Thursday, September 15, 2016

MEJA JENERALI RWEGASIRA KUFUNGA RASMI MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA CHUO CHA MAGEREZA, KIWIRA - MBEYA


Tarehe 16 Septemba, 2016 saa 3:00 asubuhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(pichani) anatarajia kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza Chuo cha Magereza Kiwira, Tukuyu – Mbeya.

Mafunzo hayo yalilenga kuwaandaa askari hao kuwa viongozi wasimamizi wa kazi za kila siku zinazopaswa kufanywa na viongozi wa ngazi hiyo Magerezani.

Sherehe hizo zitajumuisha mambo yafuatayo :-
i.    Mgeni rasmi kukagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na wahitimu hao;
ii.    Mgeni rasmi kutoa vyeti vya sifa kwa wanafunzi waliofanya vizuri na kumvisha cheo mwanafunzi mmoja kwa niaba ya wahitimu wengine na;
iii.   Mgeni rasmi kutoa hotuba.

Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zinatarajia kukamilika saa 8:00 mchana. Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye sherehe hizo tarehe 16 Septemba, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi.


Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
15 Septemba, 2016.