Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, September 23, 2016

SHEREHE ZA KUWAAGA WAASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA ZAFANA JIJINI DAR

Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipunga mikono ikiwa ni ishara ya kuwaaga Wastaafu hao wakati wakipita katika magari Maalum (hawapo pichani).
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akipita kwenye gari Maalum akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuwaaga Watumishi wa Jeshi la Magereza baada ya kustaafu rasmi Utumishi wa Umma kwa mujibu wa Sheria.

Wastaafu wa Jeshi la Magereza wakiwasili katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga, Dar es Salaam wakiwa wameongozwa na Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile wakielekea Jukwaa Kuu kupokea Salaam ya Heshima. Hafla ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi la Magereza imefanyika leo Septemba 23, 2016.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa katika Jukwaa Kuu akipokea Salaam ya Heshima kutoka kwenye Gwaride Maalum la kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akikagua Gwaride Maalum la kuwaaga Wastafu wa Jeshi la Magereza lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza.
 Gwaride Maalum likipita mbele ya Jukwaa kwa Heshima.
Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakipiga Saluti wakati Gwaride Maalum likipita mbele ya Jukwaa kwa heshima. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa pamoja na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakitoa Salaam za mwisho wakiwa kwenye magari wakati Gwaride Maalum likiwa limeunda Umbo la OMEGA.
Kamishna Mstaafu  wa Magereza Deonice Chamulesile(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Tuesday, September 20, 2016

GEREZA LA WILAYA TUKUYU MAHIRI KWA KILIMO CHA CHAI MKOANI MBEYA

 Mkuu wa Gereza Tukuyu, Mkoani Mbeya, SSP. Prosper Kinyaga akionesha  sehemu ya  eneo lenye ekari 26  linaloendesha Kilimo cha chai katika gereza hilo.
Wafungwa wa Gereza Tukuyu, Mkoani Mbeya  wakivuna chai katika Shamba la Gereza hilo kama inavyoonekana katika picha.
Muonekano wa baadhi ya mashamba ya Kilimo cha chai katika Gereza Tukuyu. Gereza hilo lilijengwa mwaka 1944 na shughuli zinazofanyika ni Kilimo cha chai, Kilimo cha Migomba, Bustani za mbogamboga pamoja na Utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti na ufugaji wa samaki kwa majaribio(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Friday, September 16, 2016

SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA KOZI NA. 22 ZAFANA CHUO CHA MAGEREZA, TUKUYU MKOANI MBEYA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(katikati) katika Jukwaa akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016(hawapo pichani) katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo leo Septemba 16, 2016 Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya.  Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akimvisha cheo cha Koplo wa Jeshi la Magereza Askari Mhitimu wa Mafunzo hayo kwa niaba ya wenzake.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kushoto) katika jukwaa kuu na Mgeni rasmi wakifuatilia maonesho mbalimbali ya kujihami askari kama wanavyoonekana katika picha.
Gwaride la Wahitimu likipita mbele ya jukwaa kwa heshima
Onesho la kijasiri kama inavyoonekana katika picha ambapo mwendesha pikipiki ameweza kupita kwa juu usawa wa tumbo huku askari hao wakiwa wamejilaza chini bila uoga.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wkichukua matukio mbalimbali kutoka Uwanja wa gwaride kama wanavyoonekana.
Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016 wakishangilia kwa makofi mara baada ya kufungwa rasmi mafunzo hay oleo Septemba 16, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba yake ya kufunga rasmi kwa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza katika Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Thursday, September 15, 2016

MEJA JENERALI RWEGASIRA KUFUNGA RASMI MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA CHUO CHA MAGEREZA, KIWIRA - MBEYA


Tarehe 16 Septemba, 2016 saa 3:00 asubuhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(pichani) anatarajia kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza Chuo cha Magereza Kiwira, Tukuyu – Mbeya.

Mafunzo hayo yalilenga kuwaandaa askari hao kuwa viongozi wasimamizi wa kazi za kila siku zinazopaswa kufanywa na viongozi wa ngazi hiyo Magerezani.

Sherehe hizo zitajumuisha mambo yafuatayo :-
i.    Mgeni rasmi kukagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na wahitimu hao;
ii.    Mgeni rasmi kutoa vyeti vya sifa kwa wanafunzi waliofanya vizuri na kumvisha cheo mwanafunzi mmoja kwa niaba ya wahitimu wengine na;
iii.   Mgeni rasmi kutoa hotuba.

Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zinatarajia kukamilika saa 8:00 mchana. Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye sherehe hizo tarehe 16 Septemba, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi.


Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
15 Septemba, 2016.

Friday, September 2, 2016

CGP - JOHN MINJA AMVISHA CHEO CHA KAMISHNA MSAIDIZI AFISA MWANDAMIZI WA MAGEREZA ALIYEKUWA AKIHUDUMU KATIKA MAANDALIZI YA PROGRAMU ZA MAGEREZA NCHINI NAMIBIA

Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akimvisha cheo cha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Afisa Mwandamizi wa Magereza, Gideon Matani ambaye alikuwa Nchini Namibia kwa jukumu la kuandaa Pogramu za Mafunzo ya Uendeshaji wa Magereza wa nchi hiyo kwa muda wa miaka miwili mfululizo. Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 3, 2016 Makao Makuu ya Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Makamishna wa Magereza wakifuatilia zoezi la uvishaji cheo hicho kwa  Afisa Mwandamizi wa Magereza, Gideon Matanicha  ambaye alikuwa Nchini Namibia kwa jukumu la kuandaa Pogramu za Mafunzo ya Uendeshaji wa Magereza wa nchi hiyo(kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akimvisha Kofia ya cheo cha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Afisa Mwandamizi wa Magereza, Gideon Matani.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Magereza baada ya zoezi la uvishaji Cheo kwa Kamishna Msaidizi wa Magereza, Gideon Matani

(Picha zote na Lucas Mboje wa Magereza).