Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Monday, August 31, 2015

Kamishna Jenerali wa Magereza ashiriki hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa makao makuu ya ulinzi wa Taifa, Lugalo jijini Dar

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba fupi kwenye hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Lugalo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2015.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Lugalo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2015.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ramani/mchoro wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Lugalo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2015(kushoto) ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange.

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange akitoa maelezo mafupi ya mradi huo wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Lugalo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2015 kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi(hayupo pichani).
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Jumbe Mangu kwenye hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Lugalo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2015.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
 Baadhi ya Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakifuatilia kwa umakini mkubwa hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama  kwenye hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Lugalo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange(wa nne kulia) walioketi. wa pili kulia waliosimama) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(wa tatu kulia waliosimama) ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Jumbe Mangu na wa kwanza kulia ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile.

Saturday, August 15, 2015

Waziri Mkuu Mizengo Pinda afunga rasmi mafunzo ya uongozi daraja la kwanza chuo cha Magereza Kiwira, mkoani Mbeya

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda(katikati) akipokea Salaam kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kwa Askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akikagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Daraja la kwanza akiongozwa na Kamanda wa Gwaride. Sherehe hizo zimefanyika leo Agosti 15, 2015 katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akitoa cheti cha sifa kwa Mwanafunzi Mhitimu wa Mafunzo hayo, Wdr. Raymond Mgosso ambaye amefanya vizuri masomo ya Darasani(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwa jukwaani akifuatilia kwa makini Onesho Maalum la zoezi la kujihami(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
 Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la kwanza likipita mbele ya Jukwaa kutoa heshima kwa Mgeni rasmi kwa mwendo wa haraka.
 Askari wa Kike ambao wamehitimu Mafunzo hayo wakionesha zoezi la kujihami(Self Defence).
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hafla ya kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akiongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) kuelekea kwenye Ukumbi wa Chuo cha Magereza Kiwira kwenye hafla ya kufunga Mafunzo hayo(wa kwanza kushoto) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza(wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(wa tatu kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)

Thursday, August 13, 2015

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda kufunga mafunzo ya uongozi daraja la kwanza chuo cha magereza Kiwira, Mbeya

WAZIRI MKUU MIZENGO PETER PINDA

Bofya hapa kupata taarifa kamili

Saturday, August 8, 2015

Jeshi la Magereza laibuka mshindi wa jumla maonesho ya wakulima nane nane kikanda taasisi za majeshi ya ulinzi na usalama

Jeshi la Magereza nchini limeibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika Kanda ya Kasikazini(Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Kanda ya Mashariki(Mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga na Dar es Salaam) pamoja na Kanda ya Magharibi(Mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga) ambapo Jeshi la Magereza limeibuka kidedea katika upande wa Uzalishaji Taasisi za Serikali pamoja na Taasisi za Serikali upande wa Teknolojia na Maonesho Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi likiwa na jukumu lake la kuwahifadhi na kuwarekebisha Wafungwa wa aina mbalimbali wawapo Magerezani ili pindi wamalizapo vifungo vyao waweze kuwa raia wema katika jamii. Pia hushiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa na Kikanda kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kupitia shughuli zake mbalimbali za uzalishaji katika Sekta za Kilimo na Mifugo.

Mbali na ushindi huo wa Kikanda, Jeshi la Magereza limeshiriki kikamilifu katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Kitaifa(Maarufu kama Nane Nane) katika Mkoa wa Lindi ambapo Jeshi hilo limeibuka Mshindi wa Pili kwa upande wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Kilele cha Maonesho hayo huku Jeshi la Kujenga Taifa likibuka Mshindi wa Kwanza wa Jumla na Mgeni rasmi katika Kilele cha Maonesho hayo Kitaifa alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kutokana na Ushindi huo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja amewapongeza Maafisa na Askari wote walioshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo hadi kufanikisha ushindi huo na amewapa changamoto ya kuongeza bidii zaidi katika utendaji wao wa majukumu ya kazi ili katika Maonesho yajayo waweze kufanya vizuri zaidi.

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Jeshi la Magereza kuibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kikanda hapa nchini tangu Mwaka 2013. Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa yamefunguliwa rasmi Agosti 04, 2015 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Matokeo Makubwa Sasa" - Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Wakulima na Wafugaji.

