Friday, October 25, 2019
SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA PILI KATIKA JESHI LA MAGEREZA ZAFANA MKOANI MOROGORO
5:31 PM
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akikagua Paredi Maalum lililoandaliwa
na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza lililofanyika
Oktoba 25, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani
Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akiwa katika jukwaa
akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa
Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).
Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi
Wasaidizi wa Magereza wakipita mbele ya
Mgeni rasmi katika Sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya
Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP Phaustine Kasike(kushoto) akimvisha cheo cha
Mkaguzi Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi
Wasaidizi wa Magereza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika
kwa muda wa miezi minne.
Baadhi
ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa
Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza wakiwa tayari wamevishwa vyeo
vipya kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP Phaustine Kasike akitoa hotuba fupi kwa
Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya
mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
Mhitimu wa Mafunzo ya Maafisa
Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa
Magereza waliosimama mstari wa nyuma(Picha
zote na Jeshi la Magereza).
Thursday, October 17, 2019
“Zingatieni Maadili ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yenu” – CGP Kasike
12:33 AM
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza
na Maafisa na askari wa Gereza Namajani lililopo Wilayani Masasi, Oktoba 16,
2019 alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara.
Baadhi
ya askari wa Gereza Namajani wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini,
Phaustine Kasike
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
akizungumza na Maafisa na askari wa Gereza Masasi, Oktoba 16, 2019
alipotembelea katika ziara yake ya
kikazi.
Mkuu wa Gereza Masasi, Mrakibu wa Magereza, Juma Mkumba
akitoa taarifa fupi ya Gereza mbele ya
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) alipotembelea Gereza hilo.
Kamishna Jenerali Phaustine Kasike akikagua Mifugo Katika Gereza la Wilaya Masasi.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na askari wa Gereza Namajani alipotembelea leo Oktoba 16, 2019 katika
ziara yake ya kikazi. Kulia ni Mkuu wa
Magereza Mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Varisanga Msuya(Picha zote
na Jeshi la Magereza).
Wednesday, October 16, 2019
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA LA WILAYA RUANGWA, LINDI TAREHE 15 OKTOBA 2019
11:15 AM
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike, akisalimiana na Msaidizi wa Mkuu wa Gereza
Ruangwa, Mkaguzi wa Magereza, Alex Munga’nzo alipowasili Oktoba 15, 2019 kwa
ziara ya kikazi Gerezani hapo.
Mkuu
wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Josephine
Semwenda(kushoto) akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Magereza Mkoani Lindi mbele ya Kamishna
Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(meza kuu) alipowasili Gereza Ruangwa Oktoba 15, 2019.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua korosho ambayo tayari
imeanza kuvunwa katika mashamba mbalimbali ya Gereza Ruangwa, lililopo Mkoani
Lindi.
Ujenzi
wa jengo litakalotumika kwa ajili ya mapokezi ya ndugu na jamaa wa wafungwa na
mahabusu wanaofika Gereza Ruangwa kuwatembelea ndugu zao ukiendelea katika
hatua mbalimbali za ujenzi.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Idara ya
Uhamiaji nchini, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala walipokutana
leo Wilayani Ruangwa ziarani (Picha zote
na Jeshi la Magereza).
Wednesday, October 9, 2019
“Simamieni wafungwa kutatua uhaba wa makazi ya askari” – CGP Kasike
11:06 AM
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia)
akikagua matofali ya kuchoma katika mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma katika
gereza la wilaya ya Mbozi alipotembelea hivi karibuni katika ziara yake ya kikazi Mkoani Songwe.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
akikagua moja ya tanulu la matofali ya kuchoma katika mradi wa ufyatuaji tofali
za kuchoma katika Kambi ya Mkwajuni ,
Wilayani Songwe, leo Oktoba 8, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Mkoani Songwe.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
akiwasili jana Oktoba 7, 2019 katika ziara yake ya kikazi Gereza Ngwala.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa(katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike(wa pili toka kulia) alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo leo
Oktoba 8, 2019. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Songwe, Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Lyazeck Mwaseba. (Picha na Jeshi la Magereza)
Na Mwandishi wetu, Songwe;
KAMISHNA
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amewataka Wakuu wa magereza Tanzania
Bara kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo agizo la Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa jeshi hilo kote nchini kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa
waliopo magerezani.
Akizungumza Mkoani Songwe mara baada
ya kukagua miradi ya ufyatuaji wa matofali ya kuchoma na ujenzi wa nyumba za
maafisa na askari katika magereza ya Ileje, Mbozi, Ngwala na Kambi ya Mkwajuni
iliyopo Mkoani Songwe, Kamishna Jenerali
Kasike amesema ujenzi wa makazi za askari unaoendelea katika vituo mbalimbali nchini
ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli katika kutatua changamoto ya
makazi kwa watumishi wa Jeshi hilo.
"Mkakati wa utatuaji wa changamoto ya uhaba wa nyumba za
Maafisa na askari lazima utiliwe mkazo na kupewa kipaumbele katika kuwatumia
wafungwa waliopo magerezani katika suala
la ujenzi sambambamba na uzalishaji wa chakula chakutosha ili kuipunguzia
Serikali gharama za kuwahudumia wahalifu wote walipo magerezani, "
alisema Kamishna Jenerali Kasike.
Katika hatua nyingine, Kamishna
Jenerali Kasike ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Songwe kwa kuanzisha ujenzi wa
Gereza jipya katika mji wa Mkwajuni ambao ni Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe.
Kamishna Jenerali Kasike amesema
uwepo wa gereza hilo katika wilaya ya Songwe utasaidia katika kumaliza tatizo
la msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye gereza la wilaya ya Mbozi.
“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki hivyo nimpongeze sana Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa Gereza hili kimsingi utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza Mbozi,” amesema Jenerali Kasike.
“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki hivyo nimpongeze sana Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa Gereza hili kimsingi utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza Mbozi,” amesema Jenerali Kasike.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Songwe.
Mhe. Samwel Opulukwa ameshukru ujio wa Kamishna Jenerali katika ziara yake ya
kikazi katika Gereza la Ngwala pamoja na Kambi ya Mkwajuni ili kujionea hali
halisi ya Uendeshaji wa Jeshi hilo, Wilayani Songwe.
“Kamishna Jenerali
nikuhakikishie tu kuwa Uongozi wa wilaya utashirikiana na Jeshi la Magereza
katika kuhakikisha kuwa tunakamilisha ujenzi wa gereza hili jipya la Mkwajuni
ili kusaidia kuondoa usumbufu wa wahalifu kwenda gereza la wilaya ya mbozi,”
Alisistiza Mhe. Opulukwa.
Kwa sasa, wakazi wa wilaya hiyo ya Songwe ambao wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali au waliohukumiwa vifungo hupelekwa katika Gereza la wilaya ya Mbozi kitendo ambacho kinawanyima wafungwa na mahabusu fursa ya kuonana na ndugu au mawakili wao kutokana na umbali uliopo ambapo kutokana na juhudi za Mkuu wa Wilaya hiyo tayari Bweni moja la Wafungwa lenye uwezo wa kuhifadhi waha;lifu 150 limekamilika pamoja na Ofisi ya Utawala na ujenzi wa Ukuta wa gereza unaendelea katika Kambi hiyo ya Mkwajuni.