Saturday, January 10, 2015

Sherehe ya maofisa magereza kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015 yafana Jijini Dar

Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015. sherehe hiyo imefanyika Januari 9, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga, Jijini Dar s Salaam.
Makamanda na Wapiganaji wa Jeshi la Magereza wakiwa katika sherehe  ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015. sherehe hiyo imefanyika Januari 9, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga, Jijini Dar s Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(wa tatu kushoto) atoe hotuba yake (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Bw. Daud Msangi(wa pili kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa tatu kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. Dickson Mwaimu(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa) .
Maofisa wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni waalikwa wakipita mbele ya Mgeni rasmi kwa ajili ya kutosi glasi za vinywaji katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015.
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akikabidhi zawadi ya Luninga mmoja wa Maofisa wa Jeshi la Magereza ambaye ni Mhakiki wa Sanaa na Lugha Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Mrakibu wa Magereza, Rashid Mtimbe katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015.
Maofisa wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni waalikwa wakisakata rumba katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015.