Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, July 10, 2020

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI MEJ.JEN. SULEIMAN MZEE,TAR. 09 JULAI 2020, AMEFUNGUA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU YA JESHI LA MAGEREZA,KOZI NA.01 KATIKA CHUO CHA KPF KILICHOPO KINGOLWIRA , MOROGORO.

    Kamishna Jenerali Suleima Mzee akiongea na wanafunzi wa Kozi ya Uongozi Ngazi ya Juu( hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Chuo cha KPF Morogoro

Baadhi ya wanafunzi wa Kozi ya Uongozi Ngazi ya Juu wakimsikiliza Kamishna Jenerali Suleiman Mzee (hayupo pichani)

Baadhi ya wakufunzi wa Kozi ya Uongozi Ngazi ya Juu wakimsikiliza Kamishna Jenerali Suleiman Mzee (hayupo pichani)

Kamishna Jenerali Suleiman Mzee( wa pili toka kulia) akiangalia mradi wa choo cha kisasa kinachojengwa chuoni hapo. Wa pili toka kushoto ni Mkuu wa Chuo KPF, Kamishna Msaidizi wa Magereza Lazaro Nyanga

Mkuu wa Chuo cha KPF, Kamishna Msaidizi wa Magereza Lazaro Nyanga(kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali Suleiman Mzee moja ya miradi inayoendelezwa chuoni hapo. ( picha na Jeshi la Magereza)

Sunday, July 5, 2020

MAKATIBU MUHTASI JESHI LA MAGEREZA WAPIGWA MSASA TAREHE 04, JULAI 2020

Mgeni rasmi katika semina ya makatibu muhtasi wa jeshi la magereza (waliokaa kushoto) kamishna wa utawala na rasmali watu CP. Uwesu Hamidu Ngarama akiwa na wawezeshaji kutoka kikolo financial solution LTD, maafisa waandamizi wa jeshi la Magereza pamoja na washiriki wa semina Ya makatibu muhtasi.

Muwezeshaji Akitoa Mada wakati wa semina ya Makatibu Muhtasi wa Jeshi la Magereza waliokaa ni washiriki katika semina hiyo.


Pichani ni Sgt Scolastica Ndunguru akifafanua jambo wakatyi wa semina ya makatibu Muhtasi wa Jeshi la Magereza.

Picha ya Pamoja kati ya Washiriki wa semina hiyo na wawezeshaji pamoja na Viongozi waanzamizi wa Jeshi la Magereza.

Msemaji wa Jeshi la Magereza Ssp Amina Kavirondo akitoa Mada katika Semina ya makatibu muhtasi wa Jeshi la Magereza kushoto kwake ni Viongozi waandamizi wa Jeshi la Magereza. picha na Jeshi la Magereza