Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Tuesday, May 19, 2020

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AKUTANA NA MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA WALIOHAMISHIWA MAKAO MAKUU YA JESHI HILO DODOMA HIVI KARIBUNI

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akizungumza katika kikao kazi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wamehamishiwa hivi karibuni Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma. Kikao hicho kimefanyika leo Mei 19, 2020 kwa lengo la kupeana mikakati mbalimbali ya kazi sambamba na maelekezo ya utekelezaji wa mageuzi yanaendelea ndani ya Jeshi hilo.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(hayupo pichani)katika kikao kazi kilichofanyika leo Mei 19, 2020 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(meza kuu) akiwa na Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Mzee Nyamka(kushoto) wakifuatilia kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kilichofanyika leo Mei 19, 2020, Jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jeshi la Magereza, SACP. Boyd Mwambingu akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee mara baada ya kikao kazi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wamehamishiwa hivi karibuni Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Thursday, May 14, 2020

SERIKALI YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI BODI ZA PAROLE NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(Mb) akitoa hotuba katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole Taifa, leo Mei 14, 2020 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa Parole akitoa maelezo mafupi kuhusiana na utendaji kazi wa Bodi za Parole nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994. Leo Mei 14, 2020 katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole Taifa, katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Dkt. Augustino Mrema akisoma taarifa fupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi azindue Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma.

Mjumbe wa Bodi ya Taifa Parole, Mchungaji wa Kanisa la KKKT  Dodoma, Marco Kinyau akijitambulisha mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(Mb) kabla ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo.

Meza kuu wakifuatilia utambulisho wa wajumbe wapya wa Bodi ya Taifa Parole. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(kushoto) ni Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Augustino Mrema.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(meza kuu katikati aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Taifa Parole(waliosimama). Wa pili toka kulia aliyeketi meza kuu ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee (Wa pili toka kushoto aliyeketi meza kuu) ni Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Augustino Mrema.
 (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Friday, May 8, 2020

WAZIRI MAVUNDE AMWAGA MISAADA YA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORANA GEREZA KUU ISANGA, DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) leo Mei 8, 2020 alipofika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma kabla ya kukabidhi vifaa vya kujikinga na janga la corona katika Gereza Kuu Isanga Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (kushoto meza kuu) akizungumza jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (kulia) leo Mei 8, 2020 alipofika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma kabla ya kukabidhi vifaa vya kujikinga na janga la corona katika Gereza Kuu Isanga.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza nje ya Gereza akikabidhi vifaa vya kujikinga na janga la corona katika Gereza Kuu Isanga, jijini Dodoma. Mhe. Mavunde amekabidhi msaada uliojumuisha vifaa mbalimbali ikiwemo sabuni, ndoo za maji pamoja na  vitakasa mikono (Sanitizer).

Baadhi ya vifaa hivyo vilivyokabidhiwa katika Gereza Kuu Isanga na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.

Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, ACP. Keneth Mwambije akimshukru Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (kushoto) baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kujikinga na janga la corona.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee( wapili kushoto) akiagana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde mara baada ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma.                                              (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Monday, May 4, 2020

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, SULEIMAN MZEE AWAFUNDA WAKUU WA MAGEREZA ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI KUHAKIKISHA WANASIMAMIA AGENDA YA MABADILIKO NDANI YA JESHI LA MAGEREZA

Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee akitoa maelekezo maalum leo Mei 04, 2020 katika kikao kazi cha Maafisa wa Jeshi la Magereza walioteuliwa hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi hilo wakiwemo wakuu wa magereza, Boharia Mkuu wa Jeshi ambapo Jenerali Mzee amewataka kuhakikisha kuwa wanasimamia ipasavyo Agenda ya mabadiliko ndani ya Jeshi la Magereza.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akiwa meza kuu pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo akiwemo Kamishna wa Magereza anayeshughulika na Utawala na Rasilimali watu, Uwesu Ngarama (kulia). Kushotoni Kamishna wa Magereza anayesimamia Divisheni ya Urekebu, Mhandisi Tusekile Mwaisabila leo Mei 04, 2020 wakifuatilia kikao kazi cha Maafisa wa Jeshi la Magereza walioteuliwa hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi hilo wakiwemo wakuu wa magereza pamoja na Boharia Mkuu wa Jeshi hilo.

Baadhi ya Maafisa walioteuliwa kushika nyadhifa malimbali katika Jeshi la Magereza wakiwemo wakuu wa magereza wakifuatilia kikao kazi cha maelekezo ambacho kilikuwa chini ya Uenyekiti wa Kamishna Jenerali wa Magereza, leo Mei 04, 2020 jijini Dodoma .Jenerali Mzee amewataka kuhakikisha kuwa wanasimamia ipasavyo  Agenda yamabadiliko ndani ya Jeshi hilo.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee leo Mei 04, 2020 akizungumza na baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza walioteuliwa hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi hilo wakiwemo wakuu wa magereza , Boharia Mkuu wa Jeshi ambapo Jenerali Mzee amewataka kuhakikisha kuwa wanasimamia ipasavyo Agenda ya mabadiliko ndani ya Jeshi la Magereza.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akizungumza na Maafisa kutoka Vyuo vya Mafunzo Zanzibar (kulia) ambao wametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Tanzania Bara, leo Mei 04, 2020 jijini Dodoma. (Picha zote na Jeshi la Magereza).