Thursday, February 5, 2015

Kikao cha kwanza cha bodi ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji gereza Kigongoni-Bagamoyo kati ya shirika la Magereza na kampuni ya Tarbim chafanyika leo mjini Bagamoyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu akitoa maelezo mafupi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo(kushoto) ni Mjumbe wa Bodi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Green Park iliyoko Bagamoyo.
Wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji kutoka Jeshi la Magereza wakisikiliza maelezo ya utambulisho kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim Bw Baddal Calikusu (hayupo pichani)

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (aliyesimama) akitoa utambulisho kwa wajumbe wapya wa Bodi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo .
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana akiwa na Wajumbe wengine wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni wakikagua eneo la Mradi utakapotekelezwa.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni mara baada ya Kikao cha kwanza kilichofanyika katika Hoteli ya Green Park iliyopo Mjini Bagamoyo (wa kwanza kulia) ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana (wa tatu kulia) ni Mjumbe wa Bodi, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Masunga.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)