Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, February 28, 2020

WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA POLISI KUACHA KUZALISHA MAHABUSU MAGEREZANI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee(kulia) leo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe        katika Wizara hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani)leo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe katika Wizara hiyo. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee( Kulia )ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu, Uwesu Ngarama.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene(meza kuu katikati) kabla ya kuongea na Maafisa na askari wa Jeshin hilo. Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu, Uwesu Ngarama.

Baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, George Simbachawene (hayupo pichani).

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene(kulia) akitoa maelekezo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee(wa pili toka kushoto) leo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe katika Wizara hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene(Kaunda suti) akiingia Gereza Kuu la Isanga, jijini Dodoma, leo, tayari kwa kuzungumza na Wafungwa na Mahabusu waliopo katika Gereza hilo.


Wednesday, February 19, 2020

JESHI LA MAGEREZA KUJITEGEMEA KWA KUTUMIA RASILIMALI ZAKE

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akiongoza Kikao kazi cha siku moja cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza,  Kikao hicho kimefanyika leo Februari 19, 2020  katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakuu wa Magereza Mikoa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(hayupo pichani)katika Kikao kazi kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma.

Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Magereza, Uwesu Ngarama akitoa taarifa fupi katika Kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Sekretarieti wakifuatilia kikao kazi hicho kilichoongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza leo Februari 19, 2020 katika Ukumbi Chuo cha Mipango, jijini Dodoma         (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Friday, February 14, 2020

MAAFISA WASHIRIKI KUTOKA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA(NDC) WATEMBELEA KIWANDA CHA GEREZA KUU UKONGA JIJINI DSM

Mkufunzi Mwandamizi  wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Bregedia Jenerali  Cherestino Msolla (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga, ACP. Nsajigwa Mwankenja walipofanya ziara ya mafunzo katika Jeshi la Magereza Februari 12, 2020.

Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakitembelea sehemu mbalimbali katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.

Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakizungumza na mfungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani wa fani ya ushonaji katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.

Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakitoka  katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kuendelea na ziara yao ya mfunzo katika maeneo mbalimbali ya Jeshi la Magereza.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Magereza, SSP. Amina Kavirondo akiwasilisha andiko linalohusu majukumu ya Jeshi hilo mbele ya Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa             (hawapo pichani).

Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa mbalimbali nkuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza ikiwemo program za urekebishaji, Jijini Dar es Salaam.

Kikundi cha Askari wa Kikosi Maalum cha Magereza kikionesha onesho la ukakamavu mbele ya Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(NDC) walipotembelea Makao Makuu ya Kikosi hicho, jijini Dar es Salaam.

Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania wakiburudika na matunda ya madafu katika ziara yao ya mafunzo katika Jeshi la Magereza.

Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama(wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Washiriki waliotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jana(waliosimama mstari wa nyuma) kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(wa pili toka kushoto walioketi) ni Mkufunzi Mwandamizi  wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Bregedia Jenerali  Cherestino Msolla (kushoto) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremiah Katungu (Picha zote na Jeshi la Magereza).



Tuesday, February 11, 2020

MAAGIZO






#MAAGIZO - KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza, Suleiman Mzee amepiga marufuku mazoea ya baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi hilo kulima mashamba yao, kufuga mifugo katika mazizi yanayomilikiwa na Jeshi pamoja na matumizi binafsi ya nguvu kazi ya wafungwa. #MagerezaTz

Monday, February 10, 2020

CGP SULEIMAN MZEE AONGOZA KIKAO KAZI LEO CHA MAAFISA NA ASKARI MAGEREZA TOKA VITUO VYA KANDA YA DAR ESALAAM

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, ACP. Joel Matani kabla ya kikao kazi cha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka katika vituo vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam, leo Februari 10, 2020.

Kamishna wa Magereza anayeshughulika na Utawala na Rasilimali watu, Uwesu Ngarama akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(katikati meza kuu) kuzungumza katika kikao kazi cha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka katika vituo vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam, leo Februari 10, 2020.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akiongoza kikao kazi cha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka katika vituo vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam, leo Februari 10, 2020.

Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mkubwa maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza aliyoyatoa katika Kikao kazi cha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka katika vituo vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam leo.

   Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza, Kanda ya Dar es Salaam wakisikiliza maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee       (hayupo pichani) katika Kikao kazi hicho   (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Sunday, February 9, 2020

WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KIWANDA KIPYA CHA NGOZI KARANGA, MOSHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Uwekezaji) Jenista Mhagama (wa tatu toka kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Andrew Massawe (wa pili toka kushoto) wakiongozana na Makamanda Waandamizi wa Jeshi la Magereza Nchini wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi wa kiwanda cha Ngozi cha Karanga kinachojengwa kwa Ubia baina ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Gereza la Karanga lilolopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Februari 8, 2020.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Uwekezaji) Jenista Mhagama (wa pili toka kulia) akitoa maelekezo leo kwa watendaji mbalimbali Naibu Kamishna wa Magereza, Afwilile Mwakijungu(kushoto) ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi wa kiwanda cha Ngozi cha Karanga kinachojengwa kwa Ubia baina ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)
 na Jeshi la Magereza.

Moja ya majengo katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Ngozi cha Karanga kinachojengwa kwa Ubia baina ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Jeshi la Magereza likiwa limefikia hatua mbalimbali za ujenzi kama inavyoonekana katika picha. Jengo hilo litatumika kuhifadhia mashine ambazo tayari zimewasili bandarini

Mhandisi wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi, Mrakibu wa Magereza, Julius Sukambi (kulia) akisoma taarifa ya ujenzi mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Uwekezaji) Jenista Mhagama (kushoto).