Imetolewa na Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Agosti 08, 2015.

Friday, August 7, 2015

Mazishi ya SACP Aneth Laurent Balibusha

 Marehemu Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Aneth Laurent Balibusha
 Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa kwanza kulia), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Lufunga (wa pili) na Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga (wa tatu kulia) wakibadilisha mawazo nyumbani kwa marehemu eneo la Segerea, Dar es salaam.
 Mwili wa Marehemu Kamanda Aneth ukibebwa kuingizwa  kwenye gari maalum kwa ajili ya kupelekwa Kanisani
 Mwili wa Marehemu SACP Aneth ukiwasili katika viwanja vya  Kanisa Katoliki Jimbo la Segerea kwa ajili ya kuombewa kabla ya kupelekwa Makaburini.
 Makamanda wakiusindikiza Mwili wa Marehemu Altareni kwa ajili ya kuombewa.
 Baadhi ya Wanafamilia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Marehemu Kamanda Aneth wakiwa Kanisani wakifuatilia Misa Takatifu.
 Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa kwanza kulia)  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh.Ally Rufunga (aliyevaa miwani) na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakhim Maswi (wa tatu kulia) wakifuatilia Misa ya kumuombea Marehemu Kamanda Aneth Balibusha.
 Sehemu ya viongozi mbalimbali wa Jeshi la Magereza wakifuatilia Misa Takatifu ya kumuombea Marehemu Kamanda Aneth.
Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika ibada maalum ya kumuombea Marehemu. Kutoka kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Dkt. Juma Malewa, Kamishna wa Fedha na Utawala Gaston Sanga, RPO-Mwanza ACP Gorea, RPO-Morogoro SACP Dkt.Katto na RPO-Arusha SACP Nkubasi 
 Paroko Msaidizi wa Parokia ya Segerea Padre Josephat Mmbaga akiubariki mwili wa marehemu Kamanda Aneth Balibusha.
 Paroko Msaidizi wa Parokia ya Segerea Padre Josephat Mmbaga akinyunyuzia maji ya Baraka Mwili wa Marehemu.
Naibu Kamishna wa Magereza Edith Malya akitoa salamu za Jeshi la Magereza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza kwa ndugu na jamaa waliohudhuria Misa Takatifu kanisani hapo.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Rufunga akitoa salamu kwa niamba ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akitoa salamu za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa niamba ya  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Kasim Mkodo  kutoka Shinyanga akitoa salamu kwa niaba wa watumishi wa Magereza Mkoani Shinyanga.
 Naibu Kamishna wa Polisi DCP Nyamuhanga akitoa salamu za Jeshi la Polisi.
 Kamishna Mstaafu wa Huduma za Urekebishaji wa Magereza  Mama Aziza Sally akitoa salamu kwa niamba ya  Wastaafu wa Jeshi la Magereza lakini pia akiwa mtu aliyefanya kazi kwa muda mrefu na marehemu.
 Kamishna Mkuu Mstaafu, Afande Nicas Banzi akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwili wa Marehemu.
 Kamishna Jenerali Mstaafu, Afande Augustino Nanyaro akitoa salamu zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiongozwa na Kamishna Dkt Juma Malewa, Naibu Kamishna Edna Malya,  Kamishna Sanga na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mhandisi Kaluvya  wakipita mbele ya Jeneza kutoa heshima zao za mwisho.


 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama  aliye pia  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Ally Rufunga, Kamishna Jenerali John Minja na Eliakhim Maswi wakitoa heshima zao za Mwisho.
 Mfanyakazi wa Jeshi la Mgereza, Ndugu Magret Achwari akilia kwa uchungu wakati wa kuaga mwili wa Marehemu.
 Binti ya Marehemu Kamanda Aneth Bulisha akilia kwa majonzi makubwa wakati wa kumuaga mama yake.
 Baada ya Misa  takatifu ya kumuombea marehemu Msafara wa ndugu jamaa na marafiki ukielekea Makaburini.
 Mwili wa Marehemu Kamanda Aneth ukiwasili  Makaburi ya Segerea tayari kwa mazishi.
 Mwili wa Marehemu SACP  Aneth ukishushwa kaburini
 Paroko Msaidizi wa kanisa Katoliki Jimbo la Segerea Padri Josephat Mmbaga akibariki Kaburi la Marehemu Kamanda  Aneth baada ya mwili kuingizwa kaburini.
 Watoto  wa Marehemu Aneth wakiweka udongo kwenye kaburi kama ishara ya kumuaga mama yao.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mbaraka Abdulwakil akiweka udongo kaburini.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja akiweka udongo kwenye kaburi.
   Wajukuu wa marehemu wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi
 Katibu wa mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mbaraka Abdulwakil akiweka shada la maua kwenye kaburi.

Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja akiweka shada la maua kwenye kaburi.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Rufunga akiweka shada la maua kwenye kaburi.
 Mkuu wa Kikosi cha  Zimamoto Mkoa wa Shinyanga akiweka shada la maua kwenye kaburi.
 Kaburi la Marehemu Kamanda Aneth Bulisha likiwa limepambwa kwa mashada ya maua yaliyowekwa na ndugu, jamaa na marafiki.

Picha zifuatazo ni Gadi maalum ya Mazishi ya Jeshi la Magereza ikitoa heshima za mwisho mbele ya Kaburi la Marehemu Kamanda Aneth Balibusha.





Na ASP Deodatus Kazinja-Makao Makuu ya Magereza
Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Anneth Balibusha Laurent umeagwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Segerea  na kuzikwa katika makaburi ya Segerea Jijini Dar es Salaam jana tarehe 06 Agosti, 2015.

SACP Anneth aliugua ghafla tarehe 29 Julai, 2015  Mkoani Shinyanga na kulazwa katika hospatali ya Mkoa huo lakini hali yake iliendelea kubadilika hivyo ikawalazimu kupelekwa katika hospitali ya Rufaa Bungando Mkoani Mwanza kwa matibabu zaidi ambapo jioni ya tarehe 30 Julai, 2015 alifariki dunia.

Akitoa salaam za Jeshi la Magereza katika msiba huo,  Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Malya kwa niamba ya Kamishna Jenerali wa Magereza alisema Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla limempoteza mtu muhimu aliyekuwa na sifa za pekee katika utendaji kazi wake lakini pia limempoteza katika umri wake mdogo.

Alitoa pole kwa familia, watumishi wa Jeshi la Magereza, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga na kwa wote walioguswa na msiba huo. Pia aliitolea mwito familia ya marehemu kuwa wavumilifu katika kipindi hiki kigumu lakini pia kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana na familia hiyo kwa hali zote.

Aidha alisema kuwa Marehemu Anneth alikuwa miongoni mwa wanawake wachache wenye wadhifa wa Ukuu wa Magereza wa Mikoa hapa nchini ambapo jumla yao wako walikuwa wane tu na hivi sasa wamebaki watatu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Uslama wa Mkoa huo  Ally Nassro Lufunga alisema Kamati yake imempoteza mtu muhimu sana kwani alikuwa ni kiungo katika shughuli zao mkoani lakini pia marehemu alikuwa ameleta mwamko mpya katika vikundi vya akina mama na akiwa kiongozi wa vikundi vya mazoezi nyakati za jioni baada ya kazi. RC Lufunga aliongozana na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama katika kumzika mjumbe mwenzao.

Kwa upande wake mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa niaba ya Katibu Mkuu alisema Wizara imempoteza mtendaji makini, kwamba wao kama wizara walimtazama Marehemu Aneth kwa kuzingatia umri, elimu , jinsia yake na cheo alichokuwa nacho kama mtu ambaye angekuja kusaidia huko mbeleni katika ule mpango wa kurithishana madaraka. “sisi kiutumishi pale wizarani ni pigo kubwa hatuna jinsi ni mipango ya Mungu  itatubidi kujipanga upya, pole nyote” Alihitimisha

Marehemu Anneth Balibusha Laurent alizaliwa mwaka 1965 katika Kijiji cha Kibwera kata ya Kihanga Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Marehemu  alijunga na Jeshi la Magereza  tarehe 01 Septemba, 1994 akiwa ni Mhitimu wa  Shahada ya Kwanza ya Sanaa katika Uchumi na Mipango  katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM)

SACP Anneth tangu kuajiriwa kwake amekuwa Afisa Mipango Makao Makuu ya Magereza hadi Octoba 2013 alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga.