Wednesday, December 11, 2019

WAFUNGWA 79 WA GEREZA KUU BUTIMBA WALIONUFAIKA NA MSAMAHA WA RAIS WAACHILIWA JIJINI MWANZA TAREHE 10 DISEMBA 2019

Mfungwa mnufaika wa Msamaha wa Rais, William Dingu akizungumza na Wanahabari(hawapo pichani) baada ya kuachiliwa huru leo. Mfungwa huyo amemshukru Rais kwa msamha huo, aidha,  amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kumwezesha ujuzi wa wa fani ya ujenzi ambao ameupatia gerezani kupitia programu ya Urekebishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo

Baadhi ya wafungwa wakiume wa Gereza Kuu Butimba walionufaika na Msamaha wa Rais wakitoka katika lango la Gereza Kuu Butimba tayari kwenda kuungana na familia zao. Wafungwa hao wamemshukru Rais Magufuli kwa msamaha huo wa kihistoria.


Wafungwa wa kike Gereza Kuu Butimba – Sehemu ya Wanawake wakitoka gerezani baada ya Msamaha wa Rais alioutoa jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru. Wafungwa hao wamemshukru Rais Magufuli kwa msamaha huo na wameahidi kutokurejea katika uhalifu.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mwanza pamoja na Kamishna  Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike wakishuhudia wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais katika Gereza Kuu Butimba wakipewa mali zao na nauli ya kwenda kuungana na familia zao  Desemba 10, 2019 kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa husika wa msamaha huo.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike akitoa taarifa fupi ya zoezi zima la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais katika mikoa mbalimbali nchini mbele ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari jijini Mwanza  Desemba 10, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo akizungumza na Wafungwa wa Gereza Kuu Butimba kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais  Desemba 10, 2019. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike.
(Picha zote na Jeshi la Magereza).