Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Wednesday, November 30, 2016

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NA MKURUGENZI TBA WAKAGUA MAENEO YATAKAYOJENGWA NYUMBA ZA ASKARI WA JESHI LA MAGEREZA JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo, Bw. Elius Mwakalinga wakiangalia moja ya eneo la Gereza Segerea ambalo litajengwa nyumba za kuishi za Maafisa na askari wa Jeshi hilo(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Kuu Segerea, ACP.  Godfrey Kavishe akiwaonesha eneo hilo walipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ya Jeshi ambapo tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Moja ya eneo litakalojengwa nyumba za Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza lililopo katika eneo la Gereza Kuu Segerea, Jijini Dar es Salaam kama linavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo, Bw. Elius Mwakalinga akisalimiana na Baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dar es Salaam alipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali yatakayojengwa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo leo Novemba 30, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(wa pili kulia) akiwa ameongozana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu pamoja na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo waliopo katika Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbalimbali yatakayojengwa nyumba za watumishi wa Jeshi hilo. 
 
Moja ya nyumba ya mabati iliyopo katika Gereza la Mahabusu Keko kama inavyoonekana katika picha. Katika kukabiliana na uhaba wa nyumba za askari wa Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Friday, November 25, 2016

SHIRIKA LA MAGEREZA NA MFUKO WA JAMII WA GEPF WAJADILI UJENZI WA KIWANDA CHA NGUO HAPA NCHINI, JIJINI DAR

Maafisa Watendaji wa Shirika la Magereza wakifuatilia majadiliano ya uanzishwaji wa Kiwanda cha nguo aina mbalimbali ikiwemo sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika Novemba 25, 2016 katika Ukumbi wa GEPF Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Watendaji Wakuu wa Mfuko wa Jamii wa GEPF wakijadiliana katika kikao hicho cha kazi(katikati) ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Festo Fule.
 Kikao kikiendelea katika Ukumbi wa GEPF Jijini Dar es Salaam kama wanavyoonekana katika picha.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiondoka katika viunga vya Ofisi za Mfuko wa Jamii wa GEPF mara baada ya kikao kazi

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Wednesday, November 2, 2016

SHIRIKA LA MAGEREZA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA KICHINA KWENYE KILIMO CHA KISASA

Kamishna Jenerali wa Mgereza – CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji wa masuala ya Kilimo cha kisasa mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake leo Novemba 2, 2016, Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei(kushoto) ni  Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi.

Na; Lucas Mboje, Jeshi la Magereza – Dar es Salaam

KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja amekutana na Wawekezaji wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China pamoja na Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION na kumuahidi kushirikiana na Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ya Kilimo cha kisasa, Madini na Viwanda vinavyoendeshwa na Shirika hilo.

Akizungumza na Wawekezaji hao leo asbuhi Ofisini kwake (Jumatano, Novemba 2, 2016)  alisema kwamba Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji mali lina fursa nyingi za miradi  ya uwekezaji kwenye sekta nyingi kama vile Kilimo, Viwanda na Madini ambapo aliwahahakishia ushirikiano wa kutosha kwenye uwekezaji wao.

Wawekezaji hao tayari wamefanya mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo wanatarajia kuiingia Makubaliano (MoU) na Jeshi la Magereza kwa ajili ya miradi mbalimbali  ikiwemo ya Kilimo cha kisasa katika Gereza Idete lililopo Mkoani Morogoro pamoja na Mradi wa Ngo’mbe wa nyama Gereza Ubena, Mkoani Pwani.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei alisema amefurahishwa na ziara waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza hapa Tanzania.

Naye, Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi ambayo inashughulikia na masuala ya Kilimo cha mazao ya chakula na nyama alisema watawekeza kwenye kilimo hususan cha umwagiliaji na watajenga Kiwanda kwa ajili ya usindikaji.

Shirika la Uzalishaji mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) lina jumla ya Miradi 23, kati ya hiyo miradi 15 ni ya kilimo na mifugo na 8 ni ya viwanda vidogo vidogo, pia zipo shughuli za mradi wa Kikosi cha Ujenzi zinazosimamiwa na Shirika hilo.

Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ikiwemo uwekezaji wa ubia kwenye miradi yake ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.
 
Mwisho.