimu, Ezra Kapesa leo katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo
Mkoani Mbeya(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia)
akimuongoza Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mbarak Abdulwakil(katikati) kuelekea kwenye Ukumbi wa Mihadhara kwa
ajili ya kufunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza leo Mei 29,
2015(kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Stanford Ntirundura.
Gadi ya Askari wa Kike ambao ni Wahitimu wa Kozi ya Awali ya Uaskari
Magereza wakila Kiapo cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
na Usalama ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(hayupo
pichani) katika sherehe za ufungaji Mafunzo hayo.
(Picha
zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Wednesday, May 27, 2015
Kikao cha maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini chaanza leo mkoani Morogoro
4:57 PM
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa
hotuba ya ufunguzi leo Mei 26, 2015 kwenye Kikao cha Maafisa Waandamizi
wa Jeshi la Magereza nchini kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya
Edema, Mkoani Morogoro.
Wajumbe wa Kikao ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
nchiniwa kifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(wa kwanza kushoto)
ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza
Joel Bukuku.
Mshauri Mwelekezi katika Maboresho ndani ya Jeshi la Magereza Nchini,
Dkt. Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha Mada
ya Maboresho ndani ya Jeshi la Magereza kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi
la Magereza nchini.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir
Minja(kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mbarak Abdulwakil kwenye kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza nchini kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani
Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(shati
jeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza nchini waliosimama nyuma(wa sita kushoto) ni Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(wa tano kushoto) ni
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(wa tatu kulia) ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul.
(Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza).
Monday, May 25, 2015
Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi afungua kikao cha bajeti ya shirika la Magereza kwa mwaka 2015/2016 leo mkoani Morogoro
2:36 PM
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(suti
nyeusi) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John
Casmir Minja mara baada ya kuwasili leo Mei 25, 2015 katika Ukumbi wa
Mikutano wa Edema, Mkoani Morogoro kwa ajili ya ufunguzi wa Kikao cha
Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016(wa pili kulia) ni
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo
mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani) kutoa hotuba ya
ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016.
Wajumbe wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016
wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi leo Mei 25, 2015 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Edema, Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimkabidhi
Begi lenye makabrasha ya Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza, Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(wa kwanza
kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak
Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikao
cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016 waliosimama(wa
tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir
Minja(wa tatu kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice
Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston
Sanga
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).