Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Friday, October 25, 2019

SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA PILI KATIKA JESHI LA MAGEREZA ZAFANA MKOANI MOROGORO

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akikagua Paredi Maalum lililoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza lililofanyika Oktoba 25, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akiwa katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).

Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza  wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika Sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP Phaustine Kasike(kushoto) akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa miezi minne.
Baadhi ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza wakiwa tayari wamevishwa vyeo vipya kama wanavyoonekana katika picha.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP Phaustine Kasike akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.

Mhitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza waliosimama mstari wa nyuma(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Thursday, October 17, 2019

“Zingatieni Maadili ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yenu” – CGP Kasike

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza na Maafisa na askari wa Gereza Namajani lililopo Wilayani Masasi,  Oktoba 16, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya  kikazi Mkoani Mtwara.

Baadhi ya askari wa Gereza Namajani wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza na Maafisa na askari wa Gereza Masasi, Oktoba 16, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya  kikazi.

Mkuu wa Gereza Masasi, Mrakibu wa Magereza, Juma Mkumba akitoa taarifa fupi ya Gereza  mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) alipotembelea Gereza hilo.

Kamishna Jenerali Phaustine Kasike akikagua Mifugo Katika Gereza la Wilaya Masasi.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na askari wa Gereza Namajani alipotembelea leo Oktoba 16, 2019 katika ziara yake ya  kikazi. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Varisanga Msuya(Picha zote na Jeshi la Magereza).


Wednesday, October 16, 2019

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA LA WILAYA RUANGWA, LINDI TAREHE 15 OKTOBA 2019

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike, akisalimiana na Msaidizi wa Mkuu wa Gereza Ruangwa, Mkaguzi wa Magereza, Alex Munga’nzo alipowasili  Oktoba 15, 2019 kwa ziara ya kikazi Gerezani hapo.

Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Josephine Semwenda(kushoto) akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Magereza Mkoani Lindi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(meza kuu) alipowasili Gereza Ruangwa  Oktoba 15, 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua korosho ambayo tayari imeanza kuvunwa katika mashamba mbalimbali ya Gereza Ruangwa, lililopo Mkoani Lindi.

Ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya mapokezi ya ndugu na jamaa wa wafungwa na mahabusu wanaofika Gereza Ruangwa kuwatembelea ndugu zao ukiendelea katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala walipokutana leo Wilayani Ruangwa ziarani (Picha zote na  Jeshi la Magereza).

Wednesday, October 9, 2019

“Simamieni wafungwa kutatua uhaba wa makazi ya askari” – CGP Kasike


Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akikagua matofali ya kuchoma katika mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma katika gereza la wilaya ya Mbozi alipotembelea hivi karibuni katika ziara yake ya  kikazi Mkoani Songwe.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua moja ya tanulu la matofali ya kuchoma katika mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma katika Kambi ya Mkwajuni  , Wilayani Songwe, leo Oktoba 8, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya  kikazi Mkoani Songwe.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiwasili jana Oktoba 7, 2019 katika ziara yake ya kikazi Gereza Ngwala.

  Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo leo Oktoba 8, 2019. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Songwe, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Lyazeck Mwaseba. (Picha na Jeshi la Magereza)


Na Mwandishi wetu, Songwe;  

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amewataka Wakuu wa magereza Tanzania Bara kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa jeshi hilo kote  nchini kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa waliopo magerezani.

Akizungumza Mkoani Songwe mara baada ya kukagua miradi ya ufyatuaji wa matofali ya kuchoma na ujenzi wa nyumba za maafisa na askari katika magereza ya Ileje, Mbozi, Ngwala na Kambi ya Mkwajuni iliyopo Mkoani Songwe,  Kamishna Jenerali Kasike amesema ujenzi wa makazi za askari unaoendelea katika vituo mbalimbali nchini ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli katika kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi wa Jeshi hilo.

 "Mkakati wa utatuaji wa changamoto ya uhaba wa nyumba za Maafisa na askari lazima utiliwe mkazo na kupewa kipaumbele katika kuwatumia wafungwa  waliopo magerezani katika suala la ujenzi sambambamba na uzalishaji wa chakula chakutosha ili kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wahalifu wote walipo magerezani, " alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Songwe kwa kuanzisha ujenzi wa Gereza jipya katika mji wa Mkwajuni ambao ni Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe.

Kamishna Jenerali Kasike amesema uwepo wa gereza hilo katika wilaya ya Songwe utasaidia katika kumaliza tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye gereza la wilaya ya Mbozi.

“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki hivyo nimpongeze sana Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa  pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa Gereza hili kimsingi utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza Mbozi,” amesema Jenerali Kasike.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Songwe. Mhe. Samwel Opulukwa ameshukru ujio wa Kamishna Jenerali katika ziara yake ya kikazi katika Gereza la Ngwala pamoja na Kambi ya Mkwajuni ili kujionea hali halisi ya Uendeshaji wa Jeshi hilo, Wilayani Songwe.

“Kamishna Jenerali nikuhakikishie tu kuwa Uongozi wa wilaya utashirikiana na Jeshi la Magereza katika kuhakikisha kuwa tunakamilisha ujenzi wa gereza hili jipya la Mkwajuni ili kusaidia kuondoa usumbufu wa wahalifu kwenda gereza la wilaya ya mbozi,” Alisistiza Mhe. Opulukwa.


Kwa sasa, wakazi wa wilaya hiyo ya Songwe ambao wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali au waliohukumiwa vifungo hupelekwa katika Gereza la wilaya ya Mbozi kitendo ambacho kinawanyima wafungwa na mahabusu fursa ya kuonana na ndugu au mawakili wao kutokana na umbali uliopo ambapo kutokana na juhudi za Mkuu wa Wilaya hiyo tayari Bweni moja la Wafungwa lenye uwezo wa kuhifadhi waha;lifu 150 limekamilika pamoja na Ofisi ya Utawala na ujenzi wa Ukuta wa gereza unaendelea katika Kambi hiyo ya Mkwajuni.