Thursday, June 25, 2015

Wakuu wa Taasisi ya Magereza kutoka nchi za Afrika watembelea kiwanda cha viatu cha gereza kuu Karanga Moshi, mkoani Kilimanjaro

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Botswana, Silas Motlalekgosi akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wa Mkoani Kilimanjaro alipotembelea Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi leo Juni 25, 2015 akiwa na Viongozi Wakuu wa Taasisi za Urekebishaji/ Magereza kutoka Nchi za Swaziland, Uganda, Kenya, Zambia.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Swaziland, Isaya Ntshangase akisaini kitabu cha Wageni alipowasili katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Viongozi hao wa Magereza kutoka Nchi za Afrika wapo ziara ya kikazi nchini Tanzania.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile akitoa utambulisho kwa Ujumbe wa Viongozi wa Magereza kutoka Nchi za Afrika ambao wapo Nchini kwa ziara ya kikazi. Viongozi hao wametembelea Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi.
Wafungwa wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakiwa wanashona viatu aina ya Buti ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini kama wanavyoonekana katika picha wakishona sehemu ya juu ya viatu hivyo. Wafungwa hao wa Gereza Kuu Karanga wananufaika na Stadi ya Ushonaji viatu katika Kiwanda hicho kwa kujipatia ujuzi wa Ushonaji.
Muonekano wa viatu aina ya Buti vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi, viatu hivyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikiwa tayari vimekwishatengenezwa kama vinavyoonekana katika picha.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).