Monday, December 23, 2019

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE AHIMIZA WAFUASI WAKE KUZINGATIA NIDHAMU JESHINI

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike akizungumza katika kikao na Maafisa na askari wa vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es Salaam ambapo kikao hicho kilijadili masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya utendaji kazi, maadili ya kazi, nidhamu na mikakati mbalimbali ya Jeshi ikiwemo ya Kilimo, viwanda na ufugaji. Kikao kazi hicho kimefanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani) kikao hicho kilijadili masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya utendaji kazi, maadili ya kazi, nidhamu na mikakati mbalimbali ya Jeshi ikiwemo ya Kilimo, viwanda na ufugaji.

Askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Magereza kutoka katika vituo vya Magereza Mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya kikao kazi na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike Desemba 20, 2019 (Picha zote na Jeshi la Magereza).