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa majengo ya kiwanda hicho (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Wednesday, February 5, 2020

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, SULEIMAN MZEE AKAGUA USIMIKAJI WA MIUNDOMBINU YA MAJI KATIKA MAJENGO YA MAKAZI YA MAAFISA NA ASKARI MAGEREZA, UKONGA DSM

Kamishna  Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee akisalimiana na Mkuu wa Kiwanda cha Samani cha Gereza Kuu Ukonga, ACP. John Itambu mapema leo alipokagua zoezi la uwekaji miundombinu ya maji katika majengo ya makazi ya Maafisa na askari Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya kutembelea eneo la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi hilo.

Mkuu wa Magereza Mkoani Dar es Salaam, SACP. Julius Ntambala(kushoto) akitoa taarifa fupi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(wa pili toka kulia) mapema leo alipokagua zoezi la uwekaji miundombinu ya maji katika majengo ya makazi ya Maafisa na askari Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya kutembelea eneo la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi hilo.

 Moja ya majengo ya makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza yaliyopo Ukonga Dar es Salaam ambayo yamekabidhiwa hivi karibuni na Rais Magufuli.

Mkuu wa Magereza Mkoani Dar es Salaam, SACP. Julius Ntambala akitoa taarifa fupi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(wa pili toka kulia) mapema leo alipokagua zoezi la uwekaji miundombinu ya maji katika majengo ya makazi ya Maafisa na askari Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya kutembelea eneo la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi hilo (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Tuesday, February 4, 2020

NIPENI USHIRIKIANO - KAMISHNA JENERALI MPYA WA MAGEREZA, SULEIMAN MZEE

Na ASP Lucas Mboje, DSM
KAMISHNA Jenerali mpya wa Magereza nchini, Suleiman Mzee (pichani) amewataka Maofisa na askari wote wa Jeshi la Magereza kumpa ushirikiano katika uongozi wake ili aweze kusimamia vyema maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Jeshi hilo ikiwemo jukukumu la kujitegemea kwa chakula cha wafungwa magerezani.
Akizungumza na Maofisa, askari na watumishi raia wa Jeshi hilo katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Magereza, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa anayomatarajio makubwa ya kuhakikisha kuwa Jeshi la Magereza linakuwa na miradi mingi ya uzalishaji mali ili kuwezesha kujitegemea badala ya kutegemea bajeti kuu ya Serikali.
“Ni lazima tuzalishe kwa wingi na kila gereza lizalishe kulingana na fursa zilizopo ikiwa tunataka kujiwekea mazingira ya kuaminika. Pia, tuhakikishe kuwa utaalam wetu katika nyanja mbalimbali lazima uwe na manufaa Jeshini”, amesisitiza Jenerali Mzee.
Aidha, Kamishna Jenerali Mzee ameongeza kuwa ni vyema maofisa na askari wa Jeshi hilo wakazingatia utii, uaminifu pamoja na uhodari katika kazi ili kuyafikia matarajio hayo makubwa ndani ya Jeshi.
“Mkizingatia utii, uaminifu pamoja na uhadari katika kazi naamini matokeo chanya yataonekana katika muda mfupi kwani upo uwezekano wa kufanya mambo makubwa ambayo yataliletea heshima na sifa Jeshi letu la Magereza”, amesema Jenerali Mzee.
Kuhusu mafunzo mbalimbali kwa maafisa na askari, amesema kuwa atapitia mitaala ya mafunzo ili kuona kama inaendana na mazingira yaliyopo pamoja na kuifanyia maboresho mbalimbali kwani mafunzo ni nguzo muhimu katika kujenga nidhamu kwa maafisa na askari.
Kwa upande wake aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(sasa Balozi Mteule) alimpongeza Jenerali Mzee kwa kuteuliwa na Rais kushika nafasi hiyo na alibainisha baadhi ya changamoto ambazo zinalikabili Jeshi hilo ikiwemo uchakavu wa makazi ya askari.
“Nafurahi kuwa naliacha Jeshi la Magereza likiwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na kuwa na baadhi ya changamoto mbalimbali ikiwemo makazi duni ya askari, naamini changamoto hizo utazifanyia kazi kwani tayari tulikwishaanza kuchukua hatua”, amesema Mhe. Balozi Kasike.
Jeshi la Magereza linamiliki ardhi yenye ukubwa wa ekari 326,205 Tanzania Bara, kati ya hizo ekari 151,350 zinafaa kwa shughuli za kilimo na mifugo. Eneo linalotumika kwa shughuli za kilimo kwa sasa ni ekari 20,580 pekee sawa na asilimia 13.60 ya eneo linalofaa kwa shughuli za kilimo. Jeshi hilo likijipanga kimkakati linaweza kujilisha, kuongeza pato serikalini pamoja na kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo hapa nchini.

MAPOKEZI YA KAMISHNA JENERALI MPYA WA MAGEREZA OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA MAGEREZA, JIJINI DAR

Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akipokea salaam ya heshima toka  Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kwa ajili yake kwa heshima katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Magereza, Jijini             Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali  mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake kwa heshima kama inavyoonekana katika picha.

Kamishna Jenerali  mpya wa Magereza, Suleiman Mzee  akisalimiana na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (sasa Balozi mteule) alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo baada ya kuapishwa rasmi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020. Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Uwesu Ngarama.

Kamishna Jenerali  mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akifanya mahojiano maalum na wanahabari baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali  mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akiongea na Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020.

Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali mpya wa Ma gereza, Suleiman Mzee mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020                         (Picha zote na Jeshi la Magereza).