Friday, October 13, 2017

MAGEREZA YAPIGWA "JEKI" VIFAA TIBA au MAREKENI YAMWAGA VIFAA TIBA KWA MAGEREZA

Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkurugenzi, Ofisi ya Afya ya Shirika na Misaada la Marekani (USAID) Bi. Laurel Fain (wa pili kulia) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Gereza la Mahabusu Segerea tayari kwa hafla ya makabidhiano ya vifaa Tiba leo tarehe 13.10.2017
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akipokea hati ya makabidhiano ya Vifaa Tiba kutoka kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Afya ya Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bi. Laurel Fain katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika leo tarehe 13.10.2017 katika viawanja vya Gereza la Mahabusu Segerea Jijini Dar Es Salaam.
Mwonekano wa sehemu ya vifaa tiba vya aina tofauti tofauti vilivyokabidhbiwa leo kwa Jeshi la Magereza Tanzania Bara na Chuo cha Mafunzo Zanzibar kutoka serikali ya Marekeni kupitia Asasi ya JSI/AIDSFree. Vifaa hivyo vyenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 1.3 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 2 fedha za Kitanzania vitasambazwa katika Zahanati za Magereza nchini, Vyuo vya Mafunzo Zanzibar na hospitali Mpya ya Jeshi la Maagereza inayojengwa sasa eneo  la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Afisa Muuguzi Staff Sajin wa Magereza Recho Komakoma (kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) jinsi kitanda cha kisasa cha kujifungulia (delivery kit) kinavyofanya kazi. Kitanda hicho ni sehemu ya vifaa mbalimbali vya tiba vilivyokabidhiwa leo tahere 13.10.2017 kutoka Serikali ya Marekani kupitia USAID chini ya Mradi wa JSI/AIDSFree. Wa kwanza kulia ni Naibu Kamishna wa Mafunzo Zanzibar Haji Omar.
Mkaguzi wa Magereza Dr. Abdilatif Mkingule (kushoto) ambaye ni daktari kutoka Zahanati ya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga akitoa maelezo ya matumizi ya mashine ya uchunguzi (surgical microscope) wa magonjwa ya koo,pua masikio na macho  katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika leo tarehe 13.10.2017 katika viawanja vya Gereza la Mahabusu Segerea Jijini Dar Es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akiwahutubia wageni waalikwa pamoja na maofisa na askari wa Jeshi la Magereza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka serikali ya Marekani kupitia Asasi ya misaada ya USAID, JSI/AIDSFree iliyofanyika leo tarehe 13.10.2017 katika viwanja vya Gereza la Segerea jijini Dar es salaam. Kamishna Malewa alizishukuru serikali ya Marekani kupitia Asasi ya USAID, AIDSFree, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano wanaoutoa katika kuboresha huduma za Afya ndani ya Jeshi la Magereza.
Mkurugenzi Mkaazi wa JSI/AIDSFree Dr. Beati Mboya akitoa maneno mafupi ya ufunguzi katika hafla ya Makabidhiano ya vifaa tiba kwa Jeshi la Magereza na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar. Dr. Mboya Ameiambia hadhira kuwa Asasi yake imekuwa nchini Tanzania tangu mwaka 2015 ikivijengea uwezo vituo vya Afya katika Jeshi la Magereza na Polisi kwa kuimarisha ubora wa huduma zao hasa katika magonjwa ya Ukimwi na Kifua Kikuu.Kwamba walengwa ni wafanyakazi katika taasisi hizi, familia zao, wafungwa,mahabusu na jamii nzima inayozunguka maeneo hayo.
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza (hayupo picha) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka Serikali ya Marekani kupitia Asasi ya USAID JSI/AIDSFree. Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 13.10.2017 katika viwanja vya Gereza Segerea Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi,Ofisi Ya Afya Bi. Laurel Fain kutoka USAID akitoa hotuba katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa Tiba kwa Jeshi la Magereza kutoka Serikali ya Marekeni kwa Jeshi la Magereza nchini.
Baadhi ya askari wa gereza la Mahabusu Segerea waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhiana vifaa tiba kutoka serikali ya Marekani kupitia Asasi ya USAID JSI/AIDSFree iliyofanyika leo tarehe 13.10.2017 jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (katikati) katika picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa Asasi ya JSI/AIDSFree waliosimama. Waliokaa kutoka kuli ni Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama na Naibu Kamishna wa Mafunzo Haji Omar kutoka Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Mkaazi wa JSI/AIDSFree Dr. Beati Mboya na Mkurugenzi, Ofisi ya Afya wa USAID Bi. Laurel  Fain.