Wednesday, May 27, 2015

Kikao cha maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini chaanza leo mkoani Morogoro

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa hotuba ya ufunguzi leo Mei 26, 2015 kwenye Kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Wajumbe wa Kikao ambao ni  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchiniwa kifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joel Bukuku.
Mshauri Mwelekezi katika Maboresho ndani ya Jeshi la Magereza Nchini, Dkt. Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha Mada ya Maboresho ndani ya Jeshi la Magereza kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil kwenye kikao  cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(shati jeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini waliosimama nyuma(wa sita kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(wa tano kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(wa tatu kulia) ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).