Monday, November 18, 2019

KAMBI YA MAGEREZA KATESH YAPEWA LENGO LA KULISHA MAGEREZA YOTE YA MKOA WA MANYARA

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike(kushoto) akikagua maandalizi ya awali ya shamba la mahindi alipofanya ziara ya kikazi  Novemba 17, 2019 katika Kambi ya Magereza – Katesh iliyopo wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Manyara, ACP. Lipina Lyimo.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akikagua moja ya trekta linalotumika kwa shughuli za Kilimo katika Kambi ya Magereza – Katesh iliyopo wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara, Novemba 17, 2019 alipotembelea Kambi hiyo.

Moja ya maghala ya kuhifadhia mazao mbalimbali yanayozalishwa katika Kambi ya Magereza – Katesh iliyopo wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua mradi wa tofali za saruji ambazo zinafyatuliwa katika Gereza la Babati tayari kwa ujenzi wa nyumba za Maafisa na askari wa kituo hicho.(Picha zote na Jeshi la Magereza).