Monday, December 23, 2019
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE AHIMIZA WAFUASI WAKE KUZINGATIA NIDHAMU JESHINI
9:05 AM
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike akizungumza katika kikao na
Maafisa na askari wa vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es Salaam ambapo kikao
hicho kilijadili masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya utendaji kazi, maadili
ya kazi, nidhamu na mikakati mbalimbali ya Jeshi ikiwemo ya Kilimo, viwanda na
ufugaji. Kikao kazi hicho kimefanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga
jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka vituo vya Magereza Mkoa wa
Dar es Salaam wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike(hayupo pichani) kikao hicho kilijadili masuala mbalimbali ikiwemo
masuala ya utendaji kazi, maadili ya kazi, nidhamu na mikakati mbalimbali ya
Jeshi ikiwemo ya Kilimo, viwanda na ufugaji.
Askari
wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Magereza kutoka katika vituo vya Magereza Mkoa
wa Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya kikao kazi na Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini Phaustine Kasike Desemba 20, 2019 (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Saturday, December 14, 2019
UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA KUWAACHILIA HURU WAFUNGWA WANUFAIKA WA MSAMAHA WA RAIS WAKAMILIKA NCHI NZIMA
11:01 AM
Na ASP. Lucas Mboje, Dar es Salaam
JUMLA ya Wafungwa
5,533 katika magereza mbalimbali nchini walionufaika na msamaha wa Rais wakati
wa maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru
wameachiliwa huru magerezani.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
Phaustine Kasike amesema kuwa utekelezaji wa zoezi la kuwaachiliwa huru
wafungwa wote walionufaika na msamaha wa Rais umekamilika nchi nzima.
“Ni
matarajio yangu kuwa wafungwa walioachiliwa wamejutia makosa yao na wataacha
kutenda uhalifu hivyo kujihusisha na shughuli halali kwa maendeleo yao, familia
zao, jamii na taifa kwa ujumla”, amesisitiza Jenerali Kasike.
Aidha,
Kamishna Jenerali Kasike ameelezea manufaa mbalimbali ya msamaha huo; mosi
kupungua kwa msongamano magerezani, pili, wanufaika wa msamaha kujumuika na
familia zao, tatu, kichocheo cha urekebishaji magerezani kwani msamaha huo
utasaidia kuimarika kwa nidhamu na kurejesha matumaini kwa wanaobakia
magerezani pamoja na wanufaika wa wamsamaha huo kupata fursa ya kujishughulisha
na shughuli za maendeleo uraiani.
“Zipo
changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa zoezi hili ambapo baadhi ya wafungwa
walionesha kuwa hawako tayari kuungana na jamii zao pamoja na waliosamehewa
kurejea kutenda makosa mara baada ya kuachiwa huru. Hata hivyo nitoe wito kwa
jamii nchini kuwapokea wafungwa hao na kuacha kuwanyanyapaa”, amesema Jenerali
Kasike.
Wakati
huo huo, Kamishna Jenerali Kasike amemshukru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kutoa msamaha huo ambao ni wa kihistoria hapa nchini. Pia
amewapongeza wanahabari wote nchini kwa namna walivyoshiriki kutoa habari za
zoezi la msamaha huo katika ngazi ya Mkoa na wilaya.
Kwa
mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 45(1) (d) imempa
mamlaka Rais kutoa msamaha kwa wafungwa waliopo magerezani. Kwa kutumia Ibara
hiyo Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa wakati wa
maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru ambapo kilele chake kilifanyika Mkoani Mwanza
Desemba 9, 2019.
Wednesday, December 11, 2019
WAFUNGWA 79 WA GEREZA KUU BUTIMBA WALIONUFAIKA NA MSAMAHA WA RAIS WAACHILIWA JIJINI MWANZA TAREHE 10 DISEMBA 2019
9:38 AM
Mfungwa mnufaika wa Msamaha wa Rais, William
Dingu akizungumza na Wanahabari(hawapo pichani) baada ya kuachiliwa huru leo.
Mfungwa huyo amemshukru Rais kwa msamha huo, aidha, amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kumwezesha
ujuzi wa wa fani ya ujenzi ambao ameupatia gerezani kupitia programu ya
Urekebishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo
Baadhi
ya wafungwa wakiume wa Gereza Kuu Butimba walionufaika na Msamaha wa Rais
wakitoka katika lango la Gereza Kuu Butimba tayari kwenda kuungana na familia
zao. Wafungwa hao wamemshukru Rais Magufuli kwa msamaha huo wa kihistoria.
Wafungwa
wa kike Gereza Kuu Butimba – Sehemu ya Wanawake wakitoka gerezani baada ya
Msamaha wa Rais alioutoa jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru. Wafungwa
hao wamemshukru Rais Magufuli kwa msamaha huo na wameahidi kutokurejea katika
uhalifu.
Kamati
ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mwanza pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
wakishuhudia wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais katika Gereza Kuu Butimba
wakipewa mali zao na nauli ya kwenda kuungana na familia zao Desemba 10,
2019 kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa husika wa msamaha huo.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike akitoa taarifa fupi ya
zoezi zima la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais katika
mikoa mbalimbali nchini mbele ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari
jijini Mwanza Desemba 10, 2019.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo akizungumza na Wafungwa wa Gereza Kuu Butimba
kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais Desemba 10, 2019. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP
- Phaustine Kasike.
(Picha
zote na Jeshi la Magereza).
Tuesday, December 10, 2019
Monday, November 18, 2019
CGP KASIKE AFANYA MAZUNGUMZO NA RC. MNYETI KABLA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI MANYARA
3:42 PM
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akitambulisha
ujumbe alioambatanao kabla ya mazungumzo mafupi na na Mkuu wa Mkoa wa Manyara,
Mhe. Alexander Mnyeti alipomtembelea Ofisini kwake kabla ya kuendelea na ziara
yake ya kikazi Gereza Mbulu, leo Novemba 18, 2019. Mkuu huyo wa Jeshi la
Magereza amehitimisha ziara yake leo ya siku tatu Mkoani Manyara ambapo
ametembelea magereza na Kambi zote za magereza mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza na Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipotembelea
Ofisini kwake leo Novemba 18, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akiteta jambo
na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti alipomtembelea Ofisi kwake
leo kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Gereza Mbulu, leo Novemba 18,
2019.
Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini - CGP Phaustine Kasike(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Mbulu,
SP. Danson Mpinga alipowasili Gereza Mbulu leo kwa ziara ya kikazi. Mkuu huyo
wa Jeshi la Magereza amehitimisha ziara yake leo ya siku tatu Mkoani Manyara
ambapo ametembelea magereza na Kambi zote za magereza mkoani humo.
Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini - CGP Phaustine Kasike akizungumza na wafungwa na mahabusu wa Gereza
Mbulu(hawapo pichani) leo Novemba 18, 2019 alipofanya ziara ya kikazi katika
gereza hilo(Picha zote na Jeshi la Magereza).
KAMBI YA MAGEREZA KATESH YAPEWA LENGO LA KULISHA MAGEREZA YOTE YA MKOA WA MANYARA
8:04 AM
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike(kushoto) akikagua
maandalizi ya awali ya shamba la mahindi alipofanya ziara ya kikazi Novemba
17, 2019 katika Kambi ya Magereza – Katesh iliyopo wilayani Hanang, Mkoa wa
Manyara. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Manyara, ACP. Lipina Lyimo.
Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akikagua moja ya trekta
linalotumika kwa shughuli za Kilimo katika Kambi ya Magereza – Katesh iliyopo
wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara, Novemba 17, 2019 alipotembelea Kambi
hiyo.
Moja ya maghala ya
kuhifadhia mazao mbalimbali yanayozalishwa katika Kambi ya Magereza – Katesh
iliyopo wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara.
Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua mradi wa tofali za saruji ambazo
zinafyatuliwa katika Gereza la Babati tayari kwa ujenzi wa nyumba za Maafisa na
askari wa kituo hicho.(Picha zote na Jeshi la Magereza).
Thursday, November 14, 2019
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AKAGUA UJENZI WA MAKAZI YA MAOFISA MAGEREZA UKONGA, APONGEZA HATUA KUBWA ILIYOFIKIWA TAREHE 13 NOVEMBA,2019
8:32 AM
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa SUMAJKT pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza
alipowasili katika eneo la ujenzi Gereza Kuu Ukonga Novemba 13, 2019 katika
ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua ujenzi unaoendelea wa makazi ya
Maafisa na askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, jijini Dar es
Salaam.
Ofisa wa SUMAJKT, Meja Ashrafu Hassan akitoa taarifa fupi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
alipotembelea Novemba 13, 2019 kwa lengo la kukagua ujenzi huo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike akikagua ujenzi wa majengo mbalimbali ya makazi ya Maafisa na Askari wa
Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga. Kulia kwake ni Ofisa wa
SUMAJKT, Meja Ashrafu Hassan akimuonesha baadhi ya maeneo ambayo bado
yanafanyia maboresho ya miundombinu.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua miundombinu ya mitaro ya
kupitishia maji ya mvua katika ujenzi wa majengo mbalimbali za makazi ya
Maafisa na Askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga.
Moja ya majengo ya ghorofa yaliyojengwa kwa ajili ya
makazi ya Maafisa na askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga,
jijini Dar es Salaam yakiwa tayari yamekamilika kama inavyoonekana katika picha (Picha na Jeshi la Magereza).
Thursday, November 7, 2019
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA MRADI WA KOKOTO GEREZA MSALATO, MKOANI DODOMA
4:38 PM
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiongea na Wafungwa wa Gereza
Msalato(hawapo pichani) wanaofanya kazi za uzalishaji kokoto katika mradi huo
wa Gereza hilo. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Keneth Mwambije.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike akikagua moja ya eneo la kulipulia mawe ya kokoto katika eneo la Gereza
Msalato leo alipofanya ziara ya kikazi.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike(aliyevaa miwani) akiangalia mtambo wa uzalishaji katika mradi wa
uzalishaji kokoto wa Gereza Msalato, Dodoma leo alipofanya ziara ya kikazi. Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA) limewekeza
mradi huo wa kokoto katika eneo
la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiangalia kokoto zinazozalishwa katika mradi huo wa Gereza
Msalato leo alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani
Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije na Kulia ni Mkuu wa
Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Huruma Mwalyaje.
Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Huruma Mwalyaje(katikati) akimwelezea jambo Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) kabla ya kutembelea eneo la mradi wa
uzalishaji kokoto. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi
wa Magereza, Keneth Mwambije (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Wednesday, November 6, 2019
SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE, LEO JIJINI DODOMA
2:49 PM
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto)
akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike akisaini kitabu cha Wageni
alipomtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Job
Ndugai(hayupo pichani), leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni,
Jijini Dodoma kwa mazungumzo maalum.
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Job Ndugai (kushoto) akiagana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike mara baada ya mazungumzo alipomtembelea leo
Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma.
Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth
Mwambije (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Friday, October 25, 2019
SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA PILI KATIKA JESHI LA MAGEREZA ZAFANA MKOANI MOROGORO
5:31 PM
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akikagua Paredi Maalum lililoandaliwa
na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza lililofanyika
Oktoba 25, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani
Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akiwa katika jukwaa
akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa
Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).
Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi
Wasaidizi wa Magereza wakipita mbele ya
Mgeni rasmi katika Sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya
Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP Phaustine Kasike(kushoto) akimvisha cheo cha
Mkaguzi Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi
Wasaidizi wa Magereza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika
kwa muda wa miezi minne.
Baadhi
ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa
Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza wakiwa tayari wamevishwa vyeo
vipya kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP Phaustine Kasike akitoa hotuba fupi kwa
Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya
mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
Mhitimu wa Mafunzo ya Maafisa
Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa
Magereza waliosimama mstari wa nyuma(Picha
zote na Jeshi la Magereza).
Thursday, October 17, 2019
“Zingatieni Maadili ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yenu” – CGP Kasike
12:33 AM
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza
na Maafisa na askari wa Gereza Namajani lililopo Wilayani Masasi, Oktoba 16,
2019 alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara.
Baadhi
ya askari wa Gereza Namajani wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini,
Phaustine Kasike
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
akizungumza na Maafisa na askari wa Gereza Masasi, Oktoba 16, 2019
alipotembelea katika ziara yake ya
kikazi.
Mkuu wa Gereza Masasi, Mrakibu wa Magereza, Juma Mkumba
akitoa taarifa fupi ya Gereza mbele ya
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) alipotembelea Gereza hilo.
Kamishna Jenerali Phaustine Kasike akikagua Mifugo Katika Gereza la Wilaya Masasi.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na askari wa Gereza Namajani alipotembelea leo Oktoba 16, 2019 katika
ziara yake ya kikazi. Kulia ni Mkuu wa
Magereza Mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Varisanga Msuya(Picha zote
na Jeshi la Magereza).
Wednesday, October 16, 2019
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA LA WILAYA RUANGWA, LINDI TAREHE 15 OKTOBA 2019
11:15 AM
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike, akisalimiana na Msaidizi wa Mkuu wa Gereza
Ruangwa, Mkaguzi wa Magereza, Alex Munga’nzo alipowasili Oktoba 15, 2019 kwa
ziara ya kikazi Gerezani hapo.
Mkuu
wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Josephine
Semwenda(kushoto) akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Magereza Mkoani Lindi mbele ya Kamishna
Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(meza kuu) alipowasili Gereza Ruangwa Oktoba 15, 2019.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua korosho ambayo tayari
imeanza kuvunwa katika mashamba mbalimbali ya Gereza Ruangwa, lililopo Mkoani
Lindi.
Ujenzi
wa jengo litakalotumika kwa ajili ya mapokezi ya ndugu na jamaa wa wafungwa na
mahabusu wanaofika Gereza Ruangwa kuwatembelea ndugu zao ukiendelea katika
hatua mbalimbali za ujenzi.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Idara ya
Uhamiaji nchini, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala walipokutana
leo Wilayani Ruangwa ziarani (Picha zote
na Jeshi la Magereza